Maisha ya ndoa na familia

Maisha ya ndoa na familia

clearmind

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2013
Posts
813
Reaction score
1,913
Sehemu YA kwanza
*(Uandishi wangu si mzuri sana)

Jina langu ni Vintage1q. Nimezaliwa mwishoni mwa miaka YA themanini na kukulia ughaibuni kwa takribani miaka 12. Nimezaliwa katika familia YA hali YA chini kabisa na mimi nikiwa ndo mtoto wa kwanza wa kiume.

Kukulia na kuishi ughaibuni kwa miaka yote 12 ilikuwa kama zali tu(nitaelezea siku nyingine). Baada ya kurudi nyumbani, mwishoni mwa miaka ya tisini, nikaangalia uhalisia wa mazingira niliyozaliwa, hakika niliumia sana. Mama yangu mzazi siku moja alinishika mkono na kuniambia kwamba jambo pekee litakalotukomboa katika hali ya umaskini, ni wewe kusoma kwa bidii. Niliamua kwenda shule na kusoma kwa bidii. Mimi ni miongoni mwa wanafunzi pengine wachache ambao nimesoma kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne nikishika namba moja pekee.

Baada ya kusoma na kumaliza kidato cha sita, wakati fulani nikiwa katika makambi ya wasabato, siku ya jumamosi, nilipokea ujumbe kwenye karatasi ndogo iliyokunjwa ukiniomba nikutane na dada mmmoja ambae alitaja jina Lake kama(hapa nintatumia Upendo). Baada ya ibada alinifuata na kunisalimia. Alikuwa bado mgeni machoni pangu. Baada ya maongezi, alinifahamisha kwamba wakati mimi nipo kidato cha nne yeye alikuwa kidato cha pili katika shule ile ile. Upendo alikuwa mrembo sana. Aliniambia dhahiri kwamba alikuwa anani-admire sana ila alikuwa anashindwa kuwa na ukaribu na mimi kwa sababu muda wote nilikuwa busy na masomo.

Baada ya mazungumzo marefu, Upendo aliniambia kwamba hata hivyo Ana bahati mbaya kwa sababu hajafanya vizuri kwenye masomo yake na hakuona nafasi ya kuwa na mimi tena kwani wanaume wengi waliosoma, wanapenda wanawake wenye hadhi yao(alipata division IV-28). Kwa utani, nilimuahidi kwamba ningemuoa na akaniomba twende nyumbani kwao kuwasalimia wazazi wake(si mbali na pale mahubiri yalikuwa yakifanyika). Tulikwenda na akanitambulisha kwa wazazi wake kwamba mimi ni rafiki yake. Wiki chache baadae matokeo ya kidato cha sita yalitoka na nilikuwa nimefaulu vizuri. Niliomba chuo na nikawa nimepata nafasi katika mojawapo ya vyuo vikubwa hapa nchini.

Nilijiandaa na hatimae kwenda kuanza masomo ya chuo kikuu. Upendo nae alipata nafasi ya kwenda kusoma chuo cha ualimu wa msingi. Baada ya kufika chuoni, niliugua sana. Nilikuwa nikivimba miguu na mikono. Nilishindwa kutembea kabisa. Kadili siku zilivyosonga, nikienda hospital na kwa wachungaji kuombewa bila nafuu, hali ilikuwa inazidi kuwa mbaya sana. Hatimae nilipata wazo la kuahirisha masomo. Niliwasiliana na Upendo na kumueleza adhima yangu hiyo. Alinisihi sana nisiache masomo na yeye alikuwa tayari kuacha masomo na kuja kuishi na mimi hadi nitakapo pata ahueni. Niliona ni jambo gumu lakini kesho yake alisafiri na kuja mpaka chuoni akapokelewa na rafiki yangu akamleta ghetoni tulipopanga.

