Maisha ya Osama kabla hajakamatwa yafichuliwa

Maisha ya Osama kabla hajakamatwa yafichuliwa

Hii ni topic ndeefu ambayo hatomfadisha yyt humu!
Nadhani ili kutafuta hitimisho naomba nikuulize swali moja fupi tu Mkuu wa chuo !
Je! Unakubali kuwa mataifa Waongo wanaoongoza ktk Dunia hii ku manipulate jamii na walimwengu kwa ujumla kwa faida zao binafsi ni MATAIFA YA MAGHARIBI!?

Kama utanipa jibu la KWELI hapa,! nadhani huu mjadala utafikia ukingoni

Hapa unaatupeleka kwa mambo ya ubishi na matamanio ya kina Lipumba na propaganda zake msikitini eti akiwa raisi atawafanya waislam wawe daraja la kwanza sijui nini.. Uwongo uwongo tu, maneno yasiyokuwa na facts wala mwelekeo ili mradi basi tu.
 
Kuna vitabu vyake vinaelezea maisha yake kuna kitabu cha Alex Hailey.

Sasa kuna Reinveting Malcom X.

Waandishi wameandika kupitia familia ya Malcom X.
vivyo hivyo na hii habari pamoja na operation yote ya kumshoot Osama ipo kwenye vitabu pia moja wapo ya kitabu kinaitwa No easy day...

mkuu RealMan aliweka attachment ya hicho kitabu na mimi nimekipata hapo waweza pitia kwenye mabandiko yake ukakiperuzi sio mbaya kuperuzi upate source nyingi zaidi...
 
Last edited by a moderator:
ku manipulate jamii kivipi? kwani we kwa mtazamo wako na fikra zako habari hizi kwamba za Osama ameuawa ni za kweli ama ni uongo?

au bwana kahtaan we ukweli upi unao ujua au habari unazo ziamini ni zipi?

Suala si habari zipi naziamini !
Hapa wote mimi na wewe, sisi wote tumeona kwenye tv!
Tofauti yetu ni kuwa mimi na Ritz tunayachuja maelezo ya hao jamaa kutokana na utata wa habari yenyewe!

Wewe umebeba nzima bila shaka hata kidogo na pia unaitetea kwa kusema ni ushahidi!
Na una haki ya kuleta mawazo yako!

Lkn kama nikikwambia wewe kam unahakika na habari hii basi toa pesa zako zoote na mimi nitoa zangu zoote tukatafute ukweli!

Na kama itaonekana kuwa si kweli pesa zako zitapotea zote.
Hapo nina imani UTAJIULIZA UHAKIKI WA HII HABARI MARA MBILIMBILI!

ni hilo tu!
 
Last edited by a moderator:
unaposema hakuna mwenye akili timamu akayapinga unamaanisha kwamba tunaoyapinga basi ni wendawazimu?

Hiyo umesema wewe ndugu Mkuu wa chuo.
Na wala wewe ujapinga maneno ya kuwa watu hurubuniwa sana na media!
Au unakataa kama hizi media zinachangia kurubuni jamii!
Na mifano hai nimekupa hapo nyuma??
 
Last edited by a moderator:
Hapa unaatupeleka kwa mambo ya ubishi na matamanio ya kina Lipumba na propaganda zake msikitini eti akiwa raisi atawafanya waislam wawe daraja la kwanza sijui nini.. Uwongo uwongo tu, maneno yasiyokuwa na facts wala mwelekeo ili mradi basi tu.

Sasa suala la huyo lipumba sijui waislamu limetokea wapi kwenye uzi huu!?

Hebu Mkuu wa chuo muulize huyu mheshimiwa!
We umeshawahi kuona mi naleta siasa humu??
Usitake kutuchafulia uzi hapa!
Huna la maana la kuongea basi kuwa mtazamaji tu!

Si lazima utuletee udini kila sehemu.

Watanzania lini mtabadilika na kuwa na busara za kujenga hoja bila kuleta udini??
 
Last edited by a moderator:
bwana kahtaan ngojea nikuulize swali wewe habari za Malcom X ulizipata wapi?

Its strange umemchagua Malcom X.

Maisha ya huyu bwana yamehifadhiwa kwenye nyanja mbalimbali na historia yake wanasomeshwa wanafunzi across america na nchi zingine.
Maisha yake yako wazi kwa kila mwenye kujua historia across the globe. !

