Shemeji yangu wa kike ni shabiki wa simba lia lia,humwambii kitu kuhusu hiyo timu
Tarehe 13 mwezi huu alikuwepo uwanja wa taifa kushuhudia ngao ya jamiii,mpira umekwisha yanga 2-1
Kwakuwa ni mtu wa majigambo na tambo nyingi,tukawa tunamsubiri kwa hamu arudi home tumshambulie kwa kejeli. ( sisi yanga)
Akawa harudi...tukampigia simu haipatikani,tukajua kwasabu timu yake imefungwa kaamua kuzima simu kwakuwa anakwepa utani wa jadi.
Kumbe bhana pikipiki aliyopanda iligongwa na gari maeneo ya kwa musuguri,walipoteza maisha palepale.
Kupata taarifa hata hatukuamini yani,shemeji yangu amekwenda kiutani namna hiyo,tumeumia sana.
Apumzike kwa amani