We umeandika bila mahesabu, ukisema " miafrika" unamaana ipi hasa?! Unajua ukiangalia Ethnic groups ya bondeni wazawa weus ndo weng na ndo waharifu wakubwa hao
Hapo kwenye neno Miafrika umeshindwa kunielewa tu... ila sio tatizo.
Hapo mnaposema Wasouth Africa weusi ndiyo waharibifu wa kubwa ndipo ninapopapinga Mimi.
Miafrika kuanzia Morocco hadi Zimbabwe yote ipo SA. Wengi wao hawana vibali. wametoka nchi zao kuja kutafuta kazi. Elewa hakuna nchi Africa yenye wageni wengi kama SA.
Kinachotokea resources ni chache lakini una kundi kubwa la watu. Lazima purukushani itokee hapa. Hao wageni wanaokuja baadhi wana skills na baadhi hawana. Hao wenye skills watachukua kazi za wazawa na wazawa watakuwa hawana kazi.
Kundi litakalo kosa kazi litajiingiza kwenye shughuli haramu ilimradi linapata chakula. Hawa Wasouth ambao wameachwa hawana kazi watajiunga na Hawa wahalifu wa kigeni na kuendeleza uhalifu.
Kazi zilizopo South Africa zingeweza kutoshea idadi ya wazawa kama wageni wote wasingejazana hapo.
Sasa wa kulaumiwa kwenye hili siku zote amekuwa Msouth Afrika mweusi... ooh mara ni wavivu, wahalifu, wapenda pombe n. k.
Wakati wanapoleta vurugu wanajaribu kutuma meseji kwa serikali Yao iliyoshindwa kucontrol illegal migrants kwasababu inaogopa maneno kutoka kwa waafrika waliowasaidia kupigania uhuru.
Kipindi Cha JK tuliona jinsi wabongo walivyopiga kelele baada ya wachina kuanza kuuza mahindi ya kuchoma mtaani. serikali ilichukua hatua mapema. Tusiwe wabinafsi... Mizimbabwe yote ipo SA na ina Fanya uhalifu wa kila namna.
Nitakueleza kisa kimoja kimetokea Limpopo few months back .. Wazimbabwe waliokaribu na Limpopo hupata huduma za afya South Africa tena bure kabisa. Sasa Dr akachoka maana imekuwa too much na wanaambiana wote wanakimbilia huko maana kwao hakuna hiyo huduma.
Siku Moja Dr akawatolea uvivu... wamekuwa wengi na serikali haiwapi bajeti inayowajumuisha Wazimbabwe. unfortunately, Kuna mtu alikuwa anachukua video . ikasambazwa online.... this lady had to step down... ila kwa mawazo yangu alikuwa sahihi kuwaambia hivyo.