Maisha ya huyu muheshimiwa sio tukio la mara moja. Na hakuna cha ajabu ktk historia yake kikakusababisha ukajiuliza maswali halafu ukakosa jibu.

Mungu ailaze roho ya ALHAJ MALIK SHABAZ also know as MALCOM X.
Mahali pepa kabisa! Peponi.
Amin.

Nadhani nimekujibu Mkuu wa chuo .
 
Last edited by a moderator:
Sasa suala la huyo lipumba sijui waislamu limetokea wapi kwenye uzi huu!?

Hebu Mkuu wa chuo muulize huyu mheshimiwa!
We umeshawahi kuona mi naleta siasa humu??
Usitake kutuchafulia uzi hapa!
Huna la maana la kuongea basi kuwa mtazamaji tu!

Si lazima utuletee udini kila sehemu.

Watanzania lini mtabadilika na kuwa na busara za kujenga hoja bila kuleta udini??

Si kila sehemu ukitajwa uislam ama upagani basi ni suala la udini. Suala kubwa ni similarities za groundless za arguments za huyu anayekataa hoja yenye source kwa kubisha bila substitute namna zinavyofanana na stories za kina lipumba na wenzake ambazo coincidentally zilifanyika msikitini. Wala hapa hakuna udini wowote. Usikariri.
 
Suala si habari zipi naziamini !
Hapa wote mimi na wewe, sisi wote tumeona kwenye tv!
Tofauti yetu ni kuwa mimi nayachuja maelezo ya hao jamaa kutokana na utata wa habari yenyewe!
Wewe umebeba nzima bila shaka hata kidogo na pia unaitetea kwa kusema ni ushahidi!
Na una haki ya kuleta mawazo yako!
Lkn kama nikikwambia wewe kam unahakika na habari hii basi toa pesa zako zoote na mimi nitoa zangu zoote tukatafute ukweli!
Na kama itaonekana kuwa si kweli pesa zako zitapotea zote.
Hapo nina imani UTAJIULIZA UHAKIKI WA HII HABARI MARA MBILIMBILI!

ni hilo tu!
bwana kahtaan umesema mambo unachuja tupatie basi hata hivyo vilivyofanikiwa kupita kwenye chujio lako tuweze kuchambua na kujadili...

wakati tukisubiri kupata vilivyo pita kwenye chujio lako hebu chukua hicho...
ISLAMABAD, Pakistan

MAKOSA na uzembe wa Pakistan ziliruhusu kiongozi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda, Osama bin Laden, kuishi nchini humo bila kutambulika kwa zaidi ya miaka tisa, ripoti mpya inaonyesha.

Ripoti hiyo ya jopo la mahakama ya Pakistan pia inatoa maelezo mapya kuhusu uvamizi wa Amerika uliomwua bin Laden.

Pia yadondoa mambo mengine ya kusisimua kuhusu maisha ya gaidi huyo ikiwemo kwamba alivalia kofia aina ya cowboy ili kukwepa upelelezi wa setilaiti za Amerika.

Wapelelezi wa shirika la kijasusi la CIA walimfuatilia bin Laden hadi mji wa kaskazini magharibi wa Abbottabad.

Ni hapa alikopigwa risasi na kuuawa na wanajeshi wa Amerika wanamaji wa kitengo spesheli (SEALs) Mei 2, 2011.

Ulikuwa uvamizi wa kuvutia uliotokea karibu na chuo cha kijeshi cha Pakistan.

Aidha, lilikuwa tukio la kufedhehesha mno katika historia ya Pakistan na kupelekea taifa hilo kukumbwa na madai ya uzembe ama kula njama na Al-Qaeda ili kumficha mtu huyo aliyekuwa akisakwa zaidi duniani.

Serikali ilizindua jopo muda mfupi baada ya uvamizi huo bunge lilipodai kufanywe uchunguzi huru.

Lilihoji maafisa wakuu wa serikali na jeshi na wajane watatu wa bin Laden kabla yao kufukuzwa hadi nchini Saudi Arabia.

Lakini ripoti ya jopo hilo ilifanywa siri hadi kituo cha habari cha Al-Jazeera kilipochapisha Jumatatu.

