Maisha ya Osama kabla hajakamatwa yafichuliwa

hata nikikuambia hautonisadiki...
utakuja na swali jingine unaweza kuniuliza nitajie majina ya walio kuwa kwenye msiba wake au utaniuliza alizikwa saa ngapi? au unaweza ukaniuliza hitma yake ilikuwa ni lini?
bwana Ritz unachekesha sana...
Siku zote watu wa magharibi huwa wanasema ukimiliki media unamilki na akili za watu hebu soma hii.
 
Mkuu wa chuo,

Wewe ndiyo umeandika kuwa kazikwa baharini mimi nimesoma mabandiko yako ndiyo maana nikajenga maswali wewe ndiyo umeyasema hayo.
inasemekana Osama alizikwa baharini na hata wavuvi hakuna aliyeona hilo tukio...

sasa unaponiuliza sehemu gani nashindwa kukujibu...
Sasa unapoleta jambo ukumbini si lazima huwe na ushahidi nalo utapoulizwa maswali.
labda wewe unaweza kujua ni sehemu gani alizikwa yamkini unaweza kutupa maelezo wewe unafahamu kwani ni bahari sehemu gani?
Mimi ninachojua baharini watu huwa hawazikwi.
kwasababu kuna story zilitoka tofauti na hiyo mimi naziita ni za uongo zinasema eti Osama alikufa muda mrefu wala sio kwa ile operation eti ni kwa ugonjwa...
Ni vizuri sasa wewe ukaja na story za ukweli kuhusu kifo cha Osama, tujifunze kutoka kwako.
Sasa swali linakuja mbona baada ya ile mission Al Zawahir ikatangazwa kuchukua nafasi ya Osama?
Nani alitangaza kuwa Ayman Mohammed Rabie al-Zawahiri kachukuwa nafasi ya Osama?

CC. kahtaan,
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wa chuo unapo sikiliza habari ambayo huna ushahidi nayo basi kama una busara unaiacha kama ilivyo!
Sasa kama watu wamekupa habari pamoja na ushahidi wenyewe nitaachaje bila kuhoji bwana kahtaan?
Kwa mfano! Hii habari hapa ! Je wewe Mkuu wa chuo uko tayari kwenda mahakamani kutoa ushahidi kuwa wale wanajeshi walimuua yule usama!?!
Ushahidi upo kuna ushahidi wa vyombo vya habari vilivyotangaza na wewe una ushahidi gani kama hawakummuua? vinginevyo useme kama na mimi nilikuwepo nilishuhudia kwa macho on spot wakati operation inafanyika hapo sikushuhudia, lakini kama evidence zipo zimeletwa...
Unaweza kuleta opinion zako kutokana na kupima mambo kwa kutumia akili Mungu aliyo kupa!
Lkn sio uuite ushahidi!
ni kweli unavyosema na mimi ndicho ninachokifanya nipo na pima tukisaidiana na nyie pia... ili tuweze kufika hitimisho...
hapo unaweza tupa darsa zaidi bwana kahtaan tutashukuru sana...
Leo hii auwawe kwa kupigwa risasi halafu kaburi lake liwekwe mafichoni!?
Na istoshe vyombo vya habari vimekata habari zake zoote!
nafikiri sababu zimewekwa wazi za kufanya hivyo, we ulitaka vyombo vya habari vifanyeje sasa kwa mfano je viwe vinatangaza sikuzote habari zake?
We hata machale hayakuchezi na ukajiuliza nini kinaendelea hapa!?
Machale yananicheza ndio maana tupo tunajaribu ku reasoning...
Basi tu kwasababu Cnn na Abc na Wale paka Fix(fox )news wamesema hivyo baaasi! Sisi huku kwa sababu km unavyosema tuko dunia ya kariakoo tukubali tu!
Sasa inabidi mpinge kwa sababu sio kwa kubisha tu mpinge mkiwa na sababu...
Alllaaa! Na sie tumeenda shule bwana!
Inabidi muonyeshe sasa hapa kwamba mmeenda shule...
Hawa si walisema wamekwenda mwezini miaka ya 60'
Mbona wametokea scientists kulipinga hilo na mpaka leo 2013 hawajaamua kuuonyesha ulimwengu wakatuma tena wale wanaojifanya kurukaruka kama ndege mwarabu! Angani!
Hao scientists ni wa wapi tunaomba darsa hapo kidogo, kumbe jamaa huwa wanarukaruka kama ndege Mwarabu?
Walikuja wakawaambia mababu zetu! "Fungeni macho tuombe" wazee maskini wakafunga!
mababu zenu wa wapi? basi walikuwa ni wajinga vinginevyo kama sijakuelewa..
Kuja kufungua! Hamadi! Wameondoka na dhahabu na almasi zoote!
Sisi wametuachia "andiko" na nyimbo kwa wingi!
hebu niambie hii migodi ya Almasi na Dhahabu imeanza lini? yaani juzi juzi watu wameshakuwa mababu kweli? Inamaana na Almasi na dhahabu zote wamemaliza, kwa hiyo hapo we ni full kuimba ma nyimbo tu?
Kwa kuwa na imani kama zako ndio maana hawa jamaa waliweza kutawala na kuwatumikisha ma babu zetu!
Leo tumeamka! Kama kuna habari inautata lzm tuulize!
Kunani paleee!?
kwani utata upo? ni kweli Osama bin Laden ameuawa hapo hakuna utata...
Kama alivyo elezea mkuu Ritz

Ni hayo tu Mkuu wa chuo.
Mbona Ritz bado sijamwelewa ameeleza nini?
 
mkuu kahtaan amekwisha nirekebisha hapa chini kama atakuwa yupo sahihi....
Mkuu wa chuo,
Nani alitangaza kuwa Ayman Mohammed Rabie al-Zawahiri kachukuwa nafasi ya Osama?

