Maisha ya ndoa na familia

Pole na hongera ndugu.
Endelea kupambana.
 
Pole sana braza Kwa mapito yako magumu lakini naimani umeyaweka hapa ili tujifunze.
Kuna vitu tunavifanya kama wanaume vinakuja kuwa bakora maisha yetu yote. Kosa la kwanza umelifanya kipindi upo na pendo ni kumuonesha kuwa Kuna mtu unamjali na kumthamini kuliko hata yeye na wazazi wako.
Kipindi umemsimasha asiende nyumbani kwenu aanze Kwa rafiki Dodoma umemfanya apate interest yakutaka kujua ananini haswa kuwa mtu muhimu kiasi hiko akajikuta anaanguka kwenye zinaa, kosa limeanzia kwako.
Kosa la pili ni Kwa yasinta, kwanza naona alikubali kuoleea na wewe baada ya kuona upo desperate na ndoa, pia unapesa. Kitendo Cha wewe kukubali masharti yake Yani kubadili dini na kimfuata manyara ulikuea umeingia kwenye mtego wake na kukuona anaweza kukuongoza sio wewe kumuongoza yeye.
Mwanaume lazima uwe na misimamo yako. Mwenye kuweza kuifuata tunaanza kumconsider.
 
Ni kweli, nilifanya makosa kadhaa. Nina imani kuna jambo la kujifunza kwa wengine na ndio maana nimeshea hapa. Asante sana.
 
Asante! "Makambi 2024 nitakwenda mimi na familia yangu". Rudi kundini mkuu.

Turudi kwenye mada, Jipange upya mkuu ukizingatia una binti anayekutegemea. Na kamwe usikubali mwanamke akuamulie mambo kama ilivyotokea kwa Yasintha.
 
Nilidhani ni story ya kutunga hadi ulipowahusisha member wa humu jukwaani, na nilitamani iwe ya kutunga kwa vile inaumiza sana mtu kupitia yote haya.

Mkuu, pole sana. Itunze imani yako, siku yako yaja na haya yote yatabaki historia badala ya maumivu.
 
Hii ni sehemu tu kati ya mengi. Nawashukuru sana wachache walionifikia.
 
Asante utafanikiwa sana
 
Pole sana mkuu kwa maswaibu unayopitia..but kosa kubwa unalofanya ww ni kuwapa kipaumbele sana wanawake kuliko kusudi la maisha Yako..

Nimekunote umesafiri mara kadhaa kufata mwanamke badala yy ndio akufate... unawezaje kuhama mji kufata mwanamke badala yy ndio akufate... unawezaje kubadili dhehebu kufata la mwanamke...

Sikia nikwambie unauza mamlaka Yako uliyopewa na Mungu ya uongoz na utawala kwa wanawake kisa mapenz,, hvo Mungu hawez kukusaidia kwa chochote sabb badala ya kumsikiliza yy unasikiliza wake zako...kama esau na yakobo,,esau kauza baraka zake sabb ya msosi alipokuja kuzililia halikuwezekana..

Sanduku la pesa I mean hazina Yako ilikuaje unamkabidhi mke na nyaraka zako pia...inafikirisha sana!!

Simamia kama mwanaume acha hayo mambo ya kupetpet mwanamke...

Mwisho uligundua mke anakusalit na kiongozi wa kanisa asa ulikua unasubir nn kumlima talaka.. mwanamke msaliti hasameeki never ever!!!!
 
Hivi ni kweli ID yako inasadifu dhamira yako? I wish to work with you. If you don't mind pm me..
 
VINTAGE, unahisi ulikosea wapi kama Mwanaume?

Ungependa vijana wa kiume ambao bado hawajaoa wajifunze nini kwenye story ya maisha yako ?
 
How a man can place his purpose above his woman?

Je maumivu ya kufeli biashara yako yanaweza kuwa makubwa kuliko ku divorce na mke wako?

Nifundishe mimi nipo tayari kupokea ushauri wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…