“Uzembe unaostahili adhabu katika viwango vyote vya serikali kwa kadiri waweza kuthibitika katika ushahidi,” ripoti hiyo ya kurasa 336 ilisema.

Jopo lilisema halikupata ushahidi wa madai ya njama lakini halikuondoa uwezekano wa “ 'kanusho la kukubalika’ la usaidizi” kutoka kwa maafisa wa sasa ama wa zamani.

Bin Laden alihepa uvamizi wa 2001 nchini Afghanistan ulioongozwa na Amerika. Aliwasili Pakistan 2002 na kuishi maeneo ya mpakani na Afghanistan, wilaya za kaskazini magharibi za Swat na Haripur.

Pia yawezekana aliishi maeneo mengine kabla kuamua kupiga kambi Abbottabad mwezi Agosti 2005.

Kufikia 2005 hiyo, shirika la ujasusi la Pakistan (ISI) lilifunga faili ya msako wa kiongozi huyo mkuu wa Al-Qaeda.

Kupuuzwa

Shutuma za kigeni kwamba yawezekana bin Laden yuko Pakistan zilipuuzwa na serikali ya wakati huo ya kiongozi wa kijeshi Pervez Musharraf.

Ushahidi wa wake zake wasema bin Laden alipohisi mgonjwa alijitibu kwa dawa za kienyeji za Kiarabu, na “alipojihisi mchovu angekula tufaha pamoja na chokoleti”

Alifuata maadili kabisa na kuelekeza elimu ya watoto na wajukuu wake “iliyojumuisha kukuza shamba dogo la mboga huku akiwapa zawadi ndogo kwa matokeo mazuri.”

Baada ya uvamizi, maafisa wa Amerika walibeba vifaa vya kompyuta na vitu vingine vya kibinafsi ikiwemo dhahabu na wosia wa bin Laden.
 
Last edited by a moderator:
Its strange umemchagua Malcom X.

Maisha ya huyu bwana yamehifadhiwa kwenye nyanja mbalimbali na historia yake wanasomeshwa wanafunzi across america na nchi zingine.
Maisha yake yako wazi kwa kila mwenye kujua historia across the globe. !

Maisha ya huyu muheshimiwa sio tukio la mara moja. Na hakuna cha ajabu ktk historia yake kikakusababisha ukajiuliza maswali halafu ukakosa jibu.

Mungu ailaze roho ya ALHAJ MALIK SHABAZ also know as MALCOM X.
Mahali pepa kabisa! Peponi.
Amin.

Nadhani nimekujibu Mkuu wa chuo .
Ni sawa ni vyema ungesema utata wenyewe uko wapi? ungekuja na maswali yenye logic ya ku reasoning moja kwa moja tungeanzia hapo kuyachambua na kujibu tuweze kuona...
 
Last edited by a moderator:
Si kila sehemu ukitajwa uislam ama upagani basi ni suala la udini. Suala kubwa ni similarities za groundless za arguments za huyu anayekataa hoja yenye source kwa kubisha bila substitute namna zinavyofanana na stories za kina lipumba na wenzake ambazo coincidentally zilifanyika msikitini. Wala hapa hakuna udini wowote. Usikariri.

Bwana Tabby usinifanye mimi nina upeo mchache wa kuona reality nyuma ya hoja!

We unasema huu sio udini!

Ktk WANASIASA WOOTE wanao ahidi uongo tz!

Wewe coincidence yako imuangukie Lipumba na Waislamu tu!

Huu mfano wako ni kama wale askari wa airport. Wanasimamisha waislamu kuwa search halafu ukiuliza wanakwambia hii ni "Random search" bahati mbaya imekuangukia wewe.!!

Kwa kukuhakikishia hili kwako ntakwambia kitu halafu usidhani mi mchawi!

Wewe bwana Tabby SIO MUISLAMU!

Sasa niambie kama nimepatia au fikra zangu zina ULAKIN.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo umesema wewe ndugu Mkuu wa chuo.
Na wala wewe ujapinga maneno ya kuwa watu hurubuniwa sana na media!
Au unakataa kama hizi media zinachangia kurubuni jamii!
Na mifano hai nimekupa hapo nyuma??
hadi serikali ya Pakistan ilithibitisha hilo, kuna vyombo kama Al Jazeera kama hutaki source za magharibi...

sasa kama unaposema ambao hawakubaliani na bwana Ritz hawana akili timamu moja kwa moja unamaanisha akili zao sio timamu...

we argue with reasons, not just ubishi tu...
 
