African Geek
JF-Expert Member
- Jul 29, 2022
- 817
- 1,470
Bibilia imetiwa mkono wa binadamu. Yesu hakushushiwa bibilia. Sasa kwanini wakristo wanatumia bibiliaHizo Biblia zote zimeandikwa na binadamu kama wewe ndio maana kuna version za kuanzia Rome mpaka American, hadithi zote za kutunga na zimewekwa na binadamu kama wewe, hata babu yako angekuwa na uwezo angeweza kuandika bible yake na leo ikaonekana ndio neno la mungu, miaka 500 ijayo inawezekana kabisa ikaja bible nyingine iliyondikwa na mtu mwenye nguvu, amini tuu na wala hakuna makosa lakini za kupewa changanya na zako
Sasa unavocriticise usichanganye kati ya mfumo na matakwa ya watu. Nakumpa mfano mdogo science ni one of the best thing happen to a man after religion. Ila kupitia science hyo hyo kuna mambo yamefanyika ya kutisha moja wapo vita inayoendelea ukraine au pia corona na mambo kadha wa kadha lakini mbona hamuipondi science ila mnawaponda watu ila mtu akitumua dini kwa manufaa yake binafsi mnaponda dini that's unfair. Unatakiwa ulete kifungu kinachofirisi watu kwenye maandiko utaeleweka.Kanisa ni mimi na wewe kuna matukio mengi hayako sawa
Kwani malaika gibril nd alieandika quran mnayotumia leo mkuu?Bibilia imetiwa mkono wa binadamu. Yesu hakushushiwa bibilia. Sasa kwanini wakristo wanatumia bibilia
Hofu ni kitu kibaya sana....
Katika safari ya kujitambua mwanadamu hufikia kumjua Mwenyezi Mungu vyema kwa kuwa yupo.....
Kumjua Mwenyezi Mungu ni kumpenda yeye tu na wala si kwa sababu ya kuugopa moto ama kuogopa kuukosa ufalme wa mbingu(levels hizi hufikia wale wenye busara tu)....
Na ndio maana akina Rabia Basra walimuabudu Mungu kwa misimamo hiyo....na hawakuwa na "MBANGO" wala kuuishi ujinga wa wapuuzi wachache walio wanadini wenzao......
Vifungu vinakusaidia nini vifungu vinakufanya usiamshe ubongo waKo kufikiri zaidiSasa unavocriticise usichanganye kati ya mfumo na matakwa ya watu. Nakumpa mfano mdogo science ni one of the best thing happen to a man after religion. Ila kupitia science hyo hyo kuna mambo yamefanyika ya kutisha moja wapo vita inayoendelea ukraine au pia corona na mambo kadha wa kadha lakini mbona hamuipondi science ila mnawaponda watu ila mtu akitumua dini kwa manufaa yake binafsi mnaponda dini that's unfair. Unatakiwa ulete kifungu kinachofirisi watu kwenye maandiko utaeleweka.
Mkuu kwani BIBLIA ni nini?!!!Bibilia imetiwa mkono wa binadamu. Yesu hakushushiwa bibilia. Sasa kwanini wakristo wanatumia bibilia
Qur'an imeshushwa kwa njia ya mdomo. Mtume naye aliwafikishia wafuasi wake kwa njia ya mdomo. Qur'an ilianza kuhifadhiwa mioyoni mwa wafuasi mpaka hapo baadae ilipokusanywa kwa maandishi. Ndo mana mpaka leo licha ya Qur'an kuwepo kwa njia ya maandishi bado watu wanaitunza mioyoni mwao ndo mana ni ngumu sana kuibadilisha Qur'anKwani malaika gibril nd alieandika quran mnayotumia leo mkuu?
[emoji106]Sasa unavocriticise usichanganye kati ya mfumo na matakwa ya watu. Nakumpa mfano mdogo science ni one of the best thing happen to a man after religion. Ila kupitia science hyo hyo kuna mambo yamefanyika ya kutisha moja wapo vita inayoendelea ukraine au pia corona na mambo kadha wa kadha lakini mbona hamuipondi science ila mnawaponda watu ila mtu akitumua dini kwa manufaa yake binafsi mnaponda dini that's unfair. Unatakiwa ulete kifungu kinachofirisi watu kwenye maandiko utaeleweka.
