Aris Saolanica
Senior Member
- Apr 27, 2017
- 124
- 84
Mwaka wa 30 nipo nyumbani. Nimejitahidi sana kutoka home nikaanzishe maisha mengine lakini mahesabu yamegonga mwamba. Naishi kwenye familia ya mzazi mmoja cha ajabu mother hasemi chochote yeye yupo bize na inshu zake. Warembo 3 wamenikimbia kisa kuendelea kwangu kukaa nyumbani. Kila napojaribu kuondoka vinatokea vikwazo lukuki hadi nimekata tamaa maana siku zote nabii hakubaliki kwao yaani kukaa kwangu home kumezuia fursa nyingi sana za kutofanikiwa kwani ujasiri wa kupambana umepungua pia kwa mazingira ya nyumbani huwezi kutengeneza network mpya kwani watu wanaokuzunguka ni wale wale. Kuna wakati naingiwa na hisia labda nimerogwa au vp. Maana kila nachofanya hakifanikiwi.
Umri wa miaka 30 sijaanza kujitegemea bado! sina mtoto sina demu na wala sijui nitaoa lini huwa naumia napoona washkaji young kuliko mimi wakiwa na familia zao wakati kwangu najiona nimeshafikia umri wa kuwa na majukumu hayo yani inaniuma sana. Mbali na hivyo bado sina kipato cha uhakika mishe zenyewe za kuungaunga leo umepata kesho umekosa so unakuta hata nashindwa kuchangia hata kwenye masuala ya kijamii hadi watu wanakuona mtu wa ajabu kutokana na life ninayoishi.
Naomba kuwasilisha wadau