Maisha magumu ni sababu kubwa inayofanya watu waanzishe dini

Maisha magumu ni sababu kubwa inayofanya watu waanzishe dini

DINI YA WAISLAMU IMEANZISHWA NA PADRE WA KATOLIKI KWA LENGO LA KUITAWALA DUNIA..

Waraqa bin Nawfal ni mtu ambaye alikuwa na ujuzi wa dini ya Kikristo na alikuwa ni binamu wa mkewe Khadija bint Khuwaylid, ambaye alikuwa mke wa kwanza wa Mtume Muhammad (S.A.W). Kuna riwaya ambazo zinasema kwamba Waraqa alitabiri kuja kwa Mtume Muhammad (S.A.W)

kabla ya kuanza kwa utume wake, na alimsaidia sana katika kuanzisha Uislamu. Waraqa alikuwa na maarifa ya Biblia na Injili, na inasemekana kuwa alikuwa amejiweka katika sehemu za kupata maarifa hayo katika enzi zake.

Baadhi ya riwaya zinasema kuwa Waraqa alisoma maneno ya kwanza ya Suratul-Alaq ambayo yaliteremshwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) katika Pango la Hira. Waraqa alikuwa mmoja wa watu wa kwanza kusilimu, na inasemekana kuwa alikuwa ameshaandika baadhi ya vitabu ambavyo vilikuwa vinaashiria kuja kwa Mtume Muhammad (S.A.W).

Hata hivyo, Waraqa alifariki kabla ya kuanza kwa utume wa Mtume Muhammad (S.A.W) na hivyo hakuwa mmoja wa Masahaba wake wa karibu.
Hii mm nakubali kuwa Mwanzo wa uislam ni Ukatolik umesema vema.. Na lengo ni ilo kuitawala dunia..
 
Naona mshashiba sasa na pumzi zinawadanganya mnataka kutuchafulia hali ya hewa.

Nikukumbushe tu aliwahi kuishi nabii aitwaye Suleiman na mpaka sasa hajawahi na hatowahi kutokea mtu mwenye utajiri, mamlaka na uwezo kama aliokuwa nao Suleiman.

Licha ya uwezo wake wote huo bado aliendelea kumtumikia Mola wake. Iweje mimi na wewe tusio na lolote tujisahau na tuanze kukashifu dini.

Mungu yupo na dini zipo ila dini ya kweli ni uislamu unaokutaka umuabudu Mungu mmoja bila ya kumshirikisha na kitu chochote. May Allah guide you and I
suleiman alikua dini gani
 
Hii mm nakubali kuwa Mwanzo wa uislam ni Ukatolik umesema vema.. Na lengo ni ilo kuitawala dunia..
Ushahidi huo wa uislamu kutoka ukatoliki uko wapi ?!!!

Dini inayoamini Yesu ni Mungu inakuwaje inayoamini Yesu ni nabii ?!!! Hili pekee halifanyi kuwa hoja yako ikose mashiko ?!!![emoji1787][emoji1787]
 
Ukiangalia kwa unfdani utaona kuwa dini nyingi ni matokeo ya maisha magumu. Kisaikolojia mtu akiwa frustrated na ugumu wa maisha huanza kuota ndoto za mchana na kufantasize maisha yasiyo na taabu. mifano mingi inaonyesha hivyo.

1. Kuanzishwa kwa dini ya kiyahudi: Kuna mtaalamu anasema kuwa Wayahudi waliishi maisha mazuri sana wakati wa mfalme Daudi. Anadai kuwa baadaye mambo yalivyokuwa magumu, wakitekwa na kufanywa watumwa huku na kule na wababiloni na waajemi wakaanza kukumbuka enzi za Daudi. Mwishowe wakaanza kuota kuwa kuna mzao wa daudi atakuja na kurudisha neema ya wakati wa Daudi. Ndiyo huyo wakamwita Messiah. Chanzo ni ugumu wa maisha na kukumbuka enzi za Daudi.

2. Musa mwenyewe utaona kuwa alianzisha dini baada ya kuona mateso wanayopitia Waebrania kule Misri.

3. Mababu zetu walianzisha dini ili kuiomba mizimu wakati wa njaa, magonjwa na vita.

4. Kuna wakati wahindi wekundu walikuwa wanasakamwa sana na wazungu huko Marekani. wWalikuwa wamenyang;anywa ardhi yote nzuri. Wamewekwa kwenye maeneo makame na hawatakiwi kutoka huko. Na wakipigwa vita na kuuwawa kama wanyama. Akatokea mhindi mmoja akasema kuwa ametokewa na Yesu. Akadai kuwa Yesu huyo ni mhindi na ameahidi kuja kuwakomboa wahindi kutokana na mateso. Wanachotakiwa ni wacheze dansi bila kupumzika. Ikawa hivyo, watu wakaanza kucheza dansi mfululizo hadi pale serikali ya wazungu ilipoingilia kati kikatili.

