Maisha ya jamii ya JamiiForums yako poa sana kuliko jamii ya Twitter, Facebook na Insta

Maisha ya jamii ya JamiiForums yako poa sana kuliko jamii ya Twitter, Facebook na Insta

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
JamiiForums ni jamii moja maridhawa mno, ambamo watu watakuonyesha tabia zao halisi zaidi ukilinganisha na jamii nyingine za mtandaoni.

Kwasababu wengi wanatumia majina kificho na picha kificho hapa JamiiForums imekuwa ni rahisi kuonywa kwa kupewa makavu laivu, tabia zako na mambo yako ya hovyo yote yanawekwa peupe, u unachanwa bila ganzi. Hiari ni yako ubadilike au uendelee kuoza.

Huko kwingine unafiki mwingi sana, uwongo uwongo na kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa.

Poa hapa jukwaani licha ya kwamba hatufajamiani, pia tunapendana na wapo wanaowachukia wenzao, Mi sina ninayemchukia, ulinizingua nakuroga tu, usiku mmoja unakuja kunilimia shambani kwangu kama mjombake UMUGHAKA na Emma walivyolimishwa na Mzee MAKONO.

Hapa na kuto onana/kufahamiana pamesaidia sana watu, hasa kwenye michongo ya kazi na deals mbalimbali.

Pia hapa pametoa connections na networks za maana sana.
Almost Tanzania nzima nina ndugu, nikiwepo tu Dar, nikitaka nyama na kichuri namtafuta rafiki yangu GENTAMYCINE, nikitaka mdudu simu ni moja tu Mshana Jr popote ulipo naomba muda wako, Bill Lugano my dearest brother atanipa kila ninachohitaji, na nikitaka kuzama kwenye books shelf namtafuta GuDume.

Yaani hapo ni wachache tu, bado sijaorodhesha warembo wenye akili zao za darasani, maisha na roho nzuri.

Moisemusajiografii na Kasie I miss you. Jiandaeni kunipokea hapo Tazara Station nakuja na treni ya Wakalamba ya Express Jumanne
 
JamiiForums ni jamii moja maridhawa mno, ambamo watu watakuonyesha tabia zao halisi zaidi ukilinganisha na jamii nyingine za mtandaon...
Uje na michembe,matobholwa na vibambara. Pitia hapo Kirumba Valley unichukulie unga wa udaga.Nimemiss sana hayo mambo.Fanya hima uje.Dalisalama joto.Utapanda bajaj upigwe na kaupepo.
 
Ningekuwa na mamlaka ningetoa PhD kwa mmiliki wa jf melo na masudi kipanya, nadhani mnawaelewa kazi zao ni very creative.
Kwani aliyempa PhD ya mchongo mama yao alikuwa na mamlaka gani?

Tukubaliane tu hapa tuwape PhD Melo na wadau wote nguli wa jf kwa kuupiga mwingi.

Nb
Binafsi jf ni pahali pangu pendwa pa kuondolea machungu naipenda sana jf.
 
Mkuu kuna muda unaenda out of control(unashindwa kubalance shobo)....
Hivi unadhani twitter,facebook,instagram ungekua na hiyo tiki ya bluu? Labda kwenye umbea,unafiki,majungu,promo hapo jf inaongoza..

Huu mtandao bado upo chini na haujafka hata theluthi ya hizo mithili ulizosema.....

Punguza haraka unapoandika....
 
Back
Top Bottom