Maisha ya madaktari wa Kitanzania na umaskini wao na kuishia katika kupata heart attack

Fahamu hili!
Kazi za Afya,Ualimu ni kazi za Wito! Hazitofautiani na kazi za Kanisa!
Siyo kazi za kutengeneza pesa! Usipojua hili unaweza kuishia kwenye "heart attack"!
Zaidi ya hapo,rushwa (CCD) haziwezi kuisha! Kazi ni kwa Wagonjwa.
 
Hata BIMA ZAO ZA AFYA NHIF BI STANDARD zipo chini sana,hazi wezi kulipia baadhi ya gharama za matubabu,yani bima za afya za madaktari zinazidiwa uwezo wa kulipia wingi wa huduma za matibabu na bima za afya za watumishi wa TANESCO,TRA,MABENKI NA WABUNGE NK...

ili hali wao ndio wanatibu hao wengine ila wao madokata bima zao haziwezi kulipia gharama baadhi,maisha ya madaktari ni ya kuwaonea huruma ,na mazingira magumu ya kazi...hawana hata risk allowance?
 
CCM wanasoma comment yako wanacheka sana.
 
CCM wanasoma comment yako wanacheka sana.
siwezi kumshauri kijana asomee udokta kwa ajili ya kuja kufanya kazi bongo.
unless uwe mwizi mpiga madili,sasa hapo utapata DHAMBI KWA MUNGU ,KUMUOMBA MGONJWA RUSHWA..HIYO ni dhambi....vinginevyo kama una hofu ya MUNGU wewe dokta ndio itabidi uwachangie wagonjwa MASIKINI pesa,nguo,chakula,pampasi,hata kulipia dawa na matibabu .na MUNGU ATAzikumbuka sadaka zako unszitoa kwa wagonjwa wako unaowahudumia)...vinginevyo ukitaka kupata hela kwenye udaktari utajikuta unachuma dhambi na laana,na unakuwa muuaji kama wale wanafanya criminal abosheni..
 
Daktari kulipwa laki nane Take home ni upuuzi na Matusi makubwa.
Kidogo wangekuwa wanaanza hata na 2M .
Inasikitisha watu ambao tumesoma vitu vya ajabu unapata x2 ya salary ya daktari.
Watu Gani TAMISEMI wanalipwa 2X ya Daktari?
 
Is all about business,anayekulipa mshahara ni muajiri wako na sio elimu yakoπŸ˜†πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Sijui maswala ya tamisemi ndugu
Upo sawa,na inawezekana mambo mengi hujui pia
Hata huko kwenye taasisi,JKCI,MOI,MNH,BOT,UDOM,OSHA etc MD wapo na wanalipwa kulingana na viwango vya taasisi husika na wana bima za afya na stahiki zingine sawa ama Kuzidi na wafanyakazi wengine
 
Pesa ya hii mifumo ya bima kama NHIF , ziwe zinachotwa ili kuongeza mishahara ya madaktari. Najua mtatukana ila ukweli hii nchi yetu serikali inakusanya mapato kidogo sana , mengine tunategemea kuomba omba bado tunatakiwa kupata huduma bure . Mtihani itafutwe jinsi hata watu wakatwe buku buku kwa kwenye baadhi ya miamala ili pesa zikaongeze mishahara ya madakatari , wafanyiwe msahama au kupunguziwa PAYE .

Muda mwingine , wakitoza hata elfu 10 basi unaambiwa rushwa , ukienda kumpongeza daktari kwa zawadi eti ni rushwa​
 
Nimesoma comment section nimestaajabu , madaktari pamoja na heshima yote kumbe mapato yangu NI mara tatu Yao , masikini kumbe madokta NI Wakuonea huruma,Serikali muwape walau Aya Ka 2M aisee,tunachokifikiriaga huku mtaani Ni kwamba madaktari Wana maisha mazuri kumbe tumajidanganyaga 900K take home what a shame ????
 
Daktari kulipwa laki nane Take home ni upuuzi na Matusi makubwa.
Kidogo wangekuwa wanaanza hata na 2M .
Inasikitisha watu ambao tumesoma vitu vya ajabu unapata x2 ya salary ya daktari.
Nchi inasikitisha sana hii dah.
 
nchi ya mazombi wakati huko tra tasac na tcra etc wahudumu tu na madereva wanakula kuanzia 3m , ukiwaambia wawaongezee mishahara madaktari unaambiwa hamna hela, huko na kule mkuu tu wa kiwilaya masikini anatembelea gari ya milioni mpaka 600. Aliyewaroga wabongo ashakufa.
 
Kua madokta wote kwenye hii nchi mapato yao, kwako ni mara 3 yake??
Kua haiwezekani mtu yeyote kwenye hii dunia kua na mapato mara 3-3000 ya madaktari?
Either wewe ni MPUMBAVU ama una wivu na madaktari,ulikosa kua MD,umegeukia chuki dhidi yao
 
Hapo shida sio hao wanasiasa,shida ni hao madaktari waliokubali kutumika kama mbuzi
 
Fahamu hili!
Kazi za Afya,Ualimu ni kazi za Wito! Hazitofautiani na kazi za Kanisa!
Siyo kazi za kutengeneza pesa! Usipojua hili unaweza kuishia kwenye "heart attack"!
Zaidi ya hapo,rushwa (CCD) haziwezi kuisha! Kazi ni kwa Wagonjwa.
Wito ilihali mahitaji yao hayatimizwi wito wa wapi huo? . Mapadri na masista wa Katoliki wale wanaambiwa kazi zao ni za wito ndio maana Kanisa linahakikisha wanapata mahitaji yote kwa wakati kuanzia chakula, mavazi, malazi,elimu, matibabu hata ikihitajika kwenda Ulaya kutibiwa Kanisa linagharamika. Sasa huyo daktari mahitaji yake hatimiziwi huo ni wito au unyonyaji? watoto wa daktari walipiwe ada na nani? kodi ya nyumba ya daktari alipiwe na nani? . Halafu hayo mambo ya wito ni Bongo tu? madaktari wa Uswisi wanaolipwa pesa ndefu kuliko mawaziri wao kazi yao sio ya wito ??
 
Serikali inakusanya mapato kidogo lakini Ina pesa za kununua magari ya mabilioni? Serikali inakusanya mapato kidogo lakini ina pesa za kuwapa wabunge mishahara ya kufuru? Serikali inakusanya mapato kidogo lakini trilioni za safari za viongozi zipo? Ila hela za kulipa vizuri madaktari ndo hamna.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…