Maisha na mikasa ya safari yangu nchini DR Congo miaka ya 2000's hadi kutaka kupigwa risasi hadharani

Maisha na mikasa ya safari yangu nchini DR Congo miaka ya 2000's hadi kutaka kupigwa risasi hadharani

Inaendeleaa sehemu ya tano....

Haya wandugu sasa tuendelea na kipindi hiki cha kutafutia usingizi naamini mlikuwa mnanisubiri kwa hamu japo afya bado mgogoro kidogo...

Kwanza niwashukuru wote mlionipa pole asanteni na mungu awabariki wote mnaocoment na wala ambao mnachungulia kiaina uzi ...

Sasa tuendelee .. giza likaingia mwisho kukakucha mapema tupo kwa jamaa japo nililala chumba kimoja na rama lakini nilivyoamka sikumuona ila mabegi yetu yapo chumbani nikajua tu huyu amedamka kumbe mpuuzi huyu kanikimbia usiku mwingi sanaa kwenda kutafuta mabibi huko aise yani ugenini lakini bado unaonyesha uhuni wako shukrani chumba tulichopewa ni chumba cha njee tena kipo karibu na barabara kabisa yanii ukifungua mlango tu upo barabarani ..duuhh .
Nikaamka ila aise nilikuwa na uchovu wa kufa mtu nilitamani nilale hadi saa sita lakini ikawa haiwezekani mtu mzima nikaamka nikajiweka safi nikatoka nje nikawa nimekaa tu kwenye jiwe nje ya chumba na msikilizia rama kama atakuja unajua miaka ile simu ilikuwa ishu ni watu wachache walikuwa na simu ila rama alikuwa nayo ya alcatel kubwa kubwa hivi ndo alikuwa anatumia kufanya mawasiliano njia nzima na jamaa wale .
Sasa kwakuwa sikua na simu nikawa nimetulia nasikilizia na kweli saa moja kamili jamaa akafika ameongezana na yule mwenyeji wetu cha kushangaza kanisalimia tu na kuniomba passport sasa nikajiuliza huyu vipi pass yangu ya nini tena mbona kazi imeishia hapo nikaona nisilete ujeuri mbele ya mwenyeji nisije onekana mkorofi labda kuna mambo anaweka sawa ili tukabidhi mzigo tusepe nikamkabidhi likawa kosa .

Akasema dogo nisubiri hapo akaondoka na yule jamaa wakakaa kama nusu saa hivi akarudi pekee yake akanikabidhi pass yangu kuangalia mama yangu kucheki imeshagongwa tayari muhuri wa zambia na congo tobaaa kwanza nikamshangaa nikamuuliza sasa ndugu si tunaishia hapa akajibu tena simple tu dogo tunatoboa hatuwezi acha dola 75 kwa kilomita 100 jiandae twenzetu wanaokuja kupokea haya magari wameshindwa jana zilichapwa njia ya kuu ya lubumbashi hivyo hawawezi kuja tumeambiwa tumalizie kazi aise nilimuangalia rama kwa hasira iliyochanganyika na hofu kubwa moyoni hadi nikajuta kwanini nimemsikiliza huyu kichaa tukaanza malumbano mle chumbani ya kwanini yeye anafanya mambo bila kunishirikisha yeye yupo kimya tu anapanga nguo zake hana habari anacheka tu .

Yani hakuna kitu kibaya kama kuongozwa na mtu ambaye hakushirikishi katika kuamua njia ipi upite yani kwanza njia huijui hujui unarudi vipi ? Pesa yote hujamaliziwa maboss wanamjua rama wewe hawakujui maanake rama ndo angenilipa.mimi sio wao nikatafakari sanaa nikasema ni kimbishia au nikiendele kuwamkaidi ntakosa haki zangu zote yani ataniacha na hela sintopata nikapiga moyo konde ngonja nione ila tukawa sasa tunatembea kuelekea kwenye gari lakini hatuongei yani tumenuniana yani jamaa ana roho ngumu vibaya .

Madereva wa maroli nauzoefu wao wote wa njia waligoma kuanzaa safari siku hiyo mpaka escort kutoka lubumbashi lakini huyu chizi analazimisha tutembee hivyo hivyo njia ambayo janaa yake tu usiku zimipigwa tena sio kupigwa tu askali wa congo walikimbia kabisa mapigano huyu mwehu analazimisha nikawa nawaza huyu jamaa ni chizi au ...

