Maisha ya depo

Maisha ya depo

MAISHA YA DEPO

SEASON-2

EPISODE 19

Alituambia kuwa inafika kipindi unachoka mpaka unakosa hamu ya tendo yaani mwanamke anaweza akawa mtupu na usifanye wala kumtamani ukamuona ni kama msela mwenzio.

Afande alitutahadharisha kuwa tujitahidi mno kipindi hicho hata mtu akidoji asiwe peke yake kwani unapodoji ukaenda kulala unaweza kulala kwa muda mrefu na ukiamka unajikuta una njaa ya kwenda.

Alitusimulia kuwa kipindi wao wako kozi kuna mwenzao alidoji peke yake walimtafuta wiki nzima bila mafanikio.

Siku moja walimkuta shambani akiwa amelala walipomuamsha hakuweza kufumbua mdomo, kuongea wala kutembea mana hata walipomsimamisha alikuwa akitetemeka na kuanguka kutokana na njaa kali aliyokuwa nao.

Tulimpinga sana afande kwenye swala la kuchoka mpaka kutotamani kufanya tendo pendwa mimi nilikuwa kinara wa hilo sikukubaliana naye.

Ilifika hatua tukawekeana viapo maana aliniambia kuwa kuna kipindi walidoji na MADAWILI kadhaa sasa kuna doja mmoja alikuwa anawachezea wale MADAWILI na hawajawahi kugundua mpaka kozi inaisha.

Nilimwambia kama huyo mwenzao aliweza kufanya hivyo basi siyo kweli na kama ni kweli basi itakuwa hao wengine wanashida ya nguvu za kiume, afande Elisha aliniahidi kunitafuta wakati huo utakapofika.

Tulipomalizana na kipengele hicho tulirejea zetu kikosini na afande Elisha ndiye aliyekuwa akiliongoza bogi hilo.

“Afande Elisha: Ewii
Sisi: Ewaaah
Afande Elisha: Ewii
Sisi: Ewaaah
Afande Elisha: Ewii
Sisi: Ewaaah
Afande Elisha: Ee Shaa, Shangazi
Sisi: Usikate shanga
Afande Elisha: Zuu zungusha
Sisi: Zungusha nyonga
Afande Elisha: Aii mama nilikuwa sijui
Sisi: Nikipata demu mauno mpaka asubuhi”.

Tulifika salama MAHANGANI na kuyafanya tuliyostahili kuyafanya ila hali ya hewa kidogokidogo ikawa inaanza kubadilika.

Ukafika muda wa msosi tukaenda zetu kuwakilisha kwa MZABUNI na hatimaye tukaelekea KOMBANIA ambako nilikutana na mazagazaga yangu kutoka kwa mtoto Linda nikayapokea na kuyapeleka HANGANI.

Ilipofika mishale ya saa tatu iliporomoka mvua kama ya buku na mdogo wake ilibidi tutolewe sehemu ile iliyokuwa wazi na kupelekwa kwenye bwalo la chakula walilokuwa wakilitumia maafande wa JKT.

Tuliwakuta Service Man hao wa JKT wakiwa wanaangalia tamthilia za azamtv hivyo ni kama tulienda kuwaharibia kwani iliwabidi waamke kwenye viti nao wasimame na viti kuviweka sehemu moja kwa kuvibananisha ili kusudi ipatikane nafasi ya kutosha.

Usiku huu haukuwa usiku wa kuimba wala kusifu ila ule usemi wa “Burudani kwa wote” ndiyo uliokuwa ukitanua mbawa zake kwa usiku huo.

Ilifika saa nne muda muafaka wa tamthilia pendwa ya Sultan ambayo iliwafanya watu kutokujali kama kuna mvua ilikuwa ikinyesha walikuwa wakiongezeka.

Alikuwa akionekana mama wa himaya Bi Hulem Sultana akiwa na chawa wake aliyemjaza nyota za kutosha wakiwa kwenye mipango ya kumpelekea pumzi ya moto Waziri mkuu aliyefahamika kwa jina la Ibrahim Pasha.

Kilikatika kipande cha kwanza kati ya vile vitatu kilipofika cha pili walikuja maafande wa zamu yaani afande Jamali aliyeongozana na afande Mpemba aliyekuwa na kifimbo chake mkononi kama cha afande Pastima.

Ilibidi runinga izimwe ili tuendelee na zoezi la lokoo lililochukua muda mrefu kutokana na kukosea kuhesabu maana tulikuwa hatusikilizani vizuri kutokana na makelele ya mvua na hata hivyo eneo lilikuwa ni dogo na tulikuwa wengi mno.

Hesabu zilipokaa sawa tuliruhusiwa na kwenda zetu MAHANGANI, asubuhi yake hakukuwa na mvua hivyo tuliendelea na ratiba nyingine.

Kipindi zinaendelea ratiba hizo nilipata kuuona umuhimu wa rainboot maana udongo wa sehemu ile haufai kabisa ulikuwa ukiteleza mno hata hivyo kulikuwa na nyakati nyingi za kukimbia hali iliyopelekea wengi wetu kwenda kuhiji Maka bila pasi na gharama yoyote ile.

Kwa kweli ardhi ya kikosi ilikuwa haitamaniki kabisa kuitazama maana kila sehemu ilikuwa imekanyagwakanyagwa utadhani watu walikuwa wakitengeneza udongo wa kufyatulia tofali za matope ama kujengea nyumba za ukuta wa udongo.

Ulipofika mchana mvua ikanyesha tena zaidi ya ile ya usiku hali iliyopelekea kupewa UTAWALA maana hakukuwa na kazi ingeweza kufanyika.

Tulifurahi na tukawa tunaomba iwe inanyesha mara kwa mara ili tusiwe tunafanya kazi kumbe tulikuwa tunajidanganya bila kujua wenyewe wana wimbo wao usemao “Haiwezekani kamanda maji kupanda mlima".

Kauli hiyo ilikuwa ikimaanisha kuwa kisichowezekana jeshini ni maji kupandisha kwenye mlima pekee na kama unakumbuka aliwahi kutuambia Afande Rashidi kuwa jeshini ni sehemu pekee ambayo kipara kinanyolewa hawa mabwana si ajabu wakatuaminisha kuwa inawezekana kabisa kuideki bahari😅.

Mvua hiyo iliyokuwa ikinyesha kwa heshima ilikuwa ikipungua na kukata kabisa ila ilikuwa tukifika KOMBANIA tu mawingu yalikuwa yakigongana na kumwaga cheche hivyo watu wakawa wanawapongeza babu zao kwa kazi wanayofanya.

Ustadhati Rehema alionekana kupata tabu na hali hiyo maana nguo zake zilikuwa zikikusanya tope la kutosha mbaya zaidi kuna kipindi tukiwa kwenye bwalo tulitakiwa kukaa chini hali iliyopelekea kukalia matope yaliyotokana na kukanyaga kwa viatu vyetu.

Asubuhi ya siku iliyofuata kulikucha shwari tukakimbia MABIO na kufanya usafi na kwenda zetu KOMBANIA tukaelekea zetu kwenye FATIKI ila tuliporudi tulijazana dukani kwa ajili ya kununua rainboot.

Siku hii hatukumkuta yule afande mnoko Koplo Jose ila tuliwakuta vijana wao wa JKT.

Wapo waliopata ila sisi wengine hatukufanikiwa maana ziliisha hivyo walichukua hela zetu na kutuambia tufuate baadaye mana waliendaa kufungasha kwa kawaida ilikuwa ni vigumu mno kuondoka dukani hapo bila ya kuacha hela.

Yaani ilikuwa ukienda ukakosa unachohitaji utawaachia hela tu labda uende ukaulizie kitu ambacho hawafungashagi ama kitu cha bei ndogo kama vile pipi ama biskuti hapo utanusurika ila si kwa bidhaa za msimu kama hizo.

Usiku ulipofika tukiwa KOMBANIA kuna dada mmoja alinifuata akiniomba nimsaidie kutoroka kikosini hapo maana alikuwa ameshapachoka.

Alikuwa ni Winifrida ambaye kama unakumbuka ile siku nawasili kikosini tukiwa maingate tunaandikisha PARTICULARS aliletwa dada mmoja na gari akisindikizwa na familia yake.

Kwanza nilimshangaa kwanini kanishirikisha jambo hilo lakini pia nilimuuliza ningewezaje wakati sikuwahi kufanya hivyo lakini niliogopa tusipofanikiwa huenda yakanikuta makubwa.

Aliniambia kuwa kwa anavyoniona ana uhakika kazi hiyo naiweza ila hata kama siwezi basi nimsaidie hata kwa mawazo.

Kwa kweli lilikuwa jambo gumu kwangu hivyo nilijaribu kumshauri asitishe na nilivyoona anang’ang’ania ilibidi nimwambie amtafute mtu mwingine. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

**************Itaendelea……….…………...

MAISHA YA DEPO

SEASON-2

EPISODE 20

Hatukumaliza mazungumzo hayo vizuri kwani afande Ashiru alikuwepo hapo kwa ajili ya lokoo hivyo nilishukuru ujio wake kwani uliniepusha na balaa hilo.