Upendo alinisaidia sana. Ndio alikuwa mtu pekee wa kunisapoti upande ambao ulikuwa na madhara zaidi na kunikokota hadi chuoni. Baadhi ya walimu wangu walimpenda sana. Wakawa wanamsihi kukaa hadi muda wa vipindi unapokwisha. Akinisaidia kutoka lecture room moja kwenda nyingine. Wazazi wake walikasirika sana. Wakamuambia kwamba si mtoto wao tena. Alikuwa akilia sana. Lakini muda wote alikuwa akiniambia kwamba faraja yake ni mimi. Alinionesha mapenzi ya dhati sana.
 
Katika mwaka wa pili wa masomo yangu, hali yangu ilikuwa mbaya sana. Nilihisi mwisho wangu wa kuishi ulikuwa umefika. Nilihisi maumivu makali sana. Nilikata tamaa. Upendo alikuwa akiketi pembeni mwa kitanda akilia na kuomba.

Jioni ile, nililia sana. Nikamuomba mwenyezi Mungu anisaidie kwa namna yoyote nifike nyumbani nikafie kwa wazazi wangu. Ghafla, nikapatwa na usingizi mzito. Nikalala fofofo. Nilizinduka kesho yake marafiki zangu pamoja na Upendo wakiwa ndani ya chumba change na sikuwa na maumivu tena. Yes, nilikuwa nimepona hadi leo ninapoandika ujumbe huu, sijawahi rudiwa tena na ile hali. Upendo alifurahi sana. Alikuwa ameshafutwa masomo tayari chuoni baada ya kutohudhuria kwa muda mrefu. Nilidhamiria kumpenda kwa moyo wangu wote. Nilipata nguvu na tukaanza kufurahia faragha ya ndoa. Upendo wangu alishika ujauzito.

Lilikuwa ni jambo la furaha sana kwetu. Baada ya kukaribia muda wa kujifungua, nakumbuka nilikuwa nikiwa najiandaa kutoka. Upendo alinifunga tai lakini baada ya muda mfupi akawa analalamika sana kichwa kuuma. Nilimuomba ajiandae twende hospital then nitaendelea na ratiba yangu baadae. Wakati ninatoka nje, nikasikia mshindo mkubwa ndani. Nikarudi kuangalia kuna nini. Alikuwa ni Upendo ameanguka Chini huku akikoroma na damu nyingi zikimtoka ukeni na mdomoni.

Alizima kabisa mithili ya mtu alie kata roho. Nilichanganyikiwa. Nilitoka nje nikipiga kelele kupata msaada wa majirani. Mama mmoja alikuja akaingia ndani na kuweka mkono wake kifuani mwa Upendo kisha akanisihi nisilie kwa sababu bado alikuwa hai. Wakati huo mwenye nyumba alifika pia na gari Lake. Tukambeba na kumuweka kwenye gari huku mimi nikikaa nae nikiwa nimembeba.

Alikuwa akitokwa na damp nyingi sana. Muda wote huo nilikuwa nikitokwa na machozi sana. Nilijua nampoteza Upendo wangu. Baada ya kufika hospital madaktari walimpokea na kumkimbiza kwenye chumba cha dharura. Baada ya muda mfupi niliitwa ili nijaze fomu apate kufanyiwa upasuaji. Nilikaa nje, ghafla nikaitwa na daktari mmoja mwanamama akaniambia nisipaniki na Upendo Angepona. Niliingia chumba cha upasuaji na Upendo alikuwa amepata fahamu. Alikuwa akilia huku akiwaambia madaktari kwamba namuhitaji Vintage1q wangu.

Alifanyiwa upasuaji na tukampata mtoto wa kike. Niliwapigia wazazi wake simu lakini hawakutaka kusikia chochote kuhusu Upendo. Baada ya kumueleza baba yake kilichotokea, alinijibu kwamba huo ni mzigo wako. Wewe fanya utakachoona kinafaa.

