Maisha haya aisee, jana ilikuwa harusi leo imekuwa msiba

We acha tu yaani!! kwamba hata tufurukute tuna mwisho na ukiishi na miaka mingi ni mateso kwa nn tudharauliane? Hii dunia tu
 
Fumbo la maisha halina ufumbuzi
 
Dah,Mzee aliongea maneno yakufikirisha sana,maneno mazito sana, nimejisikia huzuni sana!Mungu ana siri nzito mno.
 
We acha tu yaani!! kwamba hata tufurukute tuna mwisho na ukiishi na miaka mingi ni mateso kwa nn tudharauliane? Hii dunia tu
Hatari sana, muhimu kuishi kwa upendo... Tukipata nafasi ya kufurahi unafurahi!
“Kisha nikaisifu furaha, kwa sababu mwanadamu hana neno lo lote lililo jema chini ya jua, kuliko kula, na kunywa, na kucheka; na yakuwa hilo likae naye katika amali yake, siku zote za maisha yake alizompa Mungu chini ya jua.

— Mhubiri 8:15
 
Dah,Mzee aliongea maneno yakufikirisha sana,maneno mazito sana, nimejisikia huzuni sana!Mungu ana siri nzito mno.
Tuishi kwa upendo! ndio maana Mhubiri anasema yote ni ubatili.
“Maana hakuna kumbukumbu la milele la mwenye hekima, wala la mpumbavu; kwa sababu siku zijazo wote pia watakuwa wamekwisha kusahauliwa. Na mwenye hekima, jinsi gani anavyokufa sawasawa na mpumbavu!

— Mhubiri 2:16
 
Maisha ni Fumbo,,Kuna ndugu yangu mwezi wa sita kafunga ndoa takatifu na tukasherehekea Kweli kweli,,jana usiku Amefariki..yani ndoa haijatoboa hata miezi miwili [emoji24][emoji24][emoji24]
 
Aisee

Kweli tuishi Ila tusimsahau muumba.wetu

Maisha ni tafakuri nzito yenye kujaa mafumbo na Siri

Wachache wanaijui siri hii
 
Mkuu poleni sana
 
Au unakuta anaiba mapesa na kuwapa mke na wanawe madaraka utadhani wataishi milele.
At the end wajukuu zake wanakuja kuwa masikini.Thus watawala wa kizungu wao waliona ni upumbavu kuiba madarakani ni SAwa na kujiibiia mwenyewe maana hata ukiiba zaidi labda watafaidi wanao je kizazi cha wanao je si kitaishia kuwa masikini,wao waliona jibu jepesi ni kuboresha maisha ya jamii nzima,yakiwa bora na vizazi vyao vitafaidi.Afrika mtu anaiiba pesa anaenda fadhili timu ya mpira kwa kodi zetu.
Mtu anapewa tenda ya kusambaza maji vijijini anazipiga kwa kushirikiana na watendaji kisha anaenda zifanyia biashara ya mabus huku Jamii ikiteseka na maji
 
Yeah!
Duniani tupo ili tuvunje sheria, duniani tupo ili tufanye dhambi.
Hapana. Ndugu yangu kwenye hii Dunia jitahid kuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Maisha ni mafupi sana Tena yamejaa taabu na shida
 
Hao wezi ndio hawakutaka kuona kiongozi anayehakikisha kila mtu ananufaika na miradi ya maendeleo.

Kwa ubinafsi wao wanaona ni sahihi kabisa na haki kwao kujilimbikizia mapesa ya wananchi wao na familia zao.

Ni jambo la kishetani mno kuwa na watu wa aina hii wenye tamaa iliyopitiliza ya pesa na mali.

Mtu yupo tayari kuona watu wanakosa barabara au hospital yenye vifaa na madawa lakini mwanae akasome ulaya na kutibiwa huko.
 
Pesa za wizi huwa hazitoshi,kadri upatavyo na ndivyo idadi ya vimada inaongezeka
 
Yaani haya maisha kama uwezo wa kula bata unao, wewe kula bata tu.
Mhubiri 8:8
Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie roho; Wala hana mamlaka juu ya siku ya kufa; Wala hakuna kuruhusiwa katika vita vile; Wala uovu hautamwokoa yule aliyeuzoea
 
Sayansi hapa inasema ulichagua kuishi, ktk sperm kuna mamilioni ya sijui chromosome/gene hushindana mbio kuingia kwenye yai la mwanamke, so mbio zako zilikuponza, make uliwazidi wale wengine milioni kadhaa.
 
Mwanao anaongea mantiki na wewe unaongea siasa , ati ecosystem balance! , aliyeeumba huo ulimwengu hakujua kwamba tutazaliana ? Alikuwa na kila kitu at disposal kwa nini aumbe kifo ?, shetani alikuwa na ulazima gani kuumbwa?: Kwan hata angeumba bao moja tu ndo litoe mtoto baada ya hapo yanayofuata ni kwa ajili ya burudani , mbona tungezaliana kwa wastani tu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…