Tuliruhusiwa na kwenda zetu kulala ila nilipitia dukani kuulizia buti zangu nikakuta wamefunga hivyo nikanyoosha zangu HANGANI ambako nilichelewa kupata usingizi nikiliwaza swala hilo la mwanadada Wini.

Asubuhi kulikucha vizuri ingawaje ni kwa fujo na makelele kutoka kwa wazee wa mauzauza na baaada ya usafi tulienda zetu KOMBANIA.

Tukiwa tunasubiri muda wa FATIKI ufike ilisikika sauti moja ikisema “Nakuja sasa, nakuja” watu wote tuliangua vicheko.

Alikuwa ni mwamba kabisa wa kuitwa Mtalibani tulicheka kwakuwa tulijua shoo yake, mzee huyo hajawahi kupoa akiwa kazini.

Kama kawaida aliagiza ndoo zake tano za vifusi na kama ilivyo siku zote alilisimamia zoezi hilo yeye mwenyewe.

Kazi hiyo haikuwa ya kitoto kwani vifusi vyote tulivyoviweka awali vilikwenda na maji hivyo kama vijana wa China Civil (CCECC) tuliingia mzigoni chini ya mkandarasi Mzee Mtalibani.

Mzee huyo alikuwa akisisitiza vindoo vijazwe na yule aliyeleta nusu alimrudisha ama alimwaga bila kumhesabia kwa wale wenye bahati aliwaambia waunganishe na aandikwe mmoja.

Alipoona tunalegalega alitutia biti na kutuambia kuwa watakaokwenda kula mchana ni wale watakao kuwa wamelifikia lengo la kupeleka vindoo vitano.

Ilikuwa ni kivumbi na jasho siku hiyo niliwaona wengi wakihanya mfano mzuri ulikuwa ni Linda, Wini pamoja na Ustadhati Rehema niliwahurumia mno.😰

Ustadhati yeye ule upekee wake ulimsaidia na baadaye Mtalibani alimpa kitengo akituelekeza ni wapi tumimine vifusi hivyo.

Chakumshukuru muumba mbingu na ardhi ni kuwa leo hii katika wale makarani mmoja wao alikuwa ni mwanangu Amosi tuliyesoma naye ila yeye alikipiga CBG hivyo tukawa tunafanya uhuni mmoja hivi pamoja na Linda.

Kifupi ni kuwa nilipeleka ndoo tatu pekee ila alinijazia zote tano isipokuwa alikuwa akitumia akili moja hivi.

Amos hakutujazia hizo ndoo tano ilihali wengine wana mbili isipokuwa pale watu haswa wale kutoka kanda ya ziwa (sijawataja wasukuma😜) walipokuwa na ndoo mbilimbili mimi na Linda tulipeleka mojamoja ila yeye alitiki mara mbili kwa kila mmoja.

Safari nyingine tulimsaidia Wini ambaye aliandika jina kwa karani mwingine hivyo ikawa vigumu kucheza mchezo huo, ilikuwa nikibeba moja wao wanabeba ujazo wanaowezana nao wa nusunusu halafu tukikaribia kwa Mtalibani wanachangia anatoka mmoja kama kibati vile.

Awali nilikuwa nikimkwepa Wini ila aliponiona alijisogeza kwangu ikanishindwa kumkwepa tena hata hivyo nilimhurumia kipindi akihangaika safari yake ya kwanza.

Mchana wake tukiwa KOMBANIA jamaa niliyempa simu yangu akanichajie alinirejeshea baada ya siku mbili kupita akanipanga nimuongeze jero maana huko wanakochajisha bei imepanda eti kwasababu ya uwepo wetu.

Nilimkubalia ila nilimwambia kuwa ningempatia jioni maana kwa muda huo sikutembea na hela hivyo nikachukua namba yake na kumuahidi kumtafuta baadaye.

Mtalibani alikuja tena kwa awamu nyingine ila wakati huu lengo lilikuwa ni ndoo nne tulizama mzigoni na kulisongesha na isivyo bahati awamu hii Amosi hakuwepo kwenye ukarani.

Awamu hii Mtalibani alibadilisha wasaidizi wake wote isipokuwa Rehema ambaye wakati huu alionesha mabadiliko kwa kutokuja na juba.

Ustadhati alivaa suruali ya track (Mashaallah kwa mbali majaliwa tuliweza kuyaona😋) na tisheti kichwani akava kikofia chake tushindwe kuona kichwa chake nafikiri mataabiko ya mvua na matope ndiyo yalimpelekea kufanya hivyo.

Mabadiliko hayo hayakuharibu mifumo kwani mwanangu Baraka alipewa kitengo hicho hivyo mambo yaliendelea kuwa kitonga kama kawaida maana katika ndoo kumi na mbili zilizohitajika kutoka kwangu, Linda na Wini tulienda safari tatu ambazo ni sawa na ndoo sita.

Katika ndoo sita hizo tatu zilikuwa ni za kwangu na tatu nyingine ni za wale mabinti ambao waliunganisha nusunusu zao na kupata tatu kamili.

Uhuni mwingine uliokuwa ukiendelea ni kuwa watu walikuwa wanatikiwa halafu wanazuga wanamwaga kisha wanarudi na udongo wao ambao wanazugazuga nao katikati hapo (hawafiki kule unakochimbwa) na baadaye wanapeleka tena.

Kwa aliyekuwa masta wa hili ilimtosha safari moja tu kuzigeuza kuwa nne kikubwa SIFA WEPESI.

Kazi hiyo iliyokuwa na pilikapilika za hapa na pale ilifanyika mpaka ulipofika muda wa marejeo nasi tukarudi zetu MAHANGANI kuendelea na ratiba nyingine.

Kabla ya kufanya chochote nilipitia dukani kuulizia buti zangu licha ya kuwa tope lilikuwepo baadhi ya maeneo korofi ambalo sio swala swala ni kwamba nilikwishawapa maokoto ya jasho langu ambalo huwa sikubali liende bure.

Nilipofika dukani nilimkuta Koplo na aliponiona hali ikawa vilevile kwa kuwa aligundua najua sasa kukunja ngumi basi tabu ikawa palepale ila mwisho wa hadithi nilipewa buti zangu japo nilizipata kwa MASIMANGO😰 ya kiwango cha standard gauge.

Ilibidi nisubiri mpaka muda wa kula ndiyo aliniruhusu kuaondoka ingawaje alinipooza kwa juisi na biskuti kwakweli alikuwa akinichukulia poa sana😪.

Asubuhi yake ilikuwa ni siku ya Jumatatu tuliamka na kuendelea na ratiba kama zilivyokuwa zikitaka, tulienda kufanya usafi karibu na yalipo maskani ya mkuu wa kikosi ambapo mpaka kufikia wakati huo hatukuwahi kumuona.

Mara nyingi tulikuwa tukimuona makamu wake Matroni Neema aliyekuwepo kikosini wakati wote hivyo kwa upande wetu yeye ndiye tuliyemtambua kama mkuu wa kikosi.

Tukiwa tunarudi kufanya usafi njiani nilimuona Matroni Anna aliyeandikisha PARTICULARS zangu ile siku nafika ikabidi nisimame kusalimiana naye.

Nilisalimiana naye kupiga stori nikijifanya namjua na niliwahi kuonana naye mahali ila lengo halikuwa hilo kikubwa nilimuuliza kutaka kujua alichokua akikimaanisha siku ile kule main gate.

Kifupi nilitaka kujua maana ya msamiati Katerero licha ya kwamba nilijua ni jina la sehemu kule kwa kina Nshomile ila ilionekana kuwa na maana yao ya tofauti iliyowafanya wacheke.

Alitabasamu😊 na kuniambia “Aah we MZALENDO hembu niache nitafute baadaye mkiruhusiwa kwenda kulala ntakwambia”.

Nikamuuliza “Ntakuona wapi sasa hiyo saa tano wakati utakuwa ushalala zako HANGANI” akanijibu “Nitakuwa bwaloni naangalia zangu tv nalalaga saa saba eti”.

Kwa majibu hayo tu ilinibidi nifungue vitabu vyangu na maandiko mbalimbali yanayoelezea maswala ya uwekezaji katika mahaba nilipoyapitia nikagundua uwekezaji umelipa nikajisemea kumoyo “mtoto kanasa”💪🏿.

Nilijua itakuwa ni vigumu kumpata muda huo nilitaka nichukue namba yake ila simu niliiacha HANGANI kibaya zaidi nayeye yake hakuwa nayo.

Mdogomdogo niliondoka kuelekea HANGANI kwani tayari wenzangu walikwisha niacha mbali.

Nilipita njia iliyokuwa inatokea UWANJA WA DAMU ambao ulikuwa karibu na jengo la kuhifadhia silaha lililofahamika kama AMALA.

