Maisha ya machimbo ya dhahabu ni zaidi ya jeshi, nilikimbia

Hahaha umenikumbusha hapa mtaa wa pili kuna mwana alilipwa hela na muhindi ili abomolewe nyumba yake itengenezwe godauni na barabara kwa ajili ya kupitisha magari ya muhindi.

Jamaa ilikuwa ni nyumba ya urithi halafu ana dada yake ambaye ana matatizo ya akili.

Kwahiyo mchizi ni kama ilikuwa nyumba yake tu kwasababu yeye ndio kila kitu.

Mhindi alimpa kama milion 100. Mchizi akazigawanya nusu kwa nusu.

50M akaenda kuiweka benki kwenye fixed account halafu 50M iliyobaki akajilipua Chunya kwenye dhahabu.

Jamaa amerudi anasubiria muda wa fixed uishe achukue hela yake aangalie Utaratibu mwingine.
 

Hela ina codes nyingi sanaaa 😅
 
Ee pale pa Mashahidi wa Yehova napapata , karasha lao lilikua kama kinu na magurudumu mawili hivi baadae wakasepa.
 
Ee pale pa Mashahidi wa Yehova napapata , karasha lao lilikua kama kinu na magurudumu mawili hivi baadae wakasepa.
Yap wewe mwenyeji na eneo hilo kabisa yani kulikuwa na kinu chenye mawe mawili meupe.

Lakini kama utakuwa unakumbuka pia maeneo fulani ya porini kule kwenye minara ya simu kama unaenda Mlima njiwa, kulikuwa kuna mzee mmoja anaitwa "Alialiu"

Huyu naye alikuwa ana karasha lake anasaga mawe.

Huyu mzee ana historia moja ya ajabu sana
 
Tupe historia
 
Basi ninyi wa ushuani huko mnaona ni ajabu, uko machimboni ni kawaida Mtoto wa kiume chini ya miaka kumi na Tano kuanza kujifunza kuchimba.
 
Basi ninyi wa ushuani huko mnaona ni ajabu, uko machimboni ni kawaida Mtoto wa kiume chini ya miaka kumi na Tano kuanza kujifunza kuchimba.
Mkuu hapa turudi kwenye hoja ya msingi achana na ushuani v/s uswazi.
Kwakifupi uchimbaji wa kienyeji unao usema wewe ulisha pitwa na wakati kwasababu ni kazi ya kubahatisha/haina uhakika. Zaidi watu wengi wanaufanya uchimbaji wa kienyeji kutokana kutokua na mtaji wa kutosha, kukosa elimu na umasikini.
Lakini bado nasisitiza kwamba kazi ya uchimbaji wa kienyeji ni high risk because of the nature and unsafe conditions
 
jah bless us
 
Mwakitolyo namba ngapi maana Zina namba....
Kuna jamaa wa botswana wameisha kua kama wa bongo....
Wanadeal wenyewe huita MARUDIO... Wanatumia CARBON
By then nilikua nafanya kazi na kampuni Moja huko lake zone tulikuaga tunatembea izo SITE,

DO OR DIE
 
Huyo mtasikia kajiua siku si nyingi( SIOMBEI)
 
Jana tumekutana mitaa fulani hapa Mbeya!
 
Tupe historia
Huyu mzee alikuwa ni mbishi sana, alikuwa anaishi porini ana krempu yake anachimba mawe na kusaga mwenyewe kwenye karasha lake.

Hilo eneo lilikuwa na mawe yenye dhahabu sana yani hadi nje ya jiwe dhahabu ilikuwa inaonekana.

Alikuwa ni mfugaji wa kuku, alikuwa ana kuku wengi sana kiasi kwamba hakuwa na banda la kuweza kutosha wale kuku.

Hivyo kuku wengine walikuwa wanalala maporini na sometimes walikuwa wanaliwa na wanyama.

Alikuwa anazunguka maporini kumwaga ulezi sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuku wake ambao wanaishi porini.

Sasa huyu mzee kuna siku walipita wajerumani na ndege yao kufanya survey, wakagundua kuwa eneo lile kuna dhahabu.

Wajerumani walikuwa wawazi, wakamuambia hapa chini kuna dhahabu kubwa sana ambayo kutokana na vifaa vyako huwezi kuifikia.

Kwa hiyo sisi tutakujengea nyumba kali mkoa wowote unaotaka, tutakusomeshea watoto kisha tutakupa M600

Mzee akakataa offa yao akidhani kuwa watakuwa wameona ameikaribia hiyo dhahabu hivyo wanataka kumdanganya ili awaachie mzigo wote.

Mzee aliendelea kuchimba lakini eneo lile lilikuwa na maji mengi sana na vifaa vyake vilikuwa sio vya kisasa alikuwa na jenereta la kuvutia maji lakini halikuweza kumudu.

Baada ya kuchimba kwa miaka mingi na kuona haifikii tu hiyo dhahabu, wakaja wachina na offa ya 400M ikabidi awaachie tu akatimkia Arusha.
 
Stori murua kabisa, safi sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…