Ebwana baada ya kumaliza kuweka kila kitu sawa nafikiri sisi ndo tulikuwa wa kwNza kukaguliwa sikuona mtu pale custom anagonga nadhani walikuwa wanasikilizia kwanza .tukawasha gari tukavuka upande wa congo ila wakati tunakaguliwa macho ya wale jamaa custum ya zambia kama yalikuwa yanatuangalia kwa huruma vile yanii kama wanataka kuniambia jambo lakini wanasita.

Sasa ikawa ni zamu ya upande wa kongo , boda nzima imejaa wanajeshi tupu yani utafikiri vita jana ilipiganwa hapo wamechafuka vibaya yanii inaoenakana janaa walikuwa na shughuri nzito na kweli wakawa wanahadithia mapigano ya usiku wanaongea kiswahili chao kibovu lakini nikawa nawaelewa wamebeba silaha nzito za kivita hadi zile za kuchomeka kwenye gari nyuma.


Naomba niongee kitu.

Kuna utofauti mkubwa kati ya ujasiri na uoga unaweza ukawa commando au hata General lakini usiwe jasiri lakini unaweza ukawa mtu wa mtaani tu huna mafunzo hata ya mgambo lakini ukawa jasiri vibaya mno , na swala la ujasiri sio swala la kufundishwa ujasiri mtu anazaliwa nao akiwa jasiri na yale mafunzo ya sijui jeshi ,polisi sio ya kukupa ujasiri ni kwaajili ya kukufanya usiwe muoga fanyeni uchunguzi utakuja kukubaliana na mimi

Sasa wakati mimi sina hili wala lili akili.iko mbali sanaa hili.jamaa(rama ) linabonga tu na wala wanajeshi linapiga story linacheka vibaya tena kwa sauti tena wanalipa.kabisa bunduki linashika kama linalenga shabaha nao wanashangilia kama vile wamempata mwanajeshi mpya wa kujitolea aise.

Wakati tuka bado boda pale mimi sijui kinachoendelea na rama lipo kwa wanajeshi tena wameliweka mtu kati linapiga maneno kama lienyeji akaja mtu moja hivi dirishani kumbuka mimi nipo ndani ya gari nimejikunyata nasubiri kupokea amri kwa rama twende ama laa
Akagonga nikashusha kioo akawa anaulizia kuwa tunaenda lumbumbashi unajua pale mara nyingi madereva wa IT huwa wanakula vichwa vya abiria sasa nikamjibu ndio akaniuliza saa ngapi nikamwambi sii mda mrefu akaniambia yeye kaja janaa usiku hapo boda ni mfanya biashara ila njiani walikuta maiti nyingi za wanajeshi wamekufa na raia sasa iweje sisi tuharakishe kabla hali haijawa shwarii ? Ndugu zangu niseme tu ukweli nilihisi kimkojo kinanitiririka kwa mbali nikajaribu kuuzia lakini wapi hakuna kitu kibaya kama hofuu licha takuuzia mkojo lakini ulitoka.....mamaaee nikaon kifo hiki.

Itaendelea ..........ngoja niangalie beyhadh( chizi wa mapenzi ) nitarudi ishallah.
Mkuu startimes wajanja sana
 
Ukiwa na mwanaume unaishi nae akakuthamini, kukupenda na kukuheshimu kuwa wewe ni mkewe, mheshimu sana huyo mtu. Tunapitia masaibu mengi sana tunapokuwa kwenye utafutaji maalum kwa ajili ya wake na watoto wetu. Usijikute wa kubenua benua kidomo.
Kiukweli inabidi tuwe watiifu tu!wanaume mmeumbwa mateso kuhangaika.
 
Hahaaa mie ntasimulia siku moja nilivyomkata mtu mkono panga kama 30 hivi hadi nikaung'oa halafu nikaufunga kwenye kisalufeti kumpelekea boss. Miaka mingi sana iliyopita walikua wanatuibia sana mizigo tukawategea kilima kimoja nyanda huko

Boss kila siku anatukata mshahara mke wangu ana mimba safar wiki nzima narud nyumban sina hela. Tukaamua kula nao sahani moja

Tunafika Tanga nakabidhi mzigo umetimia nikamwambia boss kila siku tunaibiwa gar haina nguvu inapanda kilima kwa shida huelewi. Leo tumewashughulikia anashangaa nikamfungulia ule mfuko Hahahaha nusu akimbie ofisi. Kuanzia kwenye biceps hapa mpaka vidole mzigo kama wa roboti
[emoji44][emoji44]
 
Back
Top Bottom