Nitarudi baadae kuendelea
 
Sehemu ya Tatu

Baada ya kupata majibu ya kukatisha tamaa kutoka kwa wazazi wa Upendo, niliamua kutoendelea kuwapa taarifa kuhusu maendeleo ya Upendo. Nilibaki kuwa faraja kubwa kwake pamoja na mtoto wetu. Tuliishi kwa furaha na upendo mkubwa sana. Wakati mwingine tulikuwa tukitoa machozi tukikumbuka nyakati ngumu zilizopita.

Katika mwaka wangu wa mwisho wa masomo, nilimuomba Upendo afunge safari kuelekea nyumbani kwetu ili nipate nafasi ya kupambana na kumaliza mwaka wa mwisho salama maana ulikuwa na programs nyingi sana. Mpenzi wangu Upendo alikubali na wazazi wangu walikuwa na shauku kubwa ya kumuona. Wakati akiwa safarini, niliwasiliana na rafiki yangu ambae alikuwa akiishi Dodoma akifanya kazi. Rafiki yangu huyu tulisoma pamoja na kiukweli alikuwa kama ndugu. Mpenda dini sana. Katika kipindi chote ambacho nilimfahamu hakuwahi kuwa kwenye mahusiano na binti yoyote. Nilimueleza kuhusu mpenzi wangu kurudi nyumbani.

Rafiki yangu aliniomba Upendo wangu apite nyumbani kwake amsalimie kabla ya kuelekea nyumbani kwa wazazi wangu, Mwanza. Ilinilazimu nimtaarifu mama yangu kwamba Upendo angechelewa maana anapita Dodoma kwa rafiki yangu Charles kumsalimia. Mama alishtuka kisha akaniuliza kama Charles Ana nyumba nyingine ya Upendo kufikia. Nilimuuliza Charles akanijibu kwamba nisiwe na shaka nyumba ipo na mimi sikuwa na wasiwasi juu ya Charles. Baada ya majadiliano hayo, nilimpigia simu Upendo akiwa safarini na kumuelekeza ateremke Dodoma kumsalimia shemeji yake.

Alifika salama na kupokelewa na Charles. Baada ya siku tatu, nilimpgia simu Upendo nikimuelekeza aelekee mwanza. Baadae kidogo rafiki yangu Charles akanipigia simu akinisihi Upendo asielekee Mwanza kwamba angekwenda kuwasumbua wazazi tu na hali ngumu iliyopo nyumbani. Tuliongea mengi na kisha nikamuuliza Upendo kama alikuwa huru kuendelea kukaa pale. Alinijibu kwamba hapakuwa na shida.

Ajabu ni kwamba, siku ile usiku nilikuwa naota Upendo akiwa anafanya mapenzi na rafiki yangu. Nilifadhaika mno. Asubuhi nikampigia simu kumuuliza kama alikuwa salama, akanijibu kwamba hapakuwepo na shida. Ndoto ile iliendelea kwa siku tatu mfululizo. Niliumia sana. Nikawa mtu mwenye mawazo sana chuoni. Nilijipa moyo na kuendelea na masomo. Baada ya kumaliza chuo, nilikuwa na barua mkononi nikihitajika kwenda kufanya kazi singida katika kampuni fulani. Niliomba udhuru wa siku kadhaa kwenda kumufuata mke wangu. Nilisafiri hadi Dodoma na kufika kwa rafiki yangu. Upendo alifurahi sana kuniona laikini alikuwa mwenye mashaka. Rafiki yangu pia hakuwa na ule uchangamfu nilio uzoea. Baada ya mazungumzo mafupi, nilikaa na Upendo kwa mazungumzo. Nikamueleza kuhusu ile ndoto. Nikamkumbusha mambo mengi tuliopitia katika maisha. Kisha nikamuomba anieleze ukweli na akanithibitishia kwamba, rafiki yangu alikuwa akimuingilia kwa nguvu usiku wa manane na kweli mlango ule haukuwa unafungwa.

