Maisha ya jamii ya JamiiForums yako poa sana kuliko jamii ya Twitter, Facebook na Insta

Maisha ya jamii ya JamiiForums yako poa sana kuliko jamii ya Twitter, Facebook na Insta

NAKATAAA JF ni sawa na huko kwingine tu na ndio maana Twitter imeshika hatamu sana nowadays.

Mimi binafsi nafanya mambo ya hovyo sana huku JF na Twitter na wala sio uhalisia wangu hata kwa punje moja
Ndio umeambiwa kubadilika ni wewe na ukitaka kuendelea kuoza ni wewe
 
Screenshot_20221212-122821_Lite.jpg
 
JamiiForums ni jamii moja maridhawa mno, ambamo watu watakuonyesha tabia zao halisi zaidi ukilinganisha na jamii nyingine za mtandaoni.

Kwasababu wengi wanatumia majina kificho na picha kificho hapa JamiiForums imekuwa ni rahisi kuonywa kwa kupewa makavu laivu, tabia zako na mambo yako ya hovyo yote yanawekwa peupe, u unachanwa bila ganzi. Hiari ni yako ubadilike au uendelee kuoza.

Huko kwingine unafiki mwingi sana, uwongo uwongo na kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa.

Poa hapa jukwaani licha ya kwamba hatufajamiani, pia tunapendana na wapo wanaowachukia wenzao, Mi sina ninayemchukia, ulinizingua nakuroga tu, usiku mmoja unakuja kunilimia shambani kwangu kama mjombake UMUGHAKA na Emma walivyolimishwa na Mzee MAKONO.

Hapa na kuto onana/kufahamiana pamesaidia sana watu, hasa kwenye michongo ya kazi na deals mbalimbali.

Pia hapa pametoa connections na networks za maana sana.
Almost Tanzania nzima nina ndugu, nikiwepo tu Dar, nikitaka nyama na kichuri namtafuta rafiki yangu GENTAMYCINE, nikitaka mdudu simu ni moja tu Mshana Jr popote ulipo naomba muda wako, Bill Lugano my dearest brother atanipa kila ninachohitaji, na nikitaka kuzama kwenye books shelf namtafuta GuDume.

Yaani hapo ni wachache tu, bado sijaorodhesha warembo wenye akili zao za darasani, maisha na roho nzuri.

Moisemusajiografii na Kasie I miss you. Jiandaeni kunipokea hapo Tazara Station nakuja na treni ya Wakalamba ya Express Jumanne
We ndukghu yangku uliyehamia Mbheya una mathathizho sanha!
Lakhini ukho phowa sanha.
 
NAKATAAA JF ni sawa na huko kwingine tu na ndio maana Twitter imeshika hatamu sana nowadays.

Mimi binafsi nafanya mambo ya hovyo sana huku JF na Twitter na wala sio uhalisia wangu hata kwa punje moja
nifolo twita nitakufolo baki, hendo yangu ni hii hii
 
We ndukghu yangku uliyehamia Mbheya una mathathizho sanha!
Lakhini ukho phowa sanha.
Huwa nakukubali sana engineer msomi. Mchango wako ni mkubwa sana hapa jukwaani. Huwa napenda namna ambavyo umekuwa ukiishauri serikali. Laiti wakiufanyia kazi ushauri wako, mabadiliko makubwa tungeyaona kwa macho yetu ya nyama, tofauti na sasa tunahutubiwa maendeleo ambayo yako kwenye ulimwengu usiononekana. Utadhani mambo ya Gamboshi, uzuri wake na fahari yake inachagua nani aione
 
Naweza sema. Mods wanatukimbiza humu kwa double standards zao.

Mwanzo sijawahi itilia mkazo twitter ila siku hizi hasa huu mwaka nimeanza kuifurahia hio app

Mods wa JF rudini kwenye drawing board yenu
 
Back
Top Bottom