Niliwakuta askari wa jeshi la wananchi maarufu kama BAKABAKA wakiwa kwenye PAREDI la makabidhino ya silaha ambayo kwa siku ya jumatatu ilifahamika kama MASTER PARADE sasa bwana nikataka kujichanganya kitu kimoja. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

*************Itaendelea……………………....
 
EPISODE 21

Nilitaka kuukatiza UWANJA WA DAMU ili nitokee upande wa pili ambao ulikuwa na pacha ya njia inayokwenda HANGANI na ile ya jikoni kwa MZABUNI.

Nilichokiamini ni kuwa wakati mwingine malaika wa kheri hutembelea motoni 🔥kwani alinisimamisha afande mmoja ambaye yeye kwa bahati hakuhusika na PARADE nahisi alikuwa kwenye zamu ya lindo la jengo hilo la silaha.

Afande yule ambaye nina uhakika alikuwa na roho mtakatifu ndani yake aliniambia
“We MZALENDO ni kosa kukatiza mbele ya MASTER PARADE kama unataka kupita zunguka utokee kule”.

Sikuwahi kumuona yeyote akiadhibiwa kwa kosa hilo ila nilifikiria ukubwa wa kosa kwa kutizama waliokuwa kwenye zoezi lile walikuwa ni BAKABAKA shazi sasa vuta picha unafanya kosa mbele yao.

Nilibahatika kuziona PARADE nyingine ambazo huwa zina mchanganyiko wa BAKABAKA wachache na askari wengi wa JKT ila hii ya kuitwa MASTER PARADE sijui niielezeaje nilifikiria kuwa adhabu ambayo ningepewa ingekuwa ni zaidi ya kupelekewa pumzi ya moto.

Nilishukuru mno nikaambazaambaza zangu pembezoni mwa uwanja huo huku nikiwaona baadhi ya maafande waliopo kwenye PARADE lile wakinitupia macho kana kwamba walikuwa wanasubiri kuambiwa suuw! wanifuate.

Nilifika zangu HANGANI nikakutana na tukio la kibabe ( wazungu wanaita surprise)🙈 sijaamini bwana kumbe kipindi naenda kwenye usafi nilijichanganya nikaliacha sanduku wazi.

Wahuni walipita na kilongalonga changu pamoja na bukta moja wakaniachia laini yaani inaonekana mwizi alikuwa muungwana ila jambo la kusikitisha mpaka mwizi anafanya yote hayo hakuna aliyemuona hata huyu wa kuitwa mlinzi wa HANGA.

Ilikuwa ni siku mbaya na ndefu kuimaliza walionizoea waligundua hilo tukiwa kwenye FATIKI Wini alikuwa mmoja wao walioniuliza kilichonisibu nikamuelezea Linda yeye aliniahidi kunipa hela ninunue nyingine hivyo nisiwaze.

Usiku tukiwa KOMBANIA alinifata Wini na kuniuliza kama nimekwisha ipata jibu likawa hapana akanipanga kuwa endapo nikimsaidia kutoroka ataniachia simu yake.

Kwakweli alinisisimua nilimshangaa na kumuuliza “duuh ina maana una maanisha kweli mi nikajua umeghairisha” akanijibu kwa sauti yake ya kwanza kasoro “ndiyo bwana mi nshazichoka hizi shida” sauti yake iliwafanya watu watuzingatie ikabidi nimtonye akanielewa.

Nilimwambia anivumilie kwa siku mbili nitampa majibu Wini alinishangaa akidai kuwa hiyo siku moja yenyewe anaona kama nyigi anatamani aondoke hata kesho asubuhi yake.

Nilimsihi kuwa ingekuwa nimewahi kufanya hivyo ingekuwa rahisi ila sijawahi hivyo anipe muda tujue tunafanyaje kwani yeye mwenyewe hakujua anatorokaje ila alijua kuwa anataka kutoroka tuu basi.

Baada ya muda kufika tuliruhusiwa kwenda HANGANI nilimuomba simu Baraka na kuweka laini yangu nikampigia mwanangu Fadhili nikimtaka nionane naye ili tuongee ana kwa ana.

Aliniambia kuwa itashindikana maana yeye alikuwa MAHANGANI kwao ambako ni karibu na yalipo makazi ya mkuu wa kikosi ambako kulifahamika kama REST HOUSE.

Alisema kuwa hawaruhusiwi kutembea hovyo mida ya usiku maana njia ya kufika tulipo ilikuwa ni ile inayopita AMALA na nyingine inapita zilipo ofisi za UTAWALA.

Kwa uhalisia ni kuwa maeneo hayo yanakuwa na ulinzi mkali ambayo ni rahisi mno kufyatuliwa tunda ya moto kutoka kwenye mdomo wa maliasili ya jeshi.

Kwanza naomba nimvue uafande kwenye simulizi hii nitakuwa nikimuita jina lake siyo kwasababu nimesoma naye ama tunatoka sehemu moja ila hakuwa na sifa za kiuafande alikuwa ni mnoko.

Nasema hivyo kwasababu kabla sijaenda HANGANI nilipitia bwaloni wanakoangalia tv bwalo ambalo ukuta wake ulikuwa uko nusu kiasi kinachofanya kuwaona walioko ndani.

Nilikwenda bwaloni kwa lengo la kwenda kumtafuta Matroni Anna kama tulivyoahidiana asubuhi ila sikubahatika kumuona lakini Fadhili yeye nilimuona shida ni alikuwa katikati ambako sikuweza kufika na ule upara wangu kama si kufukuzwa ningeweza hata kuadhibiwa.

Hiyo ilinifanya niende HANGANI nikamcheki kwenye simu ili nimchomoe pale alipo kibaya ni kuwa wakati tunaongea kwenye simu nilisikia kelele za mabishano kuwa ni kibaraka yupi wa Hulem Sultana anaupiga mwingi kumzidi mwingine kati ya Gula na Sungra.

Nilimuona mnafiki kwani alinitaka niongee shida yangu kwenye simu nikampanga kuwa nahitaji kutoroka hivyo anisaidie nikamsikia akiropoka “Haah! We MZALENDO NANGA kweli umekaa wiki moja tu unataka kutoroka acha umama”.

Kwa kweli moja ya jambo lililonifanya nimshushe hadhi ni hilo na ndiyo maana nilitaka kuongea naye ana kwa ana kwani jambo hilo nilitaka liwe la usiri sana ila kuropoka kwake huko ni sawa na kuliweka hadharani jambo hilo.

Fadhili hakuishia hapo alikuja HANGANI na kuropoka maneno kibao akiwa na wenzake wawili “Sikia kutoka kwangu WAZALENDO namuulizia somebody Karim Rashidi Senkondo popote alipo mwambieni anaitwa na afande Fadhili”.

Nilimkaushia na bahati ni kuwa bado hatukuwa tukijuana vizuri sisi kwa sisi hivyo akakosa ushirikiano wowote akasepa zake.

Ikumbukwe alisema hawezi kuja kwasababu hawaruhusiwi kutembea usiku, tufanye labda aliamua kuvunja sheria hiyo ili aje anizuie kutoroka ila ukweli niliujua mimi ni mnafiki hakuwa HANGANI bali alikuwa bwaloni.

Alirudi tena HANGANI kwa mara ya pili nikamsika akisema “MZALENDO Karim nimeambiwa anaishi humu naomba mnionyeshe kitanda chake anataka kutoroka au ameshatoroka maana hata simu yake haipatikani”.

Nilimsikia MZALENDO mmoja akiropoka “Labda imeisha chaji” akamjibu “Simu nimemchajia mwenyewe jana nikampa mchana alafu namdai jero langu la kuchajia mbwa huyu kumbe ni tapeli”.

Duuh iliniuma kuitwa hivyo nilitamani niende kumvaa ila nashukuru nilipatwa na uvumilivu kiwango cha A+ na kumuacha aropoke zake.

Baadaye aliamua kupiga patrol ya kitanda kwa kitanda niliamua kutoka zangu nje na kwa bahati hakumaliza wote maana tulikuwa watu zaidi ya mia alipochoka aliondoka zake.

Sikupata usingizi mapema mana nilikuwa nikiwaza umama wa Fadhili lakini kikubwa ni kuhusu jambo la Wini aliyenipa usiku mzito kulifikiria jambo lake.

Maamuzi mengi yalikuwa ni kukataa hilo dili kwani ilikuwa ni kazi ya hatari sana kufanya kikubwa ilikuwa ni kuufanya uhuni huo dhidi ya jeshi.

Ni ofa yake tu ya kuniachia simu ndiyo iliyonishawishi kukubali ombi la binti huyo ambaye mbali na upara alionao urembo wake haukuacha kujionesha usoni mwake.

Basi usiku ukawa hakukuchi kunakucha ila mwisho wa picha kulikucha na tukaamka kuianza siku nyingine.