Sikumhoji Upendo mambo mengi. Nikajua mimi ndie mwenye makosa. Nikamuomba tuondoke pamoja na mtoto wetu. Rafiki yangu Charles, aliomba kuondoka nasi pia ili akaone tunapoishi. Tulisafiri na kufika Singida. Nikaoneshwa nyumba ya kuishi. Ilikuwa na kila kitu. Muda wote huo nilikuwa na mawazo sana. Sikuwa sawa. Niliwaza ni kwanini Upendo afanye vile. Niliingia chumbani kwenye ile nyumba. Nikatoka nikaingia jikoni. Nikaona kisu kikiwa kwenye beseni. Kipya kabisa. Akili ilinitima kwamba nilipaswa kumumaliza Charles. Nilikibeba kisu nikaelekea sebuleni alipokuwa amekaa Upendo na Charles. Nilitetemeka nikaangusha kile kisu.

Wakati huo, nilikuwa sijamueleza Charles chochote kuhusu alichokifanya kwa Upendo. Baada ya tukio lile, Upendo alilia sana. Akainama akanishika miguu na kuniomba msamaha. Niliongea na Charles kwa uchungu sana na kuamua kusitisha urafiki wetu tangu siku ile. Charles aliondoka kurudi Dodoma.

Itaendelea,,,
 
Sehemu ya nne

Niliendelea kuishi na Upendo huku nikijaribu kusahau yote yaliyopita. Baada ya wiki mbili, usiku mmoja nikiwa nimelala, majira ya saa saba usiku, nilishtuka na kugundua Upendo hakuwepo kitandani. Nilijongea taratibu kuelekea sebuleni na kumkuta akiweka nguo zake kwenye begi. Nikamuuliza kwanini alikuwa akifanya vile usiku ule na kama ana safari kwanini hakunijulisha mapema. Upendo aliniomba tukae tuongee. Alijifuta machozi yaliyokuwa yakimtiririka machoni pake. Akapiga magoti mbele yangu na kuniambia kwamba anajutia kwa yote aliyoyafanya na rafiki yangu kule Dodoma na hakuwa anajisikia amani.

Aliniomba aondoke. Nilimsihi sana asiondoke lakini alisisitiza kuondoka. Hatimae nilikubali aondoke. Asubuhi ilipofika, nilimpa nauli na akaondoka kwenda kwa wazazi wake. Mara hii, walimpokea. Baada ya mtoto wetu kufikisha miaka mitatu, Upendo alimleta kwangu. Aliniambia mtoto wetu yule ni zawadi na ishara ya upendo wetu. Kwa kipindi chote hiki, binti yangu anaishi na wazazi wangu. Mpaka naandika ujumbe huu, yupo darasa la sita sasa.

Ilipita miaka miwili bila kuwasiliana na Upendo na mimi nikawa nimehamia Dar es salaam. Siku moja nilipokea simu kutoka namba mpya. Alikuwa ni Upendo akiniomba tuonane. Alipata mawasiliano yangu nyumbani kwetu na kufahamishwa kwamba nipo Da res salaam. Nilikubali kukutana nae. Nikamuelekeza mahali akafika. Tukiwa tunaendelea kupata maji, Upendo alinieleza kwamba alikuwa kwenye hatua za mwisho kufunga ndoa na alihitaji baraka zangu. Nilimtakia kila la kheri na kumsihi kuishi vema na mme wake. Tuliagana na Upendo hatimae aliolewa na mwanaume mwingine.
 
Sehemu ya Tano
Baada ya kuishi muda mrefu nikiwa single, niliamua nitafute binti kwa ajili ya ndoa. Nilipambana na hatimae siku moja nikiwa maeneo ya posta, nikikutana na binti mmoja(tumuite Yasinta). Nilimuomba Yasinta mazungumzo. Nilivalia smart sana. Muonekano wangu ulikuwa ang'avu sana. Isingekuwa rahisi kukataa. Yasinta alikubali tukasalimiana vizuri na baada ya maongezi mafupi aliniomba tupate muda wa mazungumzo zaidi siku nyingine kwani muda ulikuwa umekwenda sana.

