Maisha ya madaktari wa Kitanzania na umaskini wao na kuishia katika kupata heart attack

Wapo wanaotoka familia zenye uwezo pia, kama sijakosea kuna mstaafu asiyestaafu ana mtoto ni Dr
 
Bila shaka wewe ni daktari. Umefanya kazi nzuri kuwasilisha mawazo ya kundi kubwa lililopo kwenye taaluma ya afya japo umegusia Madaktari pekee.

Kinachosumbua watumishi wengi nchini ni Uoga, Kutojiamini na Kutokuwa na misimamo.

Na hapo sekeseke la 'Dr Ulimboka' ndio lilifanya angalau maslahi yao kuwa mazuri.

Laiti kama wangefahamu nguvu waliyonayo, bila shaka 'watawala' wangeconsider maslahi yao.

Ni wakati sasa serikali kupitia upya 'Mishahara' ya watumishi wao ili angalau iweze kukidhi haja za maisha tuliyonayo sasa.

Wanaweza kuboresha maslahi hata kwa kuanza na makundi, mfano 2026/2027 ni walimu then 2027/2028 Afya and so forth.

Itasaidia kurudisha molari yao ya kazi katika kuwatumikia waTanzania.
 
Kabisa mkuu,yaani hii nchi kuna utamaduni wa wafanyakazi kuwa waoga, ajira inachukuliwa kama hisani, kiasi kwamba mtu anakaa kimya hata akionewa. Imagine huko Tamisemi diwani anaenda kumhoji daktari,diwani aliyeishia la 3C!!!!!!!!. Tunahitaji kushughulikia huu utamaduni wa uoga unaofanya wafanyakazi wanashindwa kutetea maslahi yao. Nchi nyingine hata wanasiasa hawachezi na kada za afya, maana wanaujua moto wao . Hapa Bongo, mjamzito akifariki kwa sababu hospital haina vifaa au dawa, manesi wa zamu wanakuja kudhalilishwa na mkuu wa wilaya kwenye vyombo vya habari, tena mkuu wa wilaya ambae hawezi hata kutaja jina la mshipa mmoja wa damu kwenye mwili.
 
Una hoja njema mkuu ila hasahasa kulingana na majukumu ya daktari.

Kuna kipindi nilizani udaktari sio kazi ambayo mtu anasomea kwa lengo la kupata kipato %100, namanisha udaktari kwangu ni kama uchunganji ule wa zamani yaani mtu anajitolea na kuridhika na kidogo atachopata.

Kama serikali haitaki kuwaongeza mshahara madaktari basi ndg watanzania tuwe na utaratibu wa kuwapa asante madaktari wetu pale wanapotuweka sawa kiafya. Binafsi hua siwezi kuondoka zahanati bila kuacha chochote kwa mhudumu wa afya alienihudumia, mf juzikati hapa mke wangu kajifungua salama manesi niliwapa 50,000 ya asante na kweli walishukuru sana ila mimi ndie niliewashukuru zaidi.

Dokta sio kama fundi pikipiki tuwajali.
 
Sekta nyingi serikalini mishahara haiendani na hali ya maisha sio madaktari peke yao, hii inafanya rushwa iwe solution ya ku-survive. Shida inakuja kwenye kada kama ualimu ambao hawana option ya kuvuta chochote kitu.. Hii sio sawa kabisa
 
Umesema vyema. Nadhani kwasasa jukwaa zuri ambalo lingetufaa kupambania maslahi yetu ni MAT. Changamoto ya MAT sasa hivi imekuwa yakisiasa sana.
Nyie machawa ndiyo mmeharibu siyo hiyo MAT tu bali karibu kila sekta kwa tamaa zenu za kuonekana na kupewa nafasi za 'kisiasa' na hao wahuni wanaojiita watawala.
 
Hivi hawa madaktari tunaopishana nao huku Agha Khan siyo waajiriwa wa serikali kweli? Daktari anayelia njaa ni yule hajielewi!
 
Hivi hawa madaktari tunaopishana nao huku Agha Khan siyo waajiriwa wa serikali kweli? Daktari anayelia njaa ni yule hajielewi!
Hao sio waajiriwa wa serikali, Aga Khan wanalipwa vizuri sana kiasi kwamba hakuna haja ya kwenda kupambana huko hospital za serikali na madiwani na wakuu wa wilaya.
 