Baada ya MABIO nilienda zangu mtoni kwa lengo la kufua na kuoga nilikwenda na tagi langu kichwa mbovu aliyefahamika kwa jina la Shukrani yeye alisoma HGL.

Tukiwa mtoni nilimshirikisha jamaa ule mchongo wa Wini nikamwambi kila kitu na nikamuomba msaada wa mawazo tukajadili na kuafikiana kuwa atanipeleka mtaani usiku tukatafute nguo na kuulizia upatikanaji wa usafiri.

Nilimuuliza tunatorokaje na mageti yote yana ulinzi aliniambia nimuachie yeye ila muhimu nikachukue advance ya kazi kwa dada kwaajili ya hizo nguo, viatu na ikiwezekana nauli kwaajili ya usafiri wa kumpeleka eneo la mbali na kikosi. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

************Itaendelea…………....………...

Oya Alfagems na Kacheda mjasiliamali awamu hii mkija mpitieni na kabwela mwenzangu wa kuitwa Poor boy
 
EPISODE 22

Tulikaa mtoni mpaka ulipofika muda wa chai tukaenda kunywa ila tulipokuwa kwenye foleni wengi walinishangaa na wakanifuata kunielezea kilichotokea.

Kumbe bwana Fadhili aliamkia KOMBANIA baada ya kunikosa usiku wa jana hivyo akaja kuniulizia.

Toka siku hiyo WAZALENDO wenzangu wakaanza kunijua vizuri kwa majina na wajihi baada ya Amosi kuwacharazia kuwa ni yule jamaa aliyepewa UTAWALA siku ile na wale MADAWILI baada ya kujibu kuwa vipara vitatu vitanyolewa kwa dakika sita.

Fadhili aliwaambia kuwa nilimpigia simu nikamuomba anisaidie kutoroka ikabidi aje kunizuia ila alipofika HANGANI hakunikuta hivyo amekuja kuthibitisha kama nimeondoka kweli.

Wapo ambao hawakumuamini maana walimuambia kuwa simu niliibiwa jana hiyohiyo tena asubuhi sasa inawezekanaje nimpigie usiku ila baada ya kutokuniona kwenye usafi na kwenye FATIKI kidogokidogo walianza kumuamini.

Fadhili aliropoka mambo kibao ikafika hatua akayaanika mpaka masuala ya familia yangu na hali ya kimaisha japo mengine hayakuwa na ukweli.

Ilinibidi niwaambie kuwa ni kweli nimetoka naye sehemu moja ila nilikuwa nikiongea naye masihara ni yeye tu ndo kachukulia seriously.

Nilichogundua ni kuwa Fadhili hakuwaambia kuwa nilisoma naye darasa moja na alikuwa kilaza ila alijipakulia minyama kwa kuwa sikuwepo na akahisi nimetoroka kweli hata hivyo nilishukuru maana ni aibu watu kujua nimesoma na kiazi kama kile.

Tulipiga zetu chai na kurudi KOMBANIA ambako number one on tranding ilikuwa ni urejeo wangu kutoka kutoroka.

Walitaka kujua kama simu yangu nimeipata nikawaambia kuwa niliomba simu ya Baraka ambaye kipindi yule kiazi anaongea alijikausha ili kujiepusha na kesi ya kuniasaidia kutoroka.

Afande wa zamu aliniulizia na kuambiwa nipo akataka kujua nilipokuwa asubuhi nikamwambia nilikuwa mtoni akataka anipe DOSO ila aliniambia ni vile tu sipo kwenye SIX WEEK ila angeninyoosha hivyo alinikanya nisirudie tena.

Kwenye soga zetu hapo KOMBANIA afande alituambia kuwa ndivyo jamaa huyo aliyemuita “homeboy wako” alisema ana swaga za kikuda na mbaya zaidi ni kitengo Military Police (MP) wa JKT yaani askari anayesimamia adhabu kwa askari wenzao wanaovunja sheria ama kufanya makosa mbalimbali hivyo huwa anawavimbia sana.

Tulienda zetu kwenye FATIKI ambapo tulipelekwa porini kufuata kuni, tulipokuwa huko muda mwingi nilikuwa na Wini niliyekuwa nikimpanga nilipofikia kuhusu swala lake la kumtorosha.

Jicho la wivu kutoka kwa Linda nalo halikuwa mbali kutokana na ukaribu wangu na Wini kuongezeka siku hadi siku.

Nilipoona anajitahidi kuwa karibu nasi nilimpanga mwamba Shukrani amchomoe wakapige zao ngano za sungura na fisi mbali nasi ili asije akatuharibia mchongo wetu ukawa mchongoma.

Kwa upande mwingine Wini aliniambia kuwa alikuwa so excited aliposikia kuwa mtu ambaye alikuwa akimshauri asitoroke yeye (yaani mimi sasa) ndio kawa wa kwanza kufanya hivyo.

Nilimpanga anipatie advance ya kazi lakini akaniambia kuwa nguo na viatu anavyo kwa hiyo atatoa ya nauli.

Niliwaza kuwa usafiri atakaotumia huenda ukambeba afande anayekwenda mjini hivyo kama akihisi chochote itakuwa ngumu kufanikiwa nikawaza iwepo kofia ya kuziba kichwa nako ikawa hapana maana kwa viburi walivyo navyo maafande si kazi kwao kuwafunua.

Machaguo yakawa mawili tupate wigi na kofia ama tutafute juba litakalomfunika mwili mzima vazi ambalo si rahisi kwa mwanajeshi kupata ujasiri wa kumvua hadharani vinginevyo wasiwepo watu wa itikadi ama wanaharakati wa kupinga jambo hilo ambalo ni la uzalilishaji kwa upande mwingine.

Wazo la kuvaa juba halikuwa jepesi kwake kulikubali nafikiri ni kwasababu za kidini hivyo alikubali wazo la kuvaa wigi japo nilifikiria nikaona wazo la kuvaa juba lilikuwa ni zuri zaidi kuliko la wigi nilimshawishi afanye mara moja kwa ajili ya usalama wetu sisi tunaomsaidia.

Nilitambua kuwa ikitokea amesanukiwa basi sisi wote tumekwisha maana mwanamke ni mwepesi mno kufunguka mpango mzima pale anapobanwa vilivyo hivyo nilitaka swala hili lifanyike kimafia zaidi na lifanikiwe.

Swala lingine ni kuwa alinitonya kuwa baba yake ni wakili japo aliniahidi kwamba atakapofika nyumbani atamalizana naye bila kututaja na atasema ametoroka mwenyewe bila kusaidiwa.

Tulimalizana na kukubaliana kuwa atanipa huo mtonyo muda wa chakula cha jioni maana mpango ulikuwa tuingie mtaani na Shukrani mishale ya saa moja ili saa tatu tuwe tumerudi kwaajili ya kuwahi lokoo.

Ulifika wakati wa chakula TUKAFOLENI zetu kwa MZABUNI kwa ajili ya kupata lakaa ya mwisho Wini alikuja na mazaga niliyomuagiza akaniachia myekundu mitano 💴na simu yake.

Nilimwambia anipe na simu ili nifanye mawasiliano nikiwa shopping na kama kuna kitu kitapelea niwapigie simu nyumbani kwetu waniongezee.

Ukweli haukuwa huo nilitaka tu niyakague malipo yangu baada ya kazi ngumu kama hiyo yaani niikague simu nitakayoachiwa ina ukubwa na uwezo kiasi gani.

Niliviweka mfukoni na kwenda HANGANI ambako tulitupia zetu kiraia na mwanangu Shukrani hatimaye tukaanza kuutafuta mtaa.

Tulitokea kwenye njia moja iliyokuwa karibu na uwanja wa mazoezi wa kikosi yaani wale askari wa kikosi waliokuwa wanapenda mpira walikuwa wakichukulia mazoezi hapo.

Nafikiri Shukrani alipajua kwakuwa alikuwa akija kujumuika nao mimi kidogo ulinipitia kushoto baada kutengua mkono nikiwa kidato cha tatu kwenye interclasses league.

Njia hiyo ilikuwa inakaribiana mno na makazi ya raia na wapo baadhi walikuwa wakijumuika uwanjani kufanya mazoezi ama kweli Shukrani alikuwa kichwa ngumu yaani tayari kwa siku hizo chache alikwisha jua chocho kibao za kutorokea.

Hiyo ilikuwa ni kawaida yake tangu tukiwa shule alikuwa akikesha sana kwenye vigodoro na kumbi za starehe.

Tulimaliza mitikasi yetu majira ya saa tatu kama tulivyopanga ila hatukufanikiwa kupata juba hivyo mwenye duka alituambia kuwa kesho yake yatakuwepo maana kaagiza mzigo mpya wenye majuba na kesho yake ndiyo anaufuata.

Tulirudi zetu kambini huku tukiizungumzia simu ya bi dada Wini kwa kweli nilitakiwa niongeze juhudi zaidi ili niipate sitokwambia ilikuwa ni simu ya aina gani ila chukua hii ilikuwa ni simu ya mtoto wa wakili we kariri neno “mtoto wa wakili”.