Tulipeana namba za simu na kuagana. Tuliendelea kuchat na kupigiana simu mara kwa mara kwa wiki kama mbili hivi. Tulioeana ahadi ya kukutana kigamboni pale kijiji beach. Tulikutana na Yasinta alinieleza kwamba alikuja nyumbani kwao Kimara kwa likizo ya mwezi mmoja. Yasinta alikuwa mfanyakazi wa taasisi binafsi huko Manyara. Nilimueleza azima yangu kuhusu ndoa na hakuonesha mashaka juu ya hilo. Alinipa sharti moja la kubadili dhehebu ili niwe mlokole maana yeye ni mlokole na Baba yake ni mchungaji. Halikuwa jambo gumu kwangu kufanya maamzi.

Nilimhakikishia kwamba ningehama kutoka usabato na kuingia kwenye ulokole ili lengo letu litimie. Tuliamua kwa pamoja kuanza safari ya uchumba. Nilihama Dar es salaam na kuelekea Manyara. Nikatafuta kazi huko na haikuchukua muda nikapata kazi. Lengo lilikuwa kuwa karibu zaidi na Yasinta na hatmae kufunga ndoa. Nilitafuta kanisa la pentecoste na kuanza mafundisho.

Niliwajulisha wazazi wangu na hatimae tukapata nafasi ya kujitambulisha kwao Yasinta. Nilishuhudia mnyukano mkali sana kati ya Baba yangu na wajomba zake Yasinta kuhusu mahari. Baada ya mvutano mrefu, niliambiwa kutoa mahari ya shilingi milioni mbili na nusu. Mwanzoni mwa mwaka 2020, nilibatizwa na November 2020 nilifunga ndoa na Yasinta.

Maisha yalikuwa mazuri mwanzoni japo baadae nilikuja kugundua kwamba Yasinta alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mojawapo ya viongozi kanisani. Mara kadhaa nilimfuma na sms za huyo kiongozi akiomba waonane wakumbushie penzi Lao. Nilikuwa mara nyingi nakaa nae na kumuelewesha kuachana na hiyo tabia. Yasinta, kumbe, alikuwa akichukia sana.

Katika nyakati zote tangu nimalize chuo kikuu, nilikuwa ba wazo la kuacha ajira ili nijiajiri. Nilikuwa nikioambana sana. Nilimulewesha mke wangu kuhusu hilo na tukakubaliana kwamba mwaka unaofuta inabidi tuache kazi na kurejea Dar es salaam. Nilikuwa nimejipanga hasa. Nilikuwa nimeweka fedha ya kutosha kuanza maisha mapya. Mwaka 2021 November, tuliacha kazi na kujipanga kurudi Dar es salaam.
 
Sehemu ya Sita

2021 tulimpata mtoto wa kike na Yasinta. Kwahiyo, nilimtaarifu Baba yake Yasinta kwamba mke wangu angerejea hapo nyumbani kwake na baada ya wiki moja ningeungana nae Dar es salaam. Baba mkwe alikubali. Nilibaki Manyara kwa muda ili nikusanye fedha yangu kiasi ambayo nilikuwa nimewakopesha baadhi ya watu pale kazini. Nilifungasha kila kitu pamoja na sanduku moja ya chuma ambayo alikuwa na pesa za kutosha. Wakati naweka akiba, sikuwa naweka benki. Ni utaratibu ambao nimekuwa nao kwa muda mrefu.

Baada ya Yasinta kufika Dar, alinieleza kwamba alikuwa na dhamira ya kurudiana na mpenzi wake wa zamani na hivyo alihitaji talaka. Nilidhani ni utani lakini kumbe alimaanisha. Baada ya hapo hakupatikana tena kwenye simu. Niilichanganyikiwa sana. Sikuwa tena na nguvu ya kuendelea kudai madeni. Nilijikuta nakuwa na mawazo mengi sana. Nilishindwa nini cha kufanya kwa wakati huo.

