Maisha na mikasa ya safari yangu nchini DR Congo miaka ya 2000's hadi kutaka kupigwa risasi hadharani

Maisha na mikasa ya safari yangu nchini DR Congo miaka ya 2000's hadi kutaka kupigwa risasi hadharani

Stori nzuri sana mkuu, asante tunasubiria muendelezo hapa....
 
Inaendelea sehemu ya sita....

Nawasalimu ndugu bila shaka mnaendelea powa sasa baada ya mechi kuahirishwa hadi saa moja naomba tuendelee sasa .

Tumeshavuka boda tuko upande wa congo huku nipo kwenye gari nafanya mazungumzo na yule jamaa anaetaka lifti mimi sikuwa na chakuongezea tena nikamshukuru jamaa nikamwambia kuna mtu ndo mwenye magari kama atakuja ntamwambia kuna kichwa akikubali tukubebe ntakubeba usijali ila.usikae mbali sanaa na hapa mimi nikapandisha kioo nikaendelea kuwaza huku nawazua aise nikiri kuwa katika maisha yangu yetu siku ile ndo nilipa msongo mkubwa wa mawazo haijapata kutokea imagine nina dolla 130$ mfukoni lakini sio raha hata kidogo kipindi hicho hiyo pesa ilikuwa juu ukiabadilisha kwa madafu unapata hata kodi ya nyumba ya mwaka mzima na chenji inabaki.

Wakati naendelea kuwaza mara ghafla rama akaja akawa ananiongelesha kuhusu hali ilivyo njiani yani linaongea utafikiri lilikuwepo anasema sasa hakuna kitu askali.wa congo walisafisha njia hakuna tena wakutusumbua tusubiri tu maboss waje watupe hela sisi tutoboe halafu anaongea huku anacheka wakati huo mimi mawazo yapo mbali sanaaa.

Kuna kosa kubwa nilifanya pale boda wakati wa kumsikiliza yule jamaa anaetaka lifti nilimwambia kuwa tutaondoka pale mda si mrefu halafi nilivyocheki ila sehemu aliyokuwa aamekaa kwenye kibanda sikumuona yani alipopea ghafla sasa katika kumpa taarifa rama kuhusu yule jamaa ghafla akabadilika akawa ananilaumu nikashangaa kumbe huo ndo mchezo wao majambazi na na watekaji wengine wanakuwa na. informer wa vikundi vya waasi mfano MaiMai yani wanatengeneza mpango kuanzia boda ili kufanikisha utekaji sasa ukiwapa taarifa zako muda wa kutoka wanajipanga vizuri nakutoa taarifa kwa wenzao walipo polini katika ya poli huo ndo unakuwa mwisho wako .wazee wa tank za mafuta wanajua hii michezo , wajinga wanaweza teka tank zima likaingizwa porini wakanyonya disel au petrol yote na wakaichoma gari moto wakikusamehe mnaachiwa gari tupu sasa kimbembe kujieleza kwa majiri lokapu lazima ukae kwanza.

Basi rama akawa ananipa hizo story nikajua kumbe ndo maana jamaa alikuwa ananihoji maswali mengi sanaa kuhusu hata aina ya gari Unajua zile gari zilikuwa mpya tena na makaratasi yake bado hivyo nikawa nimeelewa sasa ghafla tu rama akatoka kidogo akarudi tena baada ya kama nusu saa akaniambia kijana umeshaharibu ratiba sasa ngoma hapa tunaondoka saa kumi jioni hela imeshatumwa na maboss customer kwa jamaa yao tukale tupumzike kidogo ila kuna askali miongoni mwa wale alikuwa anaongea nao pale boda wanataka lift hadi lubumbashi hivyo tutakuwa nao na sasa tumepata ulinzi wa chee

Ebwanaeee nikasema sasa naingia vitani bila kupenda yanii tupo na wale askali kwenye gari na mibumduki yao ile mikubwa mikubwa hivi tukifika katika polini wakatwambia simameni tuzipige kwanza na waasi tutakataa nikawa nawaza najiuliza sasa maisha yangu ndo yamefika mwisho ...