Shukrani alianza kuipigia hesabu kuwa tukiiweka mikononi basi tutaiuza na kugawana niliona kuwa tunaenda kuvurugana nikampa tahadhari kuwa tusiamini sana huenda labda ana nyingine ndo atatuachia hii katupa tu tutamani kufanya kazi yake.

Hata hivyo hakuniambia atanipa simu gani ila alisema ataniachia simu yake pengine akanipa hela ninunue simu maana kama anayo moja hawezi kusafiri bila mawasiliano.

Baada ya maelezo hayo nilimuona mwamba kanyweya akasema “ole wako mwisho wa picha unikatae hakuna rangi utaacha ona”. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

**************Itaendelea………………........……...
 
Ulifika wakati wa chakula TUKAFOLENI zetu kwa MZABUNI kwa ajili ya kupata lakaa ya mwisho Wini alikuja na mazaga niliyomuagiza akaniachia myekundu mitano na simu yake.

EPISODE 23

Nilikuwa nikiziona simu nyingi kutoka nyumbani na jumbe za kutosha zikiingia ila nilizipotezea kutokana na mazingira tuliyo nayo kwa muda huo.

Tulisepa zetu KOMBANIA na kuwakuta wakipiga makelele nilijaribu kumtafuta Wini ila sikumuona maana watu tulishakuwa wengi tulifika zaidi hata ya buku mbili.

Nilikuja kumuona dakika za jioooni kabisa na wakati huo tulikuwa tunahesabu namba yeye alisimama kama mtu wa kumi katika yale mafungu ya watu kumikumi.

Sikuweza kumsogelea maana wakati huo maafande hawakuruhusu kabisa mjongea wa mtu yeyote kwani angeweza kuvuruga mahesabu.

Niliishia kumkariri alipo akiwa amesimama ila baada ya kukaa chini wote vimo vilikuwa sawa hivyo nikampoteza na ikawa ngumu kumuona hali hiyo iliendelea mpaka pale tuliporuhusiwa.

Nilipojaribu kumsogelea pale alipo tayari watu wote walikuwa wameamka hivyo kukawa na muingiliano uliofanya nimpoteze kabisa na mwisho wa mkanda nilitoka kapa.

Nilipitia zangu bwaloni kumtafuta Matroni Anna ambaye nilimuona lakini alikuwa yupo katikati ikawa vigumu kumfikia pale alipo.

Ni vile hajui tu ila siku ile ilikuwa ni zaidi ya muhimu kuonana naye kwani nilikuwa na bonge la simu mkononi nilichukulia kama fursa ya kumtegea ulimbo.

Sikuwa na namna nilirudi zangu HANGANI ambako bado nyumbani walikuwa wakinitafuta kwenye simu ikanibidi kupokea na kuongea nao.

“Halo baba mzima wewe”
“Ndiyo mi mzima shikamoo mama”
“Marhaba mwanangu tupo mezani hapa nimeweka loud speaker wanakusikia tuna hofu tangu jana tulipigiwa simu na Fadhili wa Mzee Mziwanda anasema eti umetoroka jeshini ni kweli baba yangu na umefika wapi tuje tukuchukue”.

Alikuwa ni mama ambaye alikuwa akiongea nami kwa mapenzi ya mzazi na mwanawe ambapo nafikiri angekuwa ni Mzee Mjuzi angekuwa anafoka hovyo na ningekwisha mkatia simu kitambo tuu maana sitaki stress na mtu wakati huu.

Tuliendelea kuongea na kumjibu “Hapana sijatoroka mama niko kambini jana nilikuwa namtania tu huyo mtu sema naona yeye kachukulia seriously”
“Kweli baba yangu”
“Ndiyo mama niamini”
“Na mbona tumempigia mchana akasema alikuja sijui ndo huko KOMBANIA mnako lala akakukosa”.

Nilicheka 😄na kumwambia “Kumbe unajua hadi na KOMBANIA nani huyo kakufundisha”

“Si ni huyo Fadhili wakati anaongea na baba yako jana nilikuwa naye nayeye aliweka loud speaker” alinijibu bi mkubwa.

Nilimwambia “sawa bana ila tunakolala kunaitwa HANGANI huko KOMBANIA ni kama mstarini ndiko tunakokusanyika” “Anhaah sawa haya tuambie ilikuwaje sasa mpaka akakukosa”.

Licha ya kumzuga bado alitaka kujua nikamjibu “Kipindi anakuja mimi nilienda mtoni kufua mama”.

Nilisikia sauti ya mshua ikiropoka “Muongo ameshindwa kutoroka amejuaje kama alimfuata wakati hukuwepo” alianza kunitoa mchezoni.

Nilianza kupaniki 😡nikamjibu kwa jazba “Niliporudi mtoni ndiyo niliambiwa kuwa aliniulizia mi sijatoroka baba”.

Nilimsikia mama akimwambia mzee “Usiwe hivyo baba Uledi basi hembu jaribu kumsikiliza mtoto usimkasirishe” nilijikuta nakata simu na kuizima.

Asubuhi niliamka nikatoa laini ili nimpelekee mwenye simu yake ila hatukubahatika kuonana ikanibidi nirudi nayo.

Baada ya MABIO nilienda zangu mtoni kuoga maana kwa mishemishe zilizopo kwenye mabomba nilijua kuwa ni vigumu kutoboa.

Nikiwa mtoni mama alinipigia nikapokea “Umeamkaje baba”
“Salama mama shikamoo”
“Marhaba baba yangu jana hatukumaliza mazungumzo ila usijali sasa hivi niko peke yangu huku uani baba yako bado kalala”
“Usijali mama wala sikukata kwa ajili yake isipokuwa simu siyo yangu nilimrudishia mwenyewe maana alikuwa anapigiwa”.

Nilimbutua na kitu kizito bi mkubwa akashangaa baada ya kumueleza kuwa simu yangu imeibiwa na nimebaki na laini hivyo huwa naombaomba kwa watu.

Nilimwambia kuwa wasiponipata wasishangae inawezekana muda huo nimetoa laini kwenye simu ya watu ama simu iko kwa mwenyewe ambaye hawezi kupokea simu zangu.

Licha ya kuniahidi kunitumia hela ninunue simu nyingine pia alinitonya kuwa tupunguze utani na Fadhili maana Mzee Mziwanda ambaye ni babaake na Fadhili yule afande kiazi ameanza kusambaza taarifa kuwa nimelishindwa jeshi kwahiyo nimetoroka tofauti na mwanaye ambaye ameakaza na mpaka leo yupo.

Moyoni nilijiambia kuwa kumbe kile kiazi haya mambo ameyarithi kutoka kwa baba yake ama kweli nyoka hazai kenge.

Nilitimba KOMBANIA nikaonana na Wini na kumuelezea hali ilivyokuwa alisikitika sana na kusema kuwa ni kheri tungechukua hata hilo wigi maana hatamani kabisa kuendelea kuwepo.

Nilimpa matumaini na kumwambia avumilie kwani ifikapo jioni ya siku hiyo tungeenda tena hivyo basi tukifanikiwa basi kesho yake asubuhi na mapema safari ni uhakika mana tukikosa juba tutachukua hata hilo wigi kifupi kesho yake itakuwa ni “do or die”.

Alinielewa nikamrejeshea simu yake mwanzo aligoma akitaka nikae nayo maana imeshakuwa yangu ila nilimgomea na nikamweleza siwezi kuchukua bila kukamilisha kazi yake kwani simu niliyoibiwa ni kwasababu nilishindwa kuitunza kwahiyo wanaweza wakaiiba na hiyo kabla sijafanikisha kazi yake haitokuwa sawa.

Idadi ya watu ilizidi kunona kiasi kwamba kukawa na ugumu kutukusanya pamoja na kutusimamia pia hivyo basi baada ya kula chakula cha mchana TULIFOLENI wote UWANJA WA DAMU.

Lengo la kufanya hivyo lilikuwa ni zoezi ambalo tulipanga mistari kibao isiyo na idadi tukahesabu namba moja mpaka nne mimi nikiwa namba tatu.

Baada ya kutuhesabu wakatoa dakika kumi za kuvurugana yaani kila mwenye namba yake alitakiwa kumfuata afande aliyeelekezwa ambaye tulitambulishwa kuwa atakuwa karani wetu.

Mimi nilienda sehemu aliyokaa afande Jala ambaye kama unakumbuka ndiye aliyetupatia magodoro ile siku tunawasili kikosini.

Walitoa majina ya makundi hayo ambapo wale walioitika namba moja walienda kwa karani Shashuda na kundi hilo liliitwa KOMBANIA ya chui (ila siyo huyu vannyboy).

Walioitika namba mbili waliitwa tembo, sisi namba tatu tuliitwa twiga na namba nne aliyoangukia Linda ilikuwa ni simba.