Last edited by a moderator:
bwana kahtaan umesema mambo unachuja tupatie basi hata hivyo vilivyofanikiwa kupita kwenye chujio lako tuweze kuchambua na kujadili...

wakati tukisubiri kupata vilivyo pita kwenye chujio lako hebu chukua hicho...

Bwana Mkuu wa chuo
Naona muda unanitupa mkono huku niliko na ningependa tuendelee kulumbana manake ndo raha zenyewe za sisi wa Tz tulishiba uzalendo bila kuleta udini na ushabiki usio na maana.

Ntaongezea machache tu hapa:-

Hio habari ulioniwekea hapo juu imejaa kasoro chungu mzima! Ntaorodhesha machache tu hapa.

1. Je! Inaingilika akilini serikali isitishe msako wa mtu anaetafutwa na taifa kubwa kama America na wanajeshi wake wakiwa wana operate ndani ya pakistan?
Kama sio mbinu za kuudanganya ulimwengu!
Kwa kuona kwamba kama utasem iliendelea kumtafuta! Ukimwengu ungejiuliza vipi miaka yote hiyo hajapatikana!?!

2.Unaweza kumwambia msomi yyt kuwa ilo kuepuka kunaswa na satelite za wamarekani basi we kavae kofia za cowboy mchezo umekwisha!

Teh teh teh teh!
Hapo nimeshindwa kuvumilia, imebidi nicheke!

Kama ni hivyo basi wale taleban tungewaona na makofia sio vilemba!

Na mengine mengi tu lkn muda haunifanyii hisani.

Until next time my friend Mkuu wa chuo
Nakutakia siku njema ndani ya bongoland.
 
Last edited by a moderator:
vivyo hivyo na hii habari pamoja na operation yote ya kumshoot Osama ipo kwenye vitabu pia moja wapo ya kitabu kinaitwa No easy day...

mkuu RealMan aliweka attachment ya hicho kitabu na mimi nimekipata hapo waweza pitia kwenye mabandiko yake ukakiperuzi sio mbaya kuperuzi upate source nyingi zaidi...

No easy day cha Mark Owen, nimekipitia, angalia lakini story za kina Rambo zipo nyingi.
 
Last edited by a moderator:
Bwana Mkuu wa chuo
Naona muda unanitupa mkono huku niliko na ningependa tuendelee kulumbana manake ndo raha zenyewe za sisi wa Tz tulishiba uzalendo bila kuleta udini na ushabiki usio na maana.

Ntaongezea machache tu hapa:-

Hio habari ulioniwekea hapo juu imejaa kasoro chungu mzima! Ntaorodhesha machache tu hapa.

1. Je! Inaingilika akilini serikali isitishe msako wa mtu anaetafutwa na taifa kubwa kama America na wanajeshi wake wakiwa wana operate ndani ya pakistan?
Kama sio mbinu za kuudanganya ulimwengu!
Kwa kuona kwamba kama utasem iliendelea kumtafuta! Ukimwengu ungejiuliza vipi miaka yote hiyo hajapatikana!?!

2.Unaweza kumwambia msomi yyt kuwa ilo kuepuka kunaswa na satelite za wamarekani basi we kavae kofia za cowboy mchezo umekwisha!

Teh teh teh teh!
Hapo nimeshindwa kuvumilia, imebidi nicheke!

Kama ni hivyo basi wale taleban tungewaona na makofia sio vilemba!

Na mengine mengi tu lkn muda haunifanyii hisani.

Until next time my friend Mkuu wa chuo
Nakutakia siku njema ndani ya bongoland.
hiyo namba 1 yamkini ndio maana walofanikisha hilo zoezi ni Wamarekani wenyewe bila ya hata intelligence ya Pakistan kujua kutokana na kikosi cha Seal team six wewe hapo huweki logic au hata ku reasoning?

hapo namba 2 mbona ni simple yamkini yeye ndio alikuwa anajidanganya akivaa cowboy basi satelite za wamarekani hazitamuona kumbe CIA wakawa wanafanya kazi zao...

