Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 12,599
- 26,263
Yaani sijawahi pata ushuhuda WA mchimbaji mdogo mdogo katoboa...woote ni misoto
Technically hawa sio wachimbaji ni wabangaizaji hawapo hata level ya mchimbaji mdogo. Hawana leseni, mtaji wala basic tools. Mtu ana sululu, jembe na nyundo huyo nae anajiita mchimbaji kweli? Hawa wana tofauti gani na mtu anyejiuzia kiatu pair moja pale Kkoo afu asema biashara ngumu, utamchukulia serious?
Sisemi uchimbanji ni rahisi ila unahitaji uwekezaji, elimu na utaalam. Chunya inatoa 300-400Kg za gold kwa mwezi yani over 35 Billion TSH monthly, wanapataje kama uchimbaji haulipi kabisa?
Wengi wanaingia na matumaini hewa wanaishia kulia tu. Uchimbaji is not a get rich quick scheme kama wengi wanavyodhani hamna rangi utaacha ona ila unalipa.