Afande jala alitupa utaratibu namna ya kukaa pale tutakapokusanyika alituhesabu namba zilizotoa makundi matatu yaliyofahamika kama PLATUNI kwakuwa nilihesabu namba moja nikawa PLATUNI ya kwanza.

Katika kila PLATUNI kulikuwa na makundi matatu yaliyoitwa SECTION namimi nilikuwa SECTION ya pili tukajipanga katika hali ya kutengeneza umbo la pembe nne (mstatili au mraba) ambalo upande mmoja ulikuwa wazi.

Pande hizo tatu zilizobaki zilikuwa ni PLATUNI ambapo ile ya kwanza ilitizamana na ya tatu na ile ya pili ilitizamana na upande uliokua wazi ambao karani wetu aliweka kiti chake na meza akawa anachukua idadi na kuorodhesha majina kwenye daftari lake la kumbukumbu.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

**************Itaendelea…………..........………...

Oya MombaDier hembu waite wenzako waambie huku kumeshakuwa kunavyotakiwa kuwa.
 
EPISODE 24

Katika mazingira yasiyo ya kutarajia kilifanyika kitu cha ajabu na chenye kushangaza katika KOMBANIA hiyo iliyokuwa chini karani Jala kulifanyika uchaguza wa ST.

Kitu cha kushangaza ni kuwa walinichagua niwe ST sikujua ni kigezo kipi walichokitumia lakini uhakika niliokuwa nao ni kuwa umaarufu pekee ndiyo uliyoniponza.

Sikuwa peke yangu pia alichaguliwa DAWILI aliyeitwa Aisha ambaye kama utakumbuka siku moja tukiwa KOMBANIA tunaimba wimbo uliokua unauliza majina yetu na tunakotoka alisema anatokea Mtwara.

Tukiachana na hilo usilolijua ni kwamba katika moja ya wale niliopangwa nao KOMBANIA hiyo alikuwa ni Wini ambaye kipindi tunahesabu alikuwa mbali na sisi Linda yeye aliangukia KOMBANIA ya simba kwasababu alikuwa ameniganda kwahiyo nilipohesabu tatu yeye akahesabu nne.

Jioni ilifika tukafanya kama tulivyopanga ila kwa mara nyingine hatukufanikiwa kupata juba ikabidi tucheze plan B ya wigi na kofia tukarudi zetu kikosini na baadaye tukaenda KOMBANIA.

Jioni hii KOMBANIA ilihama kutoka pale pa siku zote na kwenda UWANJA WA DAMU ambako kulikuwa na nafasi kubwa tofauti na pale jikoni haswa kwa ukaaji ule wa KIPLATUNI tusingetosha ilikuwa ni sahihi kwenda kukalia UWANJA WA DAMU.

Mwanzoni kipindi tunafika tulipagawa kidogo maana tulijua wenzetu WAMEFOLENI pale pa siku zote ila hatukuwakuta tukaenda bwaloni nako hawakuwepo ndipo nilikutana na matroni Anna.

Kwa kuwa muda ulikuwa una ruhusu sikuwa na woga nilimuita kuongea naye bahati nzuri hakuwa na makuu alikuja tukaongea.

Ni kama damu zilikuwa zikikimbia kwenye mrija mmoja kwa kweli tulijikuta tunaelewana bila kujali gepu lililopo kati yetu kwamba yeye ni SM na mimi ni KURUTA.

Nilimpanga matron na kumwambia kila siku nikija namkuta yupo katikati hivyo nashindwa kumuita alinielewa akanipa namba yake ili niwe namtafuta.

Kipindi anatoa namba nilikuwa na simu ya Wini mkononi hivyo nilijichukulia maujiko kwani aliniomba aione nikampa sijui ni sehemu zipi alikuwa anaangalia ila nilimsikia akiwa anaguna tu na baadaye alinirudishia.

Baada ya zoezi hilo nilimuomba anielekeze walipo WAZALENDO alinishangaa akanihoji ni kwanini sijui nikamdanganya kuwa
“Nilipitiwa na usingizi nilipoamka sikuwakuta pale tunapokaa siku zote na ndiyo ikawa sababu ya kuja kuwaangalia bwaloni kumbe Mungu alikuwa na makusudi yake huoni sasa nimekutana na malaika wake”.

Alijigunisha na kukaa kimya kwa sekunde kadhaa nikamsikia akisema
“Kumbe nawewe mpana sikutegemea ungekuwa muongeaji hivyo”.

“Aah ni kweli na uko sahihi ila hali hii hunitokea pale tu ninapokuwa na wewe najikuta maneno yananitoka mfululizo”
“Mnnh kweli”
“Ndiyo amini usiamini”
“Hunidanganyi we MZALENDO mstaafu”
“Amini kwamba sikudanganyi hata kidogo yaani nikiongea nawewe ni kama roho mtakatifu ananishukia najikuta nikinena kwa lugha mbele yako”.

Yule dada wa watu alijikuta akiangua kicheko kilichowashtua walio karibu yetu akasema “Ila wewe ni muongo sijapata kuona duka liko kule nakukuta huku unasema umekuja dukani haya nenda kwa wenzako UWANJA WA DAMU chap kwa haraka”.

Kauli hiyo inaonekana ni kana kwamba haiendani na mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea ila niliweza kumuelewa Matron kuwa alikuwa akizuga baada ya watu kumzingatia kutokana na kicheko chake.

Kupitia maneno yake nikakumbuka kitu kuwa baada ya kuorodhesha majina mchana kwa karani Jala alituambia jioni TUTAFOLENI hapo hapo badala ya kule jikoni.

Tukatimba zetu UWANJA WA DAMU nikiwa na mwanangu Shukrani aliyekuwa akinisubiri kipindi nayajenga na Matroni tukiwa njiani jamaa alitaka kujua kama nilikuwa nikimtongoza nikamkatalia.

Jamaa akaniambia kwa namna alivyomuona ni kama keshaingia kwenye kumi na nane kwahiyo ilikuwa ni mimi tu kutupa ndoano kivue kitoweo.

Pale KOMBANIA nilimtafuta Wini ambaye alikuwa yuko PLATUNI namba tatu, kusema kweli utarabibu wa kukaa hivi ulirahisisha namna ya kumpata uliyemhitaji.

Nilimueleza namna ilivyo na kumpanga kuwa ajiandae maana asubuhi yake kinanuka, alifurahi mno na alinipiga bonge la busu lililowashtua wengi wao.

Jambo la kushukuru ni kwamba muda huo hakukuwa na afande yeyote KOMBANIA hivyo tulijitenga zetu pembeni kwa hiyo hawakushtuka wengi tofauti tungekaa kwenye PLATUNI zetu ingekuwa jau.

Wini alinipongeza na kuniambia kuwa tangu siku ya kwanza aliamini kuwa naweza kufanya hiyo na ndiyo maana aliniamini na kuniambia hakujua tu nyuma ya hayo yote master mind alikuwa ni swahiba wangu Shukrani bila yeye nisingetoboa.

Katika kuuchora mpango wa namna itakavyokuwa tukagundua kuwa binti alikuwa na sanduku lake je litaondokaje maana akisema atoke nalo asubuhi watu watamshtukia.

Wakishua ni wakishua aliutegua mtego huo kwa akili ndogo sana na kusema kwake siyo shida anachotaka yeye ni kuondoka tu kuhusu hilo sanduku ataliacha ikimbidi.

Tuliruhusiwa na kurudi HANGANI nikachukua simu ya Baraka na kuweka laini yangu kisha nikumrukia matron ambaye niliziona dalili za udhaifu namimi nikataka kuutumia udhaifu huo kwani wahenga walikwisha sema “Kamba hukatikia kwenye ubovu”.

Kwenye mazungumzo yetu topic ilikuwa ni ileile Katerero ni kitu gani matron alisema kuwa angeniambia lakini siyo kwa njia ya simu labda tukionana ana kwa ana.

Nilimkumbusha kuwa tulionana na akashindwa kunieleza aliniambia kuwa ni kweli ila asingeweza kuniambia sehemu ya wazi vile hivyo ikabidi nimuulize angekuwa tayari kuniambia wapi na sehemu gani.

Matroni alinishangaza jibu lake alisema kuwa natakiwa kwenda zilipo hostel zao yaani MAHANGA ya MADAWILI sijui kama alisema hivyo makusudi ama alisema akijua sitoweza kwenda huko.

Wakati yakiendelea hayo tayari mzee wa ngezi alikuwa kanyooka haswa nikimaanisha kichwa cha chini, matron aliniuliza kama ningeweza kufanya hivyo nikamwambia kuwa hiyo ni kazi ndogo sana.

Kwakuwa Abdala kichwa wazi alikuwa akiutaka nikamwambia kuwa hata sasa hivi akitaka niko tayari kwenda.

