Maisha ya jamii ya JamiiForums yako poa sana kuliko jamii ya Twitter, Facebook na Insta

Maisha ya jamii ya JamiiForums yako poa sana kuliko jamii ya Twitter, Facebook na Insta

JamiiForums ni jamii moja maridhawa mno, ambamo watu watakuonyesha tabia zao halisi zaidi ukilinganisha na jamii nyingine za mtandaoni.

Kwasababu wengi wanatumia majina kificho na picha kificho hapa JamiiForums imekuwa ni rahisi kuonywa kwa kupewa makavu laivu, tabia zako na mambo yako ya hovyo yote yanawekwa peupe, u unachanwa bila ganzi. Hiari ni yako ubadilike au uendelee kuoza.

Huko kwingine unafiki mwingi sana, uwongo uwongo na kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa.

Poa hapa jukwaani licha ya kwamba hatufajamiani, pia tunapendana na wapo wanaowachukia wenzao, Mi sina ninayemchukia, ulinizingua nakuroga tu, usiku mmoja unakuja kunilimia shambani kwangu kama mjombake UMUGHAKA na Emma walivyolimishwa na Mzee MAKONO.

Hapa na kuto onana/kufahamiana pamesaidia sana watu, hasa kwenye michongo ya kazi na deals mbalimbali.

Pia hapa pametoa connections na networks za maana sana.
Almost Tanzania nzima nina ndugu, nikiwepo tu Dar, nikitaka nyama na kichuri namtafuta rafiki yangu GENTAMYCINE, nikitaka mdudu simu ni moja tu Mshana Jr popote ulipo naomba muda wako, Bill Lugano my dearest brother atanipa kila ninachohitaji, na nikitaka kuzama kwenye books shelf namtafuta GuDume.

Yaani hapo ni wachache tu, bado sijaorodhesha warembo wenye akili zao za darasani, maisha na roho nzuri.

Moisemusajiografii na Kasie I miss you. Jiandaeni kunipokea hapo Tazara Station nakuja na treni ya Wakalamba ya Express Jumanne
wapo wanaowachukia wenzao, Mi sina ninayemchukia, ulinizingua nakuroga tu[emoji23]
 
Unanikoshaga kwa style ya kuandika kwa ucheshi, mizaha and the like!
Huwa nafurahishwa sana na kile Kingereza chako konki cha Half London. Yaani ukiandika, lazima nitafute Oxford English Dictionary niiweke pembeni. Leo nikipewa nafasi ya kubadili kabila, ntachagua kuwa Muhaya.

Nilipata msichana akaniambia yeye ni mtu wa Bukoba, haraka haraka nikaenda kwao kujitambulisha, kumbe Mnyambo kahamia Bukoba.
 
Jamii forums ni nzuri sana. Tatizo vijana wengi wamejaa ushabiki maandazi, yaani uleushabiki wa bila logic.
Ushabiki wa mpira, ushabiki wa kiasiasa na ushabiki wa watu binafsi i.e, Diamond vs Alikiba, Messi vs Ronaldo
 
Jamii ya Twitter ni ya kutafutia ajira Serikalini.
 
NAKATAAA JF ni sawa na huko kwingine tu na ndio maana Twitter imeshika hatamu sana nowadays.

Mimi binafsi nafanya mambo ya hovyo sana huku JF na Twitter na wala sio uhalisia wangu hata kwa punje moja
Huo ndio uhalisia wako
 
Back
Top Bottom