Maisha ya Luhaga Mpina mashakani sana. Anakoelekea siyo kuzuri

Ila hoja zake ni za msingi

Tuachane na Mpina tuzungumze hoja zake ni za uongo au za kweli?
Ukizitazama kwa kina pia hazina msingi, mawaziri huwa hawana muda mrefu wa kujibu kwa kirefu kama anavyozitoa mle bungeni, huwa wanalazimika kutenga muda wa kujibu kila hoja inayoletwa na kila mbunge kuhusu wizara zao hivyo wanajikuta wakipungukiwa muda wa kujibu kwa kina.

Mengi aliyoyaongea kuhusu bandari katika suala la DP World hayana mashiko yoyote.
 
Viumbe kama nyie ndio humfanya mtu mweusi kuonekana kuwa ubongo wake bado upo kwenye evolution!! Hao kina Mandela, mwalim Nyerere, wangekuwa na akili kama hizi ingekuwaje!!!? Aibu naona mimi
 
Anaona wivu wenzie wanavyojipatia mijihela na ana hasira nao. Anateseka kwa mali ya umma kuibiwa angetulia tu kama wenzie wanavyokula.
Kila bunge anasimama na kujenga hoja zenye nia ya kuchafua mawaziri wa Samia, mlengwa haswa wa hoja huwa ni Samia mwenyewe.

Utadhani kifo cha JPM kuna mtu anayemjua ambaye alikisababisha, lipo kundi kubwa la watanzania wa aina hiyo wanataka sana kumlaumu SSH au JK kwa kifo cha mpendwa wetu lakini hawana ushahidi wa moja kwa moja wa asilimia 100.
 
Mpina kamatia hapo hapo bado hawajema #Mpakawaseme
 
Kwa hiyo ww unamwona MPINA ni shujaa na yupo hatarini kwa sababu anaongea? Kuna watu hatari zaidi yake na hao ndio wanampa mwongozo na hao ndio ambao hata MPINA mwenyewe anawahofia.
 
Watu wenye mtazamo kama huu wa kwako ni wa kunyongwa tu hadharani. Maana hamna faida yoyote ile kwenye jamii ya wapenda haki, usawa na pia mabadiliko ya kweli katika nchi.
Mpina ana faida gani, au ana faida kwako? Yule ni mnafki tu na jazba zote kwasababu ya kuukosa uwaziri. Mwambieni yule mshamba wenu arudishe mashamba ya wananchi Mvomero
 
Ndg kweli hakuna Ufisadi nchi hii?

Maana ndio hoja alizosimamia na sio yeye anasema ni Taarifa za Mashirika ya Kimataifa, Takukuru, CAG, PAC

Tukubaliane Mpina ni Muongo anasingizia mawaziri je Msukuma?, Bulaya?

Doh
 
Naunga mkono hoja 100%. Uhai ni bora kuliko vyote.
 
Wewe jamaa JUHA kwelikweli, inaonekana unaogopa sana kufa!!! Hata uogope, usiogope utakufa tu, sasa ni kipi bora kwako, ufe kwa kusema ukweli au ufe kwa unafiki??????????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…