Wanasiasa husema "hawa madaktari tumewasomesha kwa kodi zetu", utafikiri daktari kasomeshwa bure kweli lakini ana mzigo wa kulipa mkopo wa HESLB ndiyo maana huishia kupata laki 8 mwisho wa mwezi.

Daktari aliyesoma kwa mkopo wa HESLB hudaiwa si chini ya million 25 ambayo hulipia kwa zaidi ya miaka 8 kwa hiyo ili afanye mambo ya maisha yake ni lazima achukue mikopo.

Kama hawataki kuboresha mishahara basi waondoe hayo makato ya HESLB (ambayo kwa mwezi si chini ya Tsh. 200,000/-) ili wanaposema wamesomeshwa bure uwe ni ukweli.
 
Wizara ya TAMISEMI inaingilia wizara mama nadhani hii ipo Tz tu(uvuvi,barabara,afya,elimu).Hii nchi sijui walilenga nini na ukiangalia huko TAMISEMI ndio kumejaa uozo🤔.
Uozo mtupu kama nini uliza madaktari wa tamisemi saiv wengi wanajihusisha na biashara tu walishajikatia tamaa hata ya kile walichokisomea, wengi wanatoka huko kwa kwenda kujisomesha na kwenda kujisomesha kuna wale washenzi waliopo maofisini kutoa ruhusa tu hadi uonge au kujipendekeza ushenzi mtupu tu
 
Bora unaushuhuda kabisa wa haya mambo, madaktari wanatia huruma kabisa, unaweza ukamkuta daktari hata ukimpa 5000 hospital anapokea
 
Umesema vyema. Nadhani kwasasa jukwaa zuri ambalo lingetufaa kupambania maslahi yetu ni MAT. Changamoto ya MAT sasa hivi imekuwa yakisiasa sana.
MAT siasa nyingi hamna wa kutetea madaktari kule, wanajali maslahi yao na kukaa kaa karibu na wanasiasa na kusahau kutetea maslahi ya wenzao kitaaluma, hadi leo Level ya daktari bingwa bobezi haitambuliki serikalini kimishahara, lakini watu hao wanahitajika. MAT ya Dr. Ulimboka ndio ilifanya jambo ambalo hadi wewe saiv unanufaika nalo, kina kigwangala wale ndio walipigania maslahi ya wanataaluma wenzao, MAT imeoza na haitokuja kuamka kushughulikia maslahi yenu
 
Haha ha nimbe kawimbo kwanza hapa
Mimi ni nani jamaa Mimi ni mwalimu,
Kada hizi bongo ni ujinga TU , elimu, afya , ulinzi , yaani ukijikuta upo tamisemi kwisha habari yako, hebu fikiria Mimi ni mwalimu kwa miaka zaidi ya kumi sasa, take home yangu ni laki nne kama nusu ni baada ya kukopa, sasa unatoboaje , na hata nisingekopa kabisa ningekuwa nalipwa million Moja na laki mbili, pesa ambayo tunahonga wanawake zetu waliotuzalia watoto ili waendelee kuwatunza watoto,
Solution Kwa SAsa ni ipi nifuate, Mimi nilipogundua na kufahamu salary yangu , nilipochunguza watumishi walionitangulia nilifanya a very very excutive decision and sure it paid me , niliamua kutafta biashara na kuangalia wapi niwekeze, nimecheza na nafaka sana, nimecheza na kilimo sana , ukijumlisha na Mali za urithi sijadili tena mishahara,ila nimekuwa mwalimu asiyekalika kituoni, wananita flying lecture sijali namtuliza headmaster na vichenji chenji ila wakinifuatiia sana nawachia kazi Yao ya ualimu
 
Sasa kila mtu akitoroka kwenye kituo chake cha kazi kwenda kutafuta maisha mitaani, nani atatoa huduma kwa wananchi? Mm nadhani tuyatumie vizuri majukwaa ya vyama vya wafanyakazi kudai maslahi bora wakati huohuo tukiendelea kuwahudumia wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…