Kuna mshikaji wetu mmoja alimlaza mkewe ndani kwa makosa ya kijinga kijinga tu ya maisha ya ndoa... kesho yake tukaenda kumsalimia shemeji yetu tukamkuta pale nje kituoni so tukatoka naye tukaenda kupata supu jirani na kituo cha police.
Kwenye supu akatuambia sasa nawapa salaam, mpigieni simu mshikaji wenu mwambieni ya yeye leo ni zamu yake, tukacheka tukasema shemeji si yaishe tu haya mambo kifamilia, akagoma akasema na yeye lazima aje kunyea debe leo afu ndiyo tuangalie namna ya kuyamaliza.
Aisee kweli bana kabla hata hatujaondoka jamaa kafika na V8 lake, fasta bin vuu vua mkanda, kaa chini .. unapiga mkeo wewe bila makosa... mzee mzima akasonda ndani - sisi tukaendelea kupata ngano na shemeji yetu huku tukimsihi amtoe akagoma, tukakaa pale hadi saa 4 usiku ikashindikana kumtoa ikabidi tuondoke
Asubuhi yake tukafika pale ili tuone kama kesi itakwenda mahakamani, basi kuongea huku na huku yule afande akawaita wote akawaambia naona sasa kila mmoja karidhika - sasa nendenei mkayamalize nyumbani.
Jamaa akawasha V8 lake akasepa, huku shem na yeye akawasha BMW na yeye akasepa - sisi tukaona tuwaache kwanza then tuwatafute jioni tuone wamefikia wapi.
Basi ilipofika saa 11 jioni tukamcheki mshikaji akatuambia yupo sehemu tuende, tukafika pale tukawakuta yeye na mkewe wanapata Kmoto na moja moto moja baridi... asiee dunia hii.
mambo ya ndoa ni magumu sana.