Maisha haya! Nimetolewa vyombo nje na mwenye nyumba

Maisha haya! Nimetolewa vyombo nje na mwenye nyumba

alikupa notice ya miezi3? kama hapana vunja mlango urudishe vyombo ndani
Acha kumdanganya mwenzako. Aliyekwambia kuna huo utaratibu wa miezi mitatu ni nani?

Huo utaratibu ulikuwepo zamani wakati wa uhai wa sheria ya upangaji. Kwa sasa, kwa mujibu wa sheria ya ardhi ni kuwa endapo mwenye nyumba ataamua kusitisha mkataba basi atakupa notisi na siku zisizopungua 30. Hapo maana yake ni kuwa kama mkataba wako unaisha tarehe moja mwezi julai na mwenye nyumba hataki kuendelea kuwa na wewe atakutaarifu kabla ya mkataba wako kuisha na kukupa siku zisizozidi 30 baada ya huo mkataba kuisha ama atakurudishia kodi sawa na muda uliobaki na kukupa siku zisizozidi 30 uhame. Na baada ya siku hizo 30 basi anaweza kuamua kukutoa kwa nguvu nyumbani kwake.

Sasa vipi ikitokea mpangaji hajalipa kodi kama makubaliano yalivyo? Hapa mpangaji ndiye anakua amevunja mkataba hivyo anapaswa kuhama immediately na hatapewa fidia yoyote.
 
Amekusimulia kisa kizima hadi katolewa vitu vyake nje? Anadaiwa kodi ya miezi mingapi?
Wenye nyumba ni wavumilivu sana kwa mpangaji mkweli.
Sanaaa, mimi ninaungana na wewe katika hili. Hawa wenye nyumba ni wavumilivu na sisi wapangaji tumekua tukiwaonea sanaaa kisa tu sheria zimewabagua na hazijawalinda kama mpangaji anavyolindwa.
Utakuta mtu amekaa mahali bila kulipa kodi hata kwa miezi mitatu mfululizo lakini akitolewa lawama zi aelekezwa kwa mwenye nyumba, si sawa hata kidogo. Wenye nyumba wamekosa mtetezi.
 
Nimetolewa vyombo vyote nje sasa hivi mzee mwenye nyumba kashindwa kunielewa; amefungia vyeti, redio na vitu vyangu vya muhimu.

Hapa nataka niende kwa kiongnozi wa mtaa.
Ulimjibu vipi alipokuwa anakudai? Unaona amekuonea? Mwenye nyumba Nia mwanamke au mwanaume? Wewe umeajiriwa au umejiajiri? Ukienda serikali ya mtaa unataka kuwaambia nini?
 
Nimetolewa vyombo vyote nje sasa hivi mzee mwenye nyumba kashindwa kunielewa; amefungia vyeti, redio na vitu vyangu vya muhimu.

Hapa nataka niende kwa kiongnozi wa mtaa.
Ulijaribu kumueleza kiutu uzima, au ulikuwa unakimbia kimbia?
 
Kuna wakati mwingine kwenye maisha unabanwa!uchumi unakuwa mmbayaa
Hela ya chakula,kodi ya nyumba mtihani
Sasa kwq upande wa mwenye nyumba naye
Anataka hela,ili yeye aweze kuendelea na mambo yake
Mziki upo hapo

Ova
 
Amekusimulia kisa kizima hadi katolewa vitu vyake nje? Anadaiwa kodi ya miezi mingapi?
Wenye nyumba ni wavumilivu sana kwa mpangaji mkweli.
Kuna mmoja Mimi namdai Kodi ya miezi sita laki 6, ilikuwa laki nane kapunguza imebakia hiyo,
Yaan namfikiria simpatatii jibu,kingine tumetoka mbali, tangu mwaka 2019 yupo hapo kwenye banda langu, sometimes Ni hasara nyumba za kupangisha
 
Nyumba za kupangisha kuna majaribu kotekote.
Mara mia ujenge lodge, nilimpangisha mtu nyumba tena kwa bei sawa na bure, nyumba self, parking, maji, umeme, ina kuta hadi banda la mbwa la kisasa kwa bei ndogo sana kwani alilia kiwa korona imemuharibia uchumi, kama mwanaume nikamwelewa mwanaume mwenzangu.
Cha kushangaza mkataba ulipokaribia kuisha aliondoka bila kuniaga alihama usiku.
Majirani walinipigia simu kuwa wamehama na wameacha taa zinawaka usiku na mchana.
Baada ya siku 3 nikampigia hapokei wala hajibu sms.
Nilifanya kuingia kwa kuruka ukuta.
Ndani nilikuta uharibifu mkubwa sana wa zaidi ya 500,000 kurekebisha.

Nimeapa sitafanya tena ujinga huu wa kupsngisha bora ufanye lodge.
Kuna thread humu tunasema kila siku hii ni biashara kichaa! Inabidi uifanye kama unahifadhi hela benki tu,yaani badala ya kuweka benki unajenga, ila si biashara ya kukuinua kiviile. Ni mbeleni huko ukiwa mstaafu usikose hela ya mafuta na bia.
 
Kuna thread humu tunasema kila siku hii ni biashara kichaa! Inabidi uifanye kama unahifadhi hela benki tu,yaani badala ya kuweka benki unajenga, ila si biashara ya kukuinua kiviile. Ni mbeleni huko ukiwa mstaafu usikose hela ya mafuta na bia.
Kweli mkuu, sitarudia ujinga huu.
 
Nimetolewa vyombo vyote nje sasa hivi mzee mwenye nyumba kashindwa kunielewa; amefungia vyeti, redio na vitu vyangu vya muhimu.

Hapa nataka niende kwa kiongozi wa mtaa.

Long life baba mwenye nyumba. Lazima nyumba ya kupanga ukae Kwa muda si milele. Sasa jipange zaidi upate kiwanja Goba au Kinyerezi ukaweke hema
 
Basi tatizo sio mwenye nyumba
Shida iko kwako kwa kuona kufikisha iyo pesa ni ndoto.

uko radhi kua online kila siku lakini sio kutumia kila siku KuSave na upate uhakika wa malazi.

unless Kama uliandika Kama kichekesho tu!
Ni ngumu kuvaa viatu vya mwenzio, hata wale madogo wanaoosha vioo vya gari wanapambana ila kuna mtu aliwadharau nilijiskia vibaya! Yani kama vile wale hawana akili na kile walichoamua kufanya ili kujitaftia riziki! Sasa sijui walitakiwa washike bisibisi na kukaba watu vichochoroni
 
Mkubwa sasa imekuaje mpaka unatolewa usiku usiku,kwa nini hujamwambia asubirie kukuche ,halafu hivyo vyeti kavifungia vipi wakati vitu vyako vyote vimetolewa nje(na wewe ikiwemo)
 
Pole sana, Maisha haya tunapitia mengi sana.

Kuwa muwazi Kiongozi.

Je hukuwa unampiga kalenda?

Kwa mfano keshokutwa, wiki ijayo, baada ya wiki mbili, mpaka kufikia mwenye nyumba wako kukuchoka kwa ahadi zako usizozitimiza.

Uamuzi wa hivyo siyo wa siku moja, itakuwa alikuvumilia sana mpaka kufikia uvumilivu kumshindwa
Du wapangaji wasumbufu sana, mpangaji wangu ananipigia kalenda sana , Nataka nimwambie aame , Mana hata akiwa na ela analipa nusu nusu
 
Back
Top Bottom