Wakati nawaza likaja roli la jeshi la congo pale boda likaanza kuwapakia askali kadhaa kwenye roli wakapanga mle walikuwa wengi takribani kama mia nakitu hivi wakapanda waliokuwa na rama kama 15 wakagoma wakasema wao wana gari za kupanda watangulie tu wao watakuja na sisi .
Yani lile roli limejaa matundu ya risasi ubavuni aise halafu hata vioo halina halafu kilichonifurahisha lile roli alikuwa anaenda mwanamke inaonekana ni shupavu kweli kweli , waozijua zile benz za mitairi mikubwa na mfano wa gari alilokuja nalo yani lile gari kwanza halina vishukio yani nikurukia tu na kushuka unaruka tu sasa yule dereva mdada lakini shupavu kweli kweli yani alivyokata kona kuingia boda nikasema labda mwanaume aise alifungua mlango akaruka kutoka juu hadi chini bila kuteteleka hata kidogo halafu yupo full combati chini na bastora na kisu kiunoni na bomu la granade, juu yule mdada alivaa tu kusinglendi cha jeshi ebwana ee yani niseme tu ukweli yule dada aliniongezea ujasiri yanii mwanamke kwanza mwanajeshi halafu katoboa katika njia chafu kama ile mimi kwanini niogope tena mtoto wa kiume lakini nafsi nyingine inaniambia huyo ndo kazi yake kazoea lakini kwakweli alinifanya mipate faraja ya japo nilimuona tu kwa mbali wala sikupata hata nafasi ya kuongea nae.

Naomba niongee kitu kidogo kabla sijaendelea kuna mdau kwa comment anasema askali.kukupa bunduki ushike shike ni ngumu sanaa nami nakubaliana nae kabisa ila sio askali wa congo kwa kipindi hicho yani wale sio askali ni washenzi yani yule ukashampa beer zile prisner mbili tu unaweza muomba bunduki ukaenda ukafanya yako ukarudi zako hamna askali mle labda sasa sijui nidhamu sifuri halafu kipindi hicho kumuona raia anatembea na bunduki tena zile raifo za masniper mtaani ilikuwa jambo la kawaida kabisa wala hakuna wa kumshangaa mwenzio.
Kama mnafuatilia taarifa kule GOma mashariki mwa DRC haya mambo yalikuwa yanaendelea hadi majuzi mwajeshi mzalendo wa kitanzania GEneral james Mwakibolwa alivyoenda kukomesha huu ujinga kupitia operation ya ondoa waasi wa waADf na wale waliokuwa wanapata ufadhiri kutoka serikali ya Rwanda mwanajeshi muasi kibaraka wa kagame sultan Makanga mpiganaji hodari wa vita ya msituni .siku moja ntaleta story nini alifanya kule mashariki mwa drc hadi wacongo wakiona siraha wanaikimbia kwa kifupi hii ni mbinu yakuchanganya jeshi la serikali yani waasi hugawa silaha kwa raia na kuwaambia wajilinde wenyewe hivyo huvichanganya vikosi vya usalama kujua muasi ni nani ?

Itaendelee....wazee sasa tumefika patamuuu urojo.iftar inakaribia karibuni.
Chai imeanza sasa.

Mwakibolwa alipambana na M23 na wala sio ADF.

We hadithia tu khs Safari yako hayo mengine utaanza kutunywesha chai ya motoooo.
 
Stori very interesting ila Sasa kwanini usiiweke juuu mwanzo wa uzi ? Sisi watu wa tecno tunapata taabu Sana alafu namsomea mke wangu anapenda Sana

Kama upo maeneo ya huku kwetu nitakupa zawadi ya sikukuu
Unamsomea mkeo yeye hajui kusoma?
 
Yes sure,ADF waliifanyia ambush Jw kipindi hicho Gen. Mwaki akiwa ameshastaafu utumishi.
Kwahiyo una uhakika Mwaki hajapambana nao alipokuwepo?? Wao walifanya ambush tu?
Kwa taarifa tu ni kwamba M23 walikua ni almost jeshi Kamili na walipigana conventional warfare kabisa lakini ADF ndo wana mtindo wa kuingiza RAIA katikati na wanafanya ambush mtaani mpk Mwaki akabadilisha mbinu wakawa wanavaa mashuka ya kimasai na visu tu kupambana nao na sio gwanda za kitenge
 
Back
Top Bottom