Elezea ni kwa namna gani vifungu vinafanya mtu asiamshe ubongo. Maan bible inasema asiefanya kazi asile lete vinavyofanya mtu asijishughulishe. Halafu wewe unahisi watu wa dini hawajafanya mapinduzi ya technolojia sababu hujasikia wakizungumziwa katika bible maisha yao ya kawaida yalikuwaje na umekuwa brainwashed na hao wanaoandikwa maforbes lakini hujui katika safari zao wamepata maarifa kutoka kwa watu hata wa dini mbali mbali.Vifungu vinakusaidia nini vifungu vinakufanya usiamshe ubongo waKo kufikiri zaidi
Nini maana ya neno "dini"?Ukiangalia kwa unfdani utaona kuwa dini nyingi ni matokeo ya maisha magumu. Kisaikolojia mtu akiwa frustrated na ugumu wa maisha huanza kuota ndoto za mchana na kufantasize maisha yasiyo na taabu. mifano mingi inaonyesha hivyo.
1. Kuanzishwa kwa dini ya kiyahudi: Kuna mtaalamu anasema kuwa Wayahudi waliishi maisha mazuri sana wakati wa mfalme Daudi. Anadai kuwa baadaye mambo yalivyokuwa magumu, wakitekwa na kufanywa watumwa huku na kule na wababiloni na waajemi wakaanza kukumbuka enzi za Daudi. Mwishowe wakaanza kuota kuwa kuna mzao wa daudi atakuja na kurudisha neema ya wakati wa Daudi. Ndiyo huyo wakamwita Messiah. Chanzo ni ugumu wa maisha na kukumbuka enzi za Daudi.
2. Musa mwenyewe utaona kuwa alianzisha dini baada ya kuona mateso wanayopitia Waebrania kule Misri.
3. Mababu zetu walianzisha dini ili kuiomba mizimu wakati wa njaa, magonjwa na vita.
4. Kuna wakati wahindi wekundu walikuwa wanasakamwa sana na wazungu huko Marekani. wWalikuwa wamenyang;anywa ardhi yote nzuri. Wamewekwa kwenye maeneo makame na hawatakiwi kutoka huko. Na wakipigwa vita na kuuwawa kama wanyama. Akatokea mhindi mmoja akasema kuwa ametokewa na Yesu. Akadai kuwa Yesu huyo ni mhindi na ameahidi kuja kuwakomboa wahindi kutokana na mateso. Wanachotakiwa ni wacheze dansi bila kupumzika. Ikawa hivyo, watu wakaanza kucheza dansi mfululizo hadi pale serikali ya wazungu ilipoingilia kati kikatili.
5. Nilikuwa namsoma Malcom X. Dini yao ya Nation Of Islam ilianzishwa kutokana na maisha magumu waliyokuwa wanapitia watu weusi wa Marekani. Dini hiyo inasema kuwa Mtu mweupe ndiye shetani. Kwamba alizalishwa miaka elfu sita iliyopita. Na kuwa baada ya miaka elfu sita watu weusi ambao ndiyo watu asilia watarudia utukufu wao. Ni ugumu wa maisha uliozaa dini hii.
6. Budhha mwenyewe alianzisha dini yake baada ya kuoana mateso wanayopitia watu.
7. Dini nyingi zinazoanzishwa leo na wakina Gwajima, Mwamposa, Mzee wa Upako nk, zinaanzishwa sababu ya maisha magumu. Sehemu kubwa zinahubiri utajiri, uponyaji, na mafanikio kwa ujumla. Ugumu wa maisha ndizo zimefanya uwepo. Watu wakienda huko wanapata ndoto zao za mchana na kuepuka matatizo yao kwa muda.
Sababu nyingine kubwa ya kuanzisha dini ni ya kisiasa. Dini kama Ukatoliki na Uislamu n i kwa ajili ya watu kujipatia nguvu za kisiasa. Hata mifarakano kwenye dini hizi. Mfano kutokea kwa kanisa la Orthodox, Anglicana nk, ni sababu za kisiasa. Kutokea kwa Usunni na Ushia ni sababu za kisiasa.
Dini nyingi ni uzushi.