Alinitaka niache papara kwani kwa wakati huo ni vigumu na wanakuwa kwenye ulinzi mkali muda mzuri ulikuwa ni baada ya sisi kuruhusiwa pale MADAWILI wakiingia ama wao wanapotoka kuangalia tv hivyo labda kesho yake.

Tulimalizana na kukata simu nami nikamrudishia simu Baraka na kulala zangu kuuendea muda wa kazi maalum ya kimafia na kinyabumbu. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

****************Itaendelea……..…………….......
 
EPISODE 25

Basi ulifika muda wa MABIO tukaenda eneo mahsusi nikiwa na Shukrani kwaajili ya mission yetu ila cha kushangaza binti hatukumuona na kwenye simu hatukumpata.

Shukrani alimaindi na akasema kuwa ndivyo inavyokuwa ukifanya mission za hatari na wanawake na ndiyo maana tangu yuko shule hajawahi kutoroka na wanawake zaidi ya masela.

Nilimtuliza na kumwambia inabidi tujue kwanza kilichomkuta kabla ya kumlaumu hivyo angetulia kukuche tutapata majibu ilimradi hatujashtukiwa hakuna sababu ya kujiogopesha.

Shukrani alikuwa akiwaza sana maana kuna bodaboda tulimpanga amchukue binti huyo kwa lengo la kumfikisha mjini mapema kabla hata maafande hawajaanza kusafiri.

Amini usiamini hili dili tulilisuka haswa tulichukua kila tahadhari iliyostahili.

Bodaboda akawa anatupigia kupitia simu ya Shukrani ambaye aliogopa kuipokea, niliichukua na kuongea naye nilimdanganya kuwa binti alishtukiwa kipindi anatoka hivyo mchongo umebuma.

Nilimtoa hofu kuwa asijali hata kama akitutaja sisi yeye hatutomtaja kabisa hivyo aendelee kula mtori kwa mbege.

Mshikaji alielewa ingawaje alisikitika kupoteza dili la shilingi kumi na tano za kibongo ambazo alisema
“Daah wanangu mmenikosesha hesabu ya bosi ya siku mbili, leo nilikuwa nalala zangu saa tano asubuhi”.

Kulipambazuka vizuri na tukaelekea zetu KOMBANIA ambako nilimtafuta binti wa wakili na sikumuona.

Afande Jala alikuja kuchukua lokoo akiwa na afande Mbega ambaye alituambia kitendo cha kupangwa KIKOMBANIA ni ishara mbaya mno hivyo tujiandae kwa ajili ya siku inayoitwa “Introduction to the camp”.

Neno hilo lilinikumbusha nikiwa mdogo kwenye banda la video nilipokuwa nikitizama muvi za kivietinam zilizotafsiriwa na nguli mwamba kabisa Lufufu Mkandara.

Kwenye lokoo aliyochukua afande Jala alichukua list ya walinzi wa HANGA na wagonjwa ambapo taarifa za Wini ziliangukia upande wa wagonjwa kumbe bwana dada wa watu alishikwa sana usiku.

Usiku tuliporuhusiwa nilimpandia hewani Matron Anna ambaye aliniambia tukutane sehemu nami nikaenda matroni alinipa sweta lake na kanga ambayo sikuivaa alisema nijifunike mabegani chini nikabaki na suruali yangu ya track.

Kwa upande wa matron alikuwa na tisheti yake maarufu kama GREEN VEST basi tukatiririka zetu mpaka yalipo MAHANGANI kwao ambayo hayakuwa mbali na UWANJA WA DAMU.

Tulifika MAHANGANI na hatimaye chumbani kwake ambako niligundua kuwa MAHANGA yao yalikuwa tofauti kabisa na ya kwetu maana ya kwao yalikuwa hadi na vyumba.

MAHANGA ya kiume tuliyokuwa tukiitwa NGORONGORO yalikuwa ni bwalo lisilo na chumba na hata hivyo kuta zake zilikuwa zimejengwa kwa mabati.

Matroni alinisisitiza kutokujiachia wala kutotoa sauti kubwa kwenye chumba hichoambacho kilikuwa na deka iliyomaanisha kuwa wanakaa wawili ila mwenzie hatukumkuta.

Tulipiga stori kwa muda kisha akaniambia tuondoke kabla mwenzake hajarudi nilizuga sijamsikia nikamkumbusha kuhusu Katerero aliniambia atanionesha siku nyingine (elewa neno atanionesha siyo ataniambia siku nyingine😜) kwani siku hiyo hakujipanga.

Neno hajajipanga lilinipa ujasiri wa kumuuliza hajajipangaje wakati siku zote topic ilikuwa ni hiyohiyo akasema kuwa siku hiyo amefanya hivyo ili aone kama nina ujasiri wa kufika huko kwahiyo nimpe muda ataniita siku nyingine.

Siku iliyofuata tukiwa KOMBANIA tulikuwa na Wini msichana pekee kwenye picha letu la mission impossible alisema kwamba usiku ule lilimshika tumbo la period hivyo ilikuwa ni vigumu kuondoka katika hali ile.

Aliendelea kusema kuwa ilimbidi azime simu kwani kulikuwa na watu waliokuwa wakimuangalia hivyo aliogopa huenda wangemsaidia kupokea ukawa msala nilimpongeza mno kwa kujiongeza kwake.

Wini alini surprise kwa kuniambia kuwa ule mpango wa kutoroka nao ameufuta ameufungua moyo na yuko tayari kubaki kipindi chote cha mafunzo.

Kusema kweli alinifanya nimshangae nisijue kapatwa na kipi maana kuumwa tumbo pekee haiwezi kuwa sababu ya kupindua maamuzi kwa haraka hivi.

Aliponiona kwenye hali hiyo aliniambia “Worry out K najua unawaza kuhusu simu ila usijali nitakupa hela ukatafute nyingine mtaani I am so sory dear”.

Nilimjibu “Hapana Wini sikufanya hivyo kwa ajili ya malipo (nadanganya nilikuwa nalitaka tambo sana tu ☺)”.

Nikaendelea kusema “Nimefanya hivyo kutokana na kisa chako ujue hata mimi baba alinilazimisha sikupenda kabisa kuja huku na ile siku unaniambia ni kama ulikuwa unapakaza chumvi kwenye kidonda hivyo nikaona nikusaidie ili siku nyingine usije nitonesha kidonda change kinachokaribia kupona”.

Kadri siku zilivyokuwa zinasonga ndivyo ndivyo mambo yalivyokuwa yanazidi kuwa magumu hali hii ilipelekea baadhi ya watu waliokosa uvumilivu kutoroka.

Ukaribu baina yangu na Wini ukawa unaota mizizi hali iliyomfanya kujisikia amani maana sikuwahi kumsikia tena akiropoka neno kutoroka hata tulipokuwa tukipewa kazi ngumu ingawaje alikuwa akisafiria sana upepo wa cheo changu.

Siku moja tulikuwa na FATIKI ya kuvuna mahindi ya shamba la kikosi ambalo lilikuwa liko umbali wa kilomita zaidi ya nane kutoka makao makuu ya kikosi.

Kwenye shamba hilo ilikuwepo na kambi ndogo ambayo nafikiri ilikuwepo kwa ajili ya kusimamia usalama wa mazao na mashamba kwa ujumla kwani wahuni siyo watu.

Tukiwa katika kipindi cha mavuno ya zao hilo mama la taifa tulikuwa tukiamka muda wa MABIO na moja kwa moja tunazikata kilomita tukiwa na ndoo zetu mpaka shambani.

Kule shambani mara nyingi tulikuwa tukienda na mzee mmoja aliyekuwa maarufu sana kwa jina la Halichachi wakimfananisha na kilichokuwa kifurushi cha mtandao wa tigo.

Sifa ya mzee huyo ambaye cheo chake alikuwa ni msimamizi wa maswala ya nidhamu kikosini alikuwa halazi kazi yaani ni mpaka iishe ndiyo aidha mpumzike ama mle.

Kitu kibaya zaidi chakula kilikuwa kikitolewa kikosini tu waliokuwa wakila hapo ni wale waliokuwa wakikaa kwenye kambi hiyo sisi wengine ilitulazimu kutembee tena hizo kilomita mpaka kikosini.

Kuna baadhi ya siku tulikuwa tukiinywa chai mishale ye saa saba yaani tunamaliza kazi saa tano alafu tunatakiwa kutembea mwendo wa masaa mawili tukisubiriana tufike wote ndiyo chai itolewe.

Katika kitu cha kuhatarisha ni kuwa tulikuwa tukirudi na kiu kikali na moja kwa moja tulifikia kwenye matenki yaliyopo karibu na jiko na kufakamia mimaji kabla ya kunywa ingawaje maafande walikuwa wakitushauri kuwa tunywe kwanza chai lakini ilikuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

*************Itaendelea………….......…….........

Oya we jamaa wa 88 Alfagems, mtu wa Mungu MombaDier, kabwela mwenzangu Poor boy na jamaa wa fursa Kacheda mjasiliamali, sogeeni jamvini.