5. Nilikuwa namsoma Malcom X. Dini yao ya Nation Of Islam ilianzishwa kutokana na maisha magumu waliyokuwa wanapitia watu weusi wa Marekani. Dini hiyo inasema kuwa Mtu mweupe ndiye shetani. Kwamba alizalishwa miaka elfu sita iliyopita. Na kuwa baada ya miaka elfu sita watu weusi ambao ndiyo watu asilia watarudia utukufu wao. Ni ugumu wa maisha uliozaa dini hii.

6. Budhha mwenyewe alianzisha dini yake baada ya kuoana mateso wanayopitia watu.

7. Dini nyingi zinazoanzishwa leo na wakina Gwajima, Mwamposa, Mzee wa Upako nk, zinaanzishwa sababu ya maisha magumu. Sehemu kubwa zinahubiri utajiri, uponyaji, na mafanikio kwa ujumla. Ugumu wa maisha ndizo zimefanya uwepo. Watu wakienda huko wanapata ndoto zao za mchana na kuepuka matatizo yao kwa muda.

Sababu nyingine kubwa ya kuanzisha dini ni ya kisiasa. Dini kama Ukatoliki na Uislamu n i kwa ajili ya watu kujipatia nguvu za kisiasa. Hata mifarakano kwenye dini hizi. Mfano kutokea kwa kanisa la Orthodox, Anglicana nk, ni sababu za kisiasa. Kutokea kwa Usunni na Ushia ni sababu za kisiasa.

Dini nyingi ni uzushi.

Dini inayomuamini kuwa Mungu ni mmoja tu....iite vyovyote iwavyo!
zipo dini kama 10,000 zinazoamini mungu wao ni mmoja tu.tena kwenye vitabu vyao hasemi tumeumba anasema nimeumba.jibu swali alikua dini gani?
 
Ni kama ukweli fulani. Dini zinakuja kutatua matatizo. Ni upatanisho baina ya binadamu na Mungu wao. Usahihi upo kimsingi maana dini zipo Kwa namna hiyo.
 
Naona mshashiba sasa na pumzi zinawadanganya mnataka kutuchafulia hali ya hewa.

Nikukumbushe tu aliwahi kuishi nabii aitwaye Suleiman na mpaka sasa hajawahi na hatowahi kutokea mtu mwenye utajiri, mamlaka na uwezo kama aliokuwa nao Suleiman.

Licha ya uwezo wake wote huo bado aliendelea kumtumikia Mola wake. Iweje mimi na wewe tusio na lolote tujisahau na tuanze kukashifu dini.

Mungu yupo na dini zipo ila dini ya kweli ni uislamu unaokutaka umuabudu Mungu mmoja bila ya kumshirikisha na kitu chochote. May Allah guide you and I

Chizi mmoja wapo huyu hapa,akili ipo braiwashed to the max,hata akiambiwa atinduliwe ili aende kwa ala hawezi kataa yani ni kama zezeta.
 
Unaizungumzia dini gani mzee. Kama ni ukristo sawa hiyo iko wazi kuwa mnakamuliwa na wachungaji. Uislam hauna hayo mambo.

Kingine nchi za kiislam zina jali watu wao kuliko nchi zisizo na dini rasmi. Nchi kama za kwetu ndo tunakamuliwa na serikali ila nchi za kiislam maisha ni safi sana. Angalia nchi za kiarabu jinsi wananchi wake wanavyoneemeka, serikali yao inawasaidia na kuwajali.

Bila mafuta waarabu wangekua wanatawadhia michanga ya jangwani,
 
Naona mshashiba sasa na pumzi zinawadanganya mnataka kutuchafulia hali ya hewa.

Nikukumbushe tu aliwahi kuishi nabii aitwaye Suleiman na mpaka sasa hajawahi na hatowahi kutokea mtu mwenye utajiri, mamlaka na uwezo kama aliokuwa nao Suleiman.

Licha ya uwezo wake wote huo bado aliendelea kumtumikia Mola wake. Iweje mimi na wewe tusio na lolote tujisahau na tuanze kukashifu dini.

Mungu yupo na dini zipo ila dini ya kweli ni uislamu unaokutaka umuabudu Mungu mmoja bila ya kumshirikisha na kitu chochote. May Allah guide you and I
Ww ulishwahi kumuona nabii suleiman au ni story tu umekariri?
 
Back
Top Bottom