CC. kahtaan,
Hebu soma hichi kipande hapa chini
 
Last edited by a moderator:
mkuu kahtaan amekwisha nirekebisha hapa chini kama atakuwa yupo sahihi....


Hebu soma hichi kipande hapa chini

Bandiko lako ambalo unalitumia kama ushahidi umelitoa kwenye wikipedia limeandikwa na hao wazungu wenyewe.

Nakushauri kitu kimoja wasome na huwafahamu Al-Qaeda's network ni kina nani.

Twende taratibu tujadiliane.

Unajua chochote kuhusu walioshambulia WTC Manhattan, New York Marekani chanzo cha haya yote yalianzia apo.
 
Last edited by a moderator:

Unajua Mkuu wa chuo hapa tunazunguka palepale.
Na kutokana na maelezo yangu umeniuliza maswali ambayo itasababisha topic zingine ndeefu kabisa.

Nadhani nirudie mara ya mwisho!

Vitu unavo viona kwenye kwenye tv huwezi hata siku moja kuviita ushahidi!

Eti kwa sababu tv imetangaza!

Unakumbuka uchaguzi wa rais mwaka km sijakosea ni 1998. DTV walitangaza kuwa Seif sharifu ndio mshindi wa urais zanzibar!

Matokeo yakawa sivyo DTV walivyotangaza!

1947 Fix (Fox tv news channel) America

walionyesha kuwa wanamfanyia ALIEN autopsy! Eti Baada ya alien space shuttle kuanguka!!
Na watu wa magharibi juu ya elimu walizonazo karibu woote wakaamini kuwa kuna aliens!
Na mpaka leo tv nyingi za magharibi zinaonyesha footage za flying objects wakidai kuwa ni aliens!
Hata siku moja bahati mbaya isitokee mtu wa kawaida akamuona huyo alien! ?!

Huna haja ya ushahidi kuhitimisha kuwa hili ni la uongo!
Unatakiwa utumie nguvu ya fikra tu!

Ndo maana wakati mwingine Hakimu anatoa hukumu kwa kutumia fikra bila ushahidi wa wazi, anapo orodhesha facts from fictions!

Na mifano mingi tu!

Tunapo pokea habari hasa habari kubwa kama hii ya usama! Sio kuruka tu na kukubali na ukiulizwa unasema nimeona kwenye tv!
We kama utaamini iwache hiyo habari ibaki ndani ya tv! Ukiitoa nje ukasema una ushahidi hapo ndipo unapojiweka ktk mazingira magumu kabisa!

Vyombo vya habari vinatawala vichwa vya watu na lolote watakalotaka kuufahamisha umma. Basi hakuna wa kuwazuia!

Mbona tumeskia mengi ya uzushi kutoka ndani ya vyombo vya habari miaka mingi tu!
Na yule mwenye kuipinga hio habari kutokana na utata wake wewe huna haki ya kumlazimisha kutoa ushahidi wakati wewe ya kwako pia haina ushahidi ispokuwa umeona tu ndani ya tv!
 
Last edited by a moderator:
ni kweli hizo ndio source zilizopo na source zinginezo zinasema hivyo vinginevyo utupatia source zingine zenye kuaminika zinazosema tofauti na hivyo, inasemekana ni mtandao wa al qaeda ndio ulihusika pamoja na ile milipuko ya Dar es salaam na Nairobi 1998, lakini kuna habari moja nimeiona mwana jf mmoja ameileta hebu isome hapa chini inahusiana na Rockafeller family, chukua kipande hicho kidogo...
Sasa hapo tuanze kuchambua kwa undani zaidi, na wewe njoo na evidence pamoja na source zako...
 

Hii ni topic ndeefu ambayo hatomfadisha yyt humu!
Nadhani ili kutafuta hitimisho naomba nikuulize swali moja fupi tu Mkuu wa chuo !
Je! Unakubali kuwa mataifa Waongo wanaoongoza ktk Dunia hii ku manipulate jamii na walimwengu kwa ujumla kwa faida zao binafsi ni MATAIFA YA MAGHARIBI!?

Kama utanipa jibu la KWELI hapa,! nadhani huu mjadala utafikia ukingoni
 
Last edited by a moderator:
bwana kahtaan ngojea nikuulize swali wewe habari za Malcom X ulizipata wapi?
 
Last edited by a moderator:
ku manipulate jamii kivipi? kwani we kwa mtazamo wako na fikra zako habari hizi kwamba za Osama ameuawa ni za kweli ama ni uongo?

au bwana kahtaan we ukweli upi unao ujua au habari unazo ziamini ni zipi?
 
Last edited by a moderator:
bwana kahtaan ngojea nikuulize swali wewe habari za Malcom X ulizipata wapi?

Kuna vitabu vyake vinaelezea maisha yake kuna kitabu cha Alex Hailey.

Sasa kuna Reinveting Malcom X.

Waandishi wameandika kupitia familia ya Malcom X.
 
Last edited by a moderator:
Ila yote kwa yote osama alikuwa kiboko ya njia!
 
Unamwagiwa umbea unashangilia tu. Habari za alkaeda ni puzzle na wengi wanatengeneza tu. Kama alivyotengeneza Obama kumuua Osama aliyekufa more than 2 year ago.


Mkubwa, weka na ya kwako hapa tulinganishe na kuchambua. Hakuna kosa na wewe ukatoa maelezo pale unapodhani jamaa kakosea, karuka ama ukaifuta yote ya kwake na kutoa mwelekeo mpya.
 
Nitarudi tena stori ikibadilika
"VV"
hebu jipumzishe na huu wasifu kidogo tukiendelea kujadiliana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…