Niliwapigia wazazi wake Yasinta na hawakupokea simu. Nilifanya jitihada nikafika Dar es salaam. Nikaenda kwao Yasinta na wazazi wake wakaniambia kwamba Yasinta alifika akawaeleza kwamba tumeachana. Kwahiyo na wao walikuwa wakinisubiri nifike biwape maelezo kwamba kwanini niliwaambia kwamba binti yao anakuja kukaa kwa muda na yeye akafika na taarifa za kuachika.

Nilivurugika sana. Sikuwa na fedha yoyote ya ziada. Sikuwa na sehemu ya kuishi. Sikuwa na nguo za ziada. Mpaka kufika Dar es salaam kutoka Manyara, niliuza simu yangu kwa bei ya hasara ili nipate nauli. Niliondoka kwa Baba mkwe bila msaada wowote kuhusu mke wangu na mtoto. Mke wangu aliondoka na kila kitu.

Nilianza kuhangaika jijini Dar es salaam. Nilitanga tanga nikafika maeneo ya Burundi sheli nikawa hapo usiku kucha. Nilishudia mambo ambayo sijawahi ona maisha yangu yote. Ndio ilikuwa mara kwanza kuona wanawake wanajiuza. Ilikuwa mara kwanza kuona vijana kwa wazee wakijidunga madawa na kuzima kabisa. Niliogopa sana.

Sikuweza hata kutafuta kazi maana nyaraka zangu zote aliondoka nazo Yasinta. Nilijaribu mara kadhaa kuomba kwenye steshenari msaada wa komputa ili niingie kwenye email yangu maana nilikuwa na copies za vyeti kule lakini kila nilipouwa najaribu kufungua, kuna authentication code ilikuwa inatumwa kwenye namba yangu ya simu. Laini ambayo nilikuwa nimeshaipoteza tayari.

Niliumia mno na nikazidi kuwa na msongo wa mawazo. Nguo zilichakaa. Nywele zikazidi kichwani. Viatu vikachaa nikawa mchafu kupindukia. Niliondoka buguruni nikahamia Sudan pale karibia na Giraffe hotel. Nikawa nakaa najibana pale usiku unapoingia. Pale mambo yalikuwa mabaya zaidi. Ni bora hata buguruni. Kuna maeneo Dar hii ni kama jehanamu. Uchafu unaofanyika ni wa viwango vingine kabisa.

Baada ya kukaa muda mrefu huku nikimuwaza na kumtafuta mke wangu bila mafanikio, 2022 mwezi wa sita, nikiwa na hali mbaya kabisa, nilimuomba jamaa fulani hivi eneo la mtongani anisaidie simu yake nimpigie mke wangu. Namba ya mke wangu ilikuwa inapatikana. Niliongea nikamuomba anisaidie shilingi elfu 10. Nilikuwa na njaa sana. Mke wangu alinicheka sana.
 
Sehemu ya saba
Baada ya kunicheka aliniuliza kama ananitumia kwa ile namba. Akatuma elfu 10 na kisha akanitumia ujumbe kwamba yupo na mpenzi wake kwahiyo nisiwe nampigia simu. Nilimshukuru na kumtakia maisha mema. Nilimuomba anisaidie nyaraka zangu za kitaaluma na akanielekeza sehemu ambapo nitazipata.

Nipokea nyaraka zangu. Wakati huu nilikuwa nimechoka. Nilikonda na kuwa mtu wa ajabu kabisa. Kutoka kuvaa suti karibia siku tano za wiki na kufikia kuwa katika mavazi machafu yasiyoelezeka. Nilivaa ndala zilizofungwa na kamba.

