Maisha ya ndoa yana changamoto nyingi sana.

Maisha ya ndoa yana changamoto nyingi sana.

kuna muda mkewe aliondoka home kwa hasira yeye na dada wa kazi akahamia hotelini, mshikaji akabaki na watoto ( 6, 3) akawa anawalisha chipsi mchana na usiku - tukamwambia kaka utawaua hawa watoto, wapeleke kwa mama yao hotelini.
Hiyo ndoa hiyo ni balaa.The comical marriage!Pwagu na Pwaguzi.
 
kuna muda mkewe aliondoka home kwa hasira yeye na dada wa kazi akahamia hotelini, mshikaji akabaki na watoto ( 6, 3) akawa anawalisha chipsi mchana na usiku - tukamwambia kaka utawaua hawa watoto, wapeleke kwa mama yao hotelini.
tutafika paradiso tukiwa hoi aisee hizi ndoa
 
Wanapendana kinafki mgawo wa Mali unawazuia kuachana
 
Wale jamaa wa Centro wanaogopa V8 sio mchezo..
Hiyo chai kabisa Dingi V8 maza BMW hawawezi kufanya michezo ya kijinga namna hiyo
Mke ana hela mume ana hela sasa wale wanakomoana na askari washawajua si mara moja kufikishana pale kwa kesi za sampuli hiyo.

Afu usiwe na mawazo kwamba mtu mwenye V8 hawezi kulala ndani..futa mawazo hayo kabisa.
 
Wanapendana kinafki mgawo wa Mali unawazuia kuachana
Wanapendana kweli ila mshikaji wetu
chai...unajua ukiwahi kupata pesa kwa umri chini ya 40 ni balaa..ni wachache sana wanaweza kuhimili hali.

Wewe ushawahi ku date mtoto Dar afu mkapanga mkutane walau Mza kula maisha?

Sasa mwenzio mzigo unamfuata Dubai au hata UK, popote anapotaka kwenda kula bata..

Hapa ndipo tatizo linapoanzia
 
Kuna mshikaji wetu mmoja alimlaza mkewe ndani kwa makosa ya kijinga kijinga tu ya maisha ya ndoa... kesho yake tukaenda kumsalimia shemeji yetu tukamkuta pale nje kituoni so tukatoka naye tukaenda kupata supu jirani na kituo cha police.

Kwenye supu akatuambia sasa nawapa salaam, mpigieni simu mshikaji wenu mwambieni ya yeye leo ni zamu yake, tukacheka tukasema shemeji si yaishe tu haya mambo kifamilia, akagoma akasema na yeye lazima aje kunyea debe leo afu ndiyo tuangalie namna ya kuyamaliza.

Aisee kweli bana kabla hata hatujaondoka jamaa kafika na V8 lake, fasta bin vuu vua mkanda, kaa chini .. unapiga mkeo wewe bila makosa... mzee mzima akasonda ndani - sisi tukaendelea kupata ngano na shemeji yetu huku tukimsihi amtoe akagoma, tukakaa pale hadi saa 4 usiku ikashindikana kumtoa ikabidi tuondoke

Asubuhi yake tukafika pale ili tuone kama kesi itakwenda mahakamani, basi kuongea huku na huku yule afande akawaita wote akawaambia naona sasa kila mmoja karidhika - sasa nendenei mkayamalize nyumbani.

Jamaa akawasha V8 lake akasepa, huku shem na yeye akawasha BMW na yeye akasepa - sisi tukaona tuwaache kwanza then tuwatafute jioni tuone wamefikia wapi.

Basi ilipofika saa 11 jioni tukamcheki mshikaji akatuambia yupo sehemu tuende, tukafika pale tukawakuta yeye na mkewe wanapata Kmoto na moja moto moja baridi... asiee dunia hii.

mambo ya ndoa ni magumu sana.
Wanapozana 😂🤣🤣
 
Back
Top Bottom