Wazee, anachosema mtoa Uzi ni kweli kuhusu wajeda wa Congo na hata Burundi. Hawako serious au hawana Ile nidhamu ya jeshi Kama la Tz. Kukuona silaha anakupa kabisa bila shida. Mimi nilienda Burundi Kati ya mwaka 2008, mwenyeji wetu alikuwa mjeshi wa Kule Burundi na alikuwa anaishi kambini. Tulilala kwenye chumba na Cha ajabu kulikuwa na silaha; SMG, G3, na Bastola. Zote zilikuwa na magazine zimejaa na chini risasi zilikuwa zimemwaga Kama rundo la karanga. Nilikuwa na mwenzangu mmoja tuliyeenda nae. Yule mjeda alituambia kuwa, Hali ya usalama kwao ilikuwa tete, yaani jeshi like la watusi lilikuwa haliwaamini wanajeshi waasi wa kihutu waliokuwa wamejumuishwa jeshi. Hivyo, akasema tukiona Hali isiyoeleweka tujilinde. Wote akatupatia bunduki pembeni yetu. Nilishangaa na mm hivyo mnavyoshangaa. Uzuri nilikuwa nimeshapita jkt na nilikuwa nakumbuka kutumia G3 na SMG. Wazee wale hawana nidhamu ya jeshi, amini hivyo.