Wakati fulani nikiwa katika mawazo mazito, niliamua kutaka kujiua lakini kwanza nikatafuta simu niongee na mtoto wangu niliezaa na Upendo. Mtoto wangu alinisalimia kisha akaniambia kwamba, "Dad, you promised to come back for me. Please remember that I miss you". Nililia sana siku ile na nikaamua kuendelea kupambana.

Nitawataja watu wachache hapa maana najua ni kwa nia njema. Wakati nahangaika, nilitafakari kukutana na kaka yangu mmoja hapa JF. Sikuwahi kuwasiliana nae kabla lakini moyo ulinisukuma kuongea nae. Nilitamani anisaidie viatu ili nipate kwenda kwenye sehemu moja ambayo nilialikwa kwa ajili ya interview. Nilimu-pm akaniomba tuonane kibada. Nilitembea kutoka rangi tatu hadi kibada kwa mguu.
Ilikuwa bahati mbaya maana siku ile hakunipa viatu kama nilivyoomba. Alinitazama kisha akanipa elfu 10. Nilikuwa na njaa sana. Nilikuwa sijapata chakula kwa muda mrefu. Nilitumia ile pesa kiasi kupata chakula pale kibada. Baada ya kuwasiliana tena, aliniomba nifike kibaha. Nilitembea tena kwa mguu hadi kibaha. Nilichoka sana. Alinipa nguo pamoja na viatu. Brother Jr., asante sana na Mungu akubariki.

Nilikuwa na jamaa yangu mwingine yupo humu anaitwa clearmind. Nilisoma nae na alikuwa mtu wangu wa karibu sana. Nakumbuka kipindi anataka kunisaidia aligombana sana mchumba wake na kwa bahati mbaya wakaachana. Niliumia sana nikaogopa kuendelea kumuomba msaada.

Nilipona msongo wa mawazo. Nipo Dar napambana. Sipo kama nilivyokuwa japo hali bado ni ngumu sana. Nina imani nitarejea tena upya. Yaliyotokea yote katika maisha yangu nayaangalia kama changamoto mpya zinazonijenga kuelekea kwenye hatima yangu iliyo njema zaidi. Nimejisikia amani kushea nanyi safari yangu hii ambayo imekuwa na matukio mengi ya kuumiza. Asanteni sana na Mungu awabariki.
Vintage1q.
Enjoy your life to the fullest today because tomorrow's never promised!
 
Sehemu ya saba
Baada ya kunicheka aliniuliza kama ananitumia kwa ile namba. Akatuma elfu 10 na kisha akanitumia ujumbe kwamba yupo na mpenzi wake kwahiyo nisiwe nampigia simu. Nilimshukuru na kumtakia maisha mema. Nilimuomba anisaidie nyaraka zangu za kitaaluma na akanielekeza sehemu ambapo nitazipata.

Nipokea nyaraka zangu. Wakati huu nilikuwa nimechoka. Nilikonda na kuwa mtu wa ajabu kabisa. Kutoka kuvaa suti karibia siku tano za wiki na kufikia kuwa katika mavazi machafu yasiyoelezeka. Nilivaa ndala zilizofungwa na kamba.

Wakati fulani nikiwa katika mawazo mazito, niliamua kutaka kujiua lakini kwanza nikatafuta simu niongee na mtoto wangu niliezaa na Upendo. Mtoto wangu alinisalimia kisha akaniambia kwamba, "Dad, you promised to come back for me. Please remember that I miss you". Nililia sana siku ile na nikaamua kuendelea kupambana.