Sasa hicho ulichotaja na bible tofauti yake nini? Unadhan manabii hekima walikuwa wanatoa wapi mpaka wanawafundisha watu? Halafu unatak Yesu ashushiwe wakati anayajua yote.Qur'an imeshushwa kwa njia ya mdomo. Mtume naye aliwafikishia wafuasi wake kwa njia ya mdomo. Qur'an ilianza kuhifadhiwa mioyoni mwa wafuasi mpaka hapo baadae ilipokusanywa kwa maandishi. Ndo mana mpaka leo licha ya Qur'an kuwepo kwa njia ya maandishi bado watu wanaitunza mioyoni mwao ndo mana ni ngumu sana kuibadilisha Qur'an
Tafiti imefanyika na kuthibitisha kuwa toka ishushwe haijabadilishwa....kupunguzwa....wala kuongezwa aya zake...Qur'an imeshushwa kwa njia ya mdomo. Mtume naye aliwafikishia wafuasi wake kwa njia ya mdomo. Qur'an ilianza kuhifadhiwa mioyoni mwa wafuasi mpaka hapo baadae ilipokusanywa kwa maandishi. Ndo mana mpaka leo licha ya Qur'an kuwepo kwa njia ya maandishi bado watu wanaitunza mioyoni mwao ndo mana ni ngumu sana kuibadilisha Qur'an
Yesu alishushiwa Injili (Gospel). Walivyokuja akina John, Mathew na Luke kila mmoja wao akaja na version yake ya Injili. Bible ni mchanganyiko wa Injili ya John, Mathew, Luke na vitabu vingine na ndio maana inakasoro nyingi na umefanyika uchakachuani mwingi. Bibilia yenyewe haijawahi kuwa stable inabadilika badilika.Mkuu kwani BIBLIA ni nini?!!!
Ni mkusanyiko wa vitabu....je vitabu gani ?!!!
Vitabu vyenyewe vimeanishwa.....
Kwani mtume Muhammad SAW alishushiwa kitabu ama maneno ?!!!!
Ni kweli kuna utofauti kiasi kati ya maneno ya vitabu hivyo viwili(Quran na Biblia)....Quran ilishushwa na aliyeshushiwa akaifundisha kama yalivyo sawia maneno aliyoshushiwa....kwa upande wa BIBLIA....yako maandishi mengi yaliandikwa miaka mingi baada ya Yesu A.S kuondoka duniani....yako yaliyoandikwa na wanafunzi wake....yako yaliyoandikwa na watu wengine na ikasemwa ni maandiko ya wanafunzi wake.....swali la kutafakari ni je kuna uhakika gani kuwa kila andiko linatoka moja kwa moja kwa mwalimu ?!!!!
Je kumepatikana historia sahihi ya kusemwa kuwa wanafunzi wake walikuwa wanaandika katika magome ama "vitambaa" kila lililonenwa na mwalimu wao Jesus?!!!
Hapa ndipo fikra chanya na upembuzi hutakikana....
Umeusoma ukristo? Yesu alishushiwa injili na sio bibilia. Na bibilia haijahusisha injili aliyopewa Yesu bali imehusishwa injili ya John, Mathew na LukeSasa hicho ulichotaja na bible tofauti yake nini? Unadhan manabii hekima walikuwa wanatoa wapi mpaka wanawafundisha watu? Halafu unatak Yesu ashushiwe wakati anayajua yote.
Hapa uliposema Yesu anayajua yote ndipo watu hufikia kupingana[emoji1787][emoji1787]Sasa hicho ulichotaja na bible tofauti yake nini? Unadhan manabii hekima walikuwa wanatoa wapi mpaka wanawafundisha watu? Halafu unatak Yesu ashushiwe wakati anayajua yote.
Yesu hakushushiwa injili ndugu ila alihubiri injili alishushiwa na nani wakati alikuja nayo.Umeusoma ukristo? Yesu alishushiwa injili na sio bibilia
Bible haijaandikwa kama gazeti la mwanahalisi ni mafundisho ya jinsi mwanadamu mkamilifu anatakiwa aishi. Kuna mambo Yesu aliyasema kama mwanadamu kama lengo lake la kuja duniani so inabidi uelew muktadha. Lakini kuna mambo aliyasema kama Mungu usichanganye hapo.Hapa uliposema Yesu anayajua yote ndipo watu hufikia kupingana[emoji1787][emoji1787]
Kwa imani yako ni kweli Yesu hwenda anayajua yote kwani ni MUNGU.....
Ila ndani ya Biblia anasema "haijui saa ya kiama"....je kutoijua saa ya kiama hakumpunguzii sifa ya kuyajua yote?!!!
Namshukuru Mungu kwakila jambo na amenipa uwezo mzuri wa kufikiri hapa nilipo naandika kitabu cha ujasirimali ambacho kimesheni vitu vingi nipo jf kwa muda kuchangamusha akiliElezea ni kwa namna gani vifungu vinafanya mtu asiamshe ubongo. Maan bible inasema asiefanya kazi asile lete vinavyofanya mtu asijishughulishe. Halafu wewe unahisi watu wa dini hawajafanya mapinduzi ya technolojia sababu hujasikia wakizungumziwa katika bible maisha yao ya kawaida yalikuwaje na umekuwa brainwashed na hao wanaoandikwa maforbes lakini hujui katika safari zao wamepata maarifa kutoka kwa watu hata wa dini mbali mbali.
Sahihi.....Umeusoma ukristo? Yesu alishushiwa injili na sio bibilia