Maisha ya machimbo ya dhahabu ni zaidi ya jeshi, nilikimbia

Kazi zingine Mimi siyokuja kudhubutu kuzifanya hata niwe nimepigika kiasi gani
 
Unakaa unatunga uongo wa kitoto na kutuletea watu wazima humu!!:huo uongo wa kipumbavu wadanganye watoto wenzio.
 
Anaitwa nani?
 
Huko kuko kama kama za wakimbizi wa sudan....kumejaa maturubali na vibanda wanaopata hupata kidogo sana
 
Mkuu....
Hiyo Busulwangili, Nyalwanzaja, Namba 9, Namba 2 unauonaje mziki wake kwa wachimbaji wadogo...??
Wanapata pesa kiduchu ...tajiri nae yuko mob na wenzake wakipata 100m wanagawana na kuishi kunywa bei n wanawake
 
Mwanzishaji thread na waliochangia. Kwenye migodi kuna mengi. Kuna watu wa kada mbalimbali. Wengi wanaozungumziwa humu ni wale wafanyakazi wa migodini, yaani waponjaji. Waponjaji ndio kazi yao. Hawaiogopi na wanaifurahia sana. Hao ninkama vibarua huku mitaani. Niambieni mbeba zege au mchanganya mchanga anayetoboa. Au mvuvi, sio mwenye mtumbwi.
Kule inategemea na mtaji ulio nao. Kuna watu wanaenda kule wao kazi yao ni kununua hizo poont point. Anakusanya zinakuwa gramu anaenda kuuza. Na wanafanikiwa.
Kuna wale wanaonunua makrasha wanawasagia wenzao, wanapata pia.
Kuna wanaosambaza viroba vya sulphate, maana vinatumika sana. Hao ni wafanya biashara.

Nawaomba mtofautishe vibarua na wafanbiashara hata kama wana mitaji midogo.
 
Kwenye shughuli ya machimbo unabeba zana ya jembe?

Basi hiyo ardhi ni soft sana

Nenda Chunya utaoneshwa sululu zilizopinda baada ya kukutana na hardcore rocks na vijana hawataki kukubali kuwa imeshindikana.
Get Rich or die trying....

Wachimbaji wadogo wana imani kali sana kuwa ipo siku tu atatoboa haijalishi kachimba na kutoka hola kwa miaka mingapi.
 
Kwa 25M alidhani atapata nini? 25M kwenye madini is nothing Bora angefuga kuku tu. Tatizo wengi wanadhani uchimbaji is a get rich quick scheme it's absolutely not.
Mtaji mzuri wa kuanzia ni upi chief ?
 
Mtaji mzuri wa kuanzia ni upi chief ?

Mkuu, inategemea unataka kufanya nini kwenye hii sekta. Unataka kuchimba, kuuza madawa na vifaa, kukodisha vifaa, kumiliki plants kama elution na leaching plants.

Uchimbaji unahitaji gharama, muda na utaalamu zaidi. Kadhalika uchimbaji ni risky ila return yake inaweza kuwa kubwa zaidi. Risks za uchimbaji zinaepukika kwa kuwekeza kwenye maarifa na utaalamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…