Nitawataja watu wachache hapa maana najua ni kwa nia njema. Wakati nahangaika, nilitafakari kukutana na kaka yangu mmoja hapa JF. Sikuwahi kuwasiliana nae kabla lakini moyo ulinisukuma kuongea nae. Nilitamani anisaidie viatu ili nipate kwenda kwenye sehemu moja ambayo nilialikwa kwa ajili ya interview. Nilimu-pm akaniomba tuonane kibada. Nilitembea kutoka rangi tatu hadi kibada kwa mguu.
Ilikuwa bahati mbaya maana siku ile hakunipa viatu kama nilivyoomba. Alinitazama kisha akanipa elfu 10. Nilikuwa na njaa sana. Nilikuwa sijapata chakula kwa muda mrefu. Nilitumia ile pesa kiasi kupata chakula pale kibada. Baada ya kuwasiliana tena, aliniomba nifike kibaha. Nilitembea tena kwa mguu hadi kibaha. Nilichoka sana. Alinipa nguo pamoja na viatu. Brother Jr., asante sana na Mungu akubariki.

Nilikuwa na jamaa yangu mwingine yupo humu anaitwa clearmind. Nilisoma nae na alikuwa mtu wangu wa karibu sana. Nakumbuka kipindi anataka kunisaidia aligombana sana mchumba wake na kwa bahati mbaya wakaachana. Niliumia sana nikaogopa kuendelea kumuomba msaada.

Nilipona msongo wa mawazo. Nipo Dar napambana. Sipo kama nilivyokuwa japo hali bado ni ngumu sana. Nina imani nitarejea tena upya. Yaliyotokea yote katika maisha yangu nayaangalia kama changamoto mpya zinazonijenga kuelekea kwenye hatima yangu iliyo njema zaidi. Nimejisikia amani kushea nanyi safari yangu hii ambayo imekuwa na matukio mengi ya kuumiza. Asanteni sana na Mungu awabariki.
Vintage1q.
Enjoy your life to the fullest today because tomorrow's never promised!
Man utakua tajiri na kiongozi mkubwa sana!

Hope tutakuja kufanya KAZI office Moja na tutakua team wazalendo!

Nadhani utaniunga mkono kwenye dhamira yangu ya kupunguza mapesa mengi kulipa wanasiasa mishahara na maposho kibao wakati huduma za kijamii zinalega lega!!

Paulo mtume anaandika"najua kushiba na kuona njaa" akielezea Kwa kina mapito yenye maumivu meengi!

Tunapitia nyakati kama hizo maishani ili tukipata tuelewe Hali zote wanazopitia watu wote Ili tuwe msaada!!

See you at the top!! Trust me nitakutafuta ngoja kwanza litimie neno fulani!!
 
Man utakua tajiri na kiongozi mkubwa sana!

Hope tutakuja kufanya KAZI office Moja na tutakua team wazalendo!

Nadhani utaniunga mkono kwenye dhamira yangu ya kupunguza mapesa mengi kulipa wanasiasa mishahara na maposho kibao wakati huduma za kijamii zinalega lega!!

Paulo mtume anaandika"najua kushiba na kuona njaa" akielezea Kwa kina mapito yenye maumivu meengi!

Tunapitia nyakati kama hizo maishani ili tukipata tuelewe Hali zote wanazopitia watu wote Ili tuwe msaada!!

See you at the top!! Trust me nitakutafuta ngoja kwanza litimie neno fulani!!
Amina mtu wa Baba
 
Dah wanawake ni hatari kuliko bomu la nuclear,,,,,
Mkuu kuna kitu sijaelewa vizuri,,,
Kuhusu Pesa uliyoikusanya kwa ajiri ya kuja kujiajiri dar es salaam, umeandika uliiweka kwenye sanduku la chuma, natamani kujua ilikuwa kama kiasi gani? Na Yasinta ndio aliondoka nayo akaemda kwa huyo mpenzi wake???
 
Dah wanawake ni hatari kuliko bomu la nuclear,,,,,
Mkuu kuna kitu sijaelewa vizuri,,,
Kuhusu Pesa uliyoikusanya kwa ajiri ya kuja kujiajiri dar es salaam, umeandika uliiweka kwenye sanduku la chuma, natamani kujua ilikuwa kama kiasi gani? Na Yasinta ndio aliondoka nayo akaemda kwa huyo mpenzi wake???
Yasinta aliondoka nayo yote
 
Back
Top Bottom