All in all, hizo habari unaweza kuta labda ni maoni ya mwandishi au ya mtu lakini ukweli unabaki pale pale iliendeshwa operation ya kummaliza Osama na ikafanikiwa...

Uje ujaribu kupitia na mabandiko ya mkuu FUHRER unaweza ukajenga picha hapo zaidi...

okay my friend bwana kahtaan next time... uje na chujio uweze kuchuja na vilivyo chujwa tuvione...
 
Last edited by a moderator:
No easy day cha Mark Owen, nimekipitia, angalia lakini story za kina Rambo zipo nyingi.
Haijalishi stori za kina Rambo zipo nyingi, issue ni kwamba mission ilipigwa na ikafanikiwa...

wewe unadhani mission inge fail kungekuwa na story hizo unazosema kama za kina Rambo...

mission imefanikiwa ndio maana wanabidi waongeze na chumvi kama unavyosema...

kwa mfano sawa sawa na wewe umtandike mtu aliyekuwa anakusumbua unaweza ukaja kunisimulia ulifanikiwa kumpiga kwa pigo la Tai Chi kumbe hata hamna...

lakini bwana Ritz tukubali tu jamaa wako njema sana hakuna ubabaishaji...
 
Last edited by a moderator:
Bila kuwasahau kina willy gamba!
Na alibaba na wizi 40.
yeah ni kweli pamoja na yule jamaa aliyetoka Geita hadi Dar es salaam Magogoni kwa baiskeli mwaka 2010 kuja kumpa hongera mheshimiwa rais kwa kushinda urais...
 
yeah ni kweli pamoja na yule jamaa aliyetoka Geita hadi Dar es salaam Magogoni kwa baiskeli mwaka 2010 kuja kumpa hongera mheshimiwa rais kwa kushinda urais...
Mkuu wa chuo hapa umemaliza....jamaa zangu wanashindwa kukubali kwamba hakuna story telling iliyo 100% precise. Kuna distortions katika kila stage lakini bado haiondoi ukweli wa story yenyewe....
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wa chuo hapa umemaliza....jamaa zangu wanashindwa kukubali kwamba hakuna story telling iliyo 100% precise. Kuna distortions katika kila stage lakini bado haiondoi ukweli wa story yenyewe....
mkuu RealMan hawa jamaa bwana ni kwenda nao hivyo hivyo mdogo mdogo mwishowe anakimbia mmoja baada ya mwingine, sasa wenyewe wanabisha ukiwauliza ukweli mnaoujua ni upi wanabaki kuzunguka tu mara wanaanza kuhoji eti unaziamini kweli hizo source, ukiwaambia hebu leteni source zenu ambazo ni credible wanabaki kuzunguka tu

Lakini yote kwa yote story hiyo itabaki kuwa kweli kama unavyosema hata kama kuna distortions katika hypothesis Testing upande wa research haswa kwenye hesabu lazima kuwe na level of significance, vivyo hivyo na mambo kama haya...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wa chuo,

Wewe ndiyo umeandika kuwa kazikwa baharini mimi nimesoma mabandiko yako ndiyo maana nikajenga maswali wewe ndiyo umeyasema hayo.

Sasa unapoleta jambo ukumbini si lazima huwe na ushahidi nalo utapoulizwa maswali.

Mimi ninachojua baharini watu huwa hawazikwi.

Ni vizuri sasa wewe ukaja na story za ukweli kuhusu kifo cha Osama, tujifunze kutoka kwako.

Nani alitangaza kuwa Ayman Mohammed Rabie al-Zawahiri kachukuwa nafasi ya Osama?

CC. kahtaan,

wadau mnaweza kupitia haka kakipande hapa chini
Osama bin Laden ambaye alikuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda aliuliwa kwa kupigwa risasi ya jicho la kushoto baada ya kukataa kujisalimisha kwa majeshi ya Marekani.

Rais wa Marekani, Barack Obama pamoja na maafisa wake wa ulinzi na CIA walilifuatilia shambulizi la kumuua Osama bin Laden LIVE kupitia video zilizokuwa zikirekodiwa kwa kutumia video kamera zilizowekwa kwenye helmet za makomandoo wa Marekani walioivamia nyumba ya Osama.