Ila kusema kweli nimeimiss reply ya realMamy na ile NICE ya Numbisa 😁
 
MAISHA YA DEPO

SEASON-2

EPISODE 25

Basi ulifika muda wa MABIO tukaenda eneo mahsusi nikiwa na Shukrani kwaajili ya mission yetu ila cha kushangaza binti hatukumuona na kwenye simu hatukumpata.

Shukrani alimaindi na akasema kuwa ndivyo inavyokuwa ukifanya mission za hatari na wanawake na ndiyo maana tangu yuko shule hujawahi kutoroka na wanawake zaidi ya masela.

Nilimtuliza na kumwambia inabidi tujue kwanza kilichomkuta kabla ya kumlaumu hivyo angetulia kukuche tutapata majibu ilimradi hatujashtukiwa hakuna sababu ya kujiogopesha.

Shukrani alikuwa akiwaza sana maana kuna bodaboda tulimpanga amchukue binti hiyo kwa lengo la kumfikisha mjini mapema kabla hata maafande hawajaanza kusafiri.

Amini usiamini hili dili tulilisuka haswa tulichukua kila tahadhari iliyostahili. Bodaboda akawa anatupigia kupitia simu ya Shukrani ambaye aliogopa kuipokea, niliichukua na kuongea naye nilimdanganya kuwa binti alishtukiwa kipindi anatoka hivyo mchongo umebuma.

Nilimtoa hofu kuwa asijali hata kama akitutaja sisi yeye hatutomtaja kabisa hivyo aendelee kula mtori kwa mbege.

Mshikaji alielewa ingawaje alisikitika kupoteza dili la shilingi kumi na tano za kibongo ambazo alisema
“Daah wanangu mmenikosesha hesabu ya bosi ya siku mbili, leo nilikuwa nalala zangu saa tano asubuhi”.

Kulipambazuka vizuri na tukaelekea zetu KOMBANIA ambako nilimtafuta binti wa wakili na sikumuona.

Afande Jala alikuja kuchukua lokoo akiwa na afande Mbega ambaye alituambia kitendo cha kupangwa KIKOMBANIA ni ishara mbaya mno hivyo tujiandae kwa ajili ya siku inayoitwa “Introduction to the camp”.

Neno hilo lilinikumbusha nikiwa mdogo kwenye banda la video nilipokuwa nikitizama muvi za kivietinam zilizotafsiriwa na nguli mamba kabisa Lufufu Mkandara.

Kwenye lokoo aliyochukua afande Jala alichukua list ya walinzi wa HANGA na wagonjwa ambapo taarifa za Wini ziliangukia upande wa wagonjwa kumbe bwana dada wa watu alishikwa sana usiku.

Usiku tuliporuhusiwa nilimpandia hewani Matron Anna ambaye aliniambia tukutane sehemu nami nikaenda matroni alinipa sweta lake na kanga ambayo sikuivaa alisema nijifunike mabegani chini nikabaki na suruali yangu ya track.

Kwa upande wa matron alikuwa na tisheti yake maarufu kama GREEN VEST basi tukatiririka zetu mpaka yalipo MAHANGANI kwao ambayo hayakuwa mbali na UWANJA WA DAMU.

Tulifika MAHANGANI na hatimaye chumbani kwake ambako niligundua kuwa MAHANGA yao yalikuwa tofauti kabisa na ya kwetu maana ya kwao yalikuwa hadi na vyumba.

MAHANGA ya kiume tuliokuwa tukiitwa NGORONGORO yalikuwa ni bwalo lisilo na chumba na hata hivyo kuta zake zilikuwa zimejengwa kwa mabati.

Matroni alinisisitiza kutokujiachia wala kutotoa sauti kubwa kwenye chumba hichoambacho kilikuwa na deka iliyomaanisha kuwa wanakaa wawili ila mwenzie hatukumkuta.

Tulipiga stori kwa muda kisha akaniambia tuondoke kabla mwenzake hajarudi nilizuga sijamsikia nikamkumbusha kuhusu Katerero aliniambia atanionesha siku nyingine (elewa neno atanionesha siyo ataniambia siku nyingine😜) kwani siku hiyo hakujipanga.

Neno hajajipanga lilinipa ujasiri wa kumuuliza hajajipangaje wakati siku zote topic ilikuwa ni hiyohiyo akasema kuwa siku hiyo amefanya hivyo ili aone kama nina ujasiri wa kufika huko kwahiyo nimpe muda ataniita siku nyingine.

Siku iliyofuata tukiwa KOMBANIA tulikuwa na Wini msichana pekee kwenye picha letu la mission impossible alisema kwamba usiku ule lilimshika tumbo la period hivyo ilikuwa ni vigumu kuondoka katika hali ile.

Aliendelea kusema kuwa ilimbidi azime simu kwani kulikuwa na watu waliokuwa wakimuangalia hivyo aliogopa huenda wangemsaidia kupokea ukawa msala nilimpongeza mno kwa kujiongeza kwake.

Wini alini surprise kwa kuniambia kuwa ule mpango wa kutoroka nao ameufuta ameufungua moyo na yuko tayari kubaki kipindi chote cha mafunzo.

Kusema kweli alinifanya nimshangae nisijue kapatwa na kipi maana kuumwa tumbo pekee haiwezi kuwa sababu ya kupindua maamuzi kwa haraka hivi.

Aliponiona kwenye hali hiyo aliniambia “Worry out K najua unawaza kuhusu simu ila usijali nitakupa hela ukatafute nyingine mtaani I am so sory dear”.

Nilimjibu “Hapana Wini sikufanya hivyo kwa ajili ya malipo (nadanganya nilikuwa nalitaka tambo sana tu ☺)”.

Nikaendelea kusema “Nimefanya hivyo kutokana na kisa chako ujue hata mimi baba alinilazimisha sikupenda kabisa kuja huku na ile siku unaniambia ni kama ulikuwa unapakaza chumvi kwenye kidonda hivyo nikaona nikusaidie ili siku nyingine usije nitonesha kidonda change kinachokaribia kupona”.

Kadri siku zilivyokuwa zinasonga ndivyo ndivyo mambo yalivyokuwa yanazidi kuwa magumu hali hii ilipelekea baadhi ya watu waliokosa uvumilivu kutoroka.

Ukaribu baina yangu na Wini ukawa unaota mizizi hali iliyomfanya kujisikia amani maana sikuwahi kumsikia tena akiropoka neno kutoroka hata tulipokuwa tukipewa kazi ngumu ingawaje alikuwa akisafiria sana upepo wa cheo changu.

Siku moja tulikuwa na FATIKI ya kuvuna mahindi ya shamba la kikosi ambalo lilikuwa liko umbali wa kilomita zaidi ya nane kutoka makao makuu ya kikosi.

Kwenye shamba hilo ilikuwepo na kambi ndogo ambayo nafikiri ilikuwepo kwa ajili ya kusimamia usalama wa mazao na mashamba kwa ujumla kwani wahuni siyo watu.

Tukiwa katika kipindi cha mavuno ya zao hilo mama la taifa tulikuwa tukiamka muda wa MABIO na moja kwa moja tunazikata kilomita tukiwa na ndoo zetu mpaka shambani.

Kule shambani mara nyingi tulikuwa tukienda na mzee mmoja aliyekuwa maarufu sana kwa jina la Halichachi wakimfananisha na kilichokuwa kifurushi cha mtandao wa tigo.

Sifa ya mzee huyo ambaye cheo chake alikuwa ni msimamizi wa maswala ya nidhamu kikosini alikuwa halazi kazi yaani ni mpaka iishe ndiyo aidha mpumzike ama mle.

Kitu kibaya zaidi chakula kilikuwa kikitolewa kikosini tu waliokuwa wakila hapo ni wale waliokuwa wakikaa kwenye kambi hiyo sisi wengine ilitulazimu kutembee tena hizo kilomita mpaka kikosini.

Kuna baadhi ya siku tulikuwa tukiinywa chai mishale ye saa saba yaani tunamaliza kazi saa tano alafu tunatakiwa kutembea mwendo wa masaa mawili tukisubiriana tufike wote ndiyo chai itolewe.

Katika kitu cha kuhatarisha ni kuwa tulikuwa tukirudi na kiu kikali na moja kwa moja tulifikia kwenye matenki yaliyopo karibu na jiko na kufakamia mimaji kabla ya kunywa ingawaje maafande walikuwa wakitushauri kuwa tunywe kwanza chai lakini ilikuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

*************Itaendelea………….......…….........

Oya we jamaa wa 88 Alfagems, mtu wa Mungu MombaDier, kabwela mwenzangu Poor boy na jamaa wa fursa Kacheda mjasiliamali, sogeeni jamvini.

Ila kusema kweli nimeimiss reply ya realMamy na ile NICE ya Numbisa 😁
Unachelewesha sana Story we kijana 😜 ila haya mambo yangenipata kule Songea kama ningeenda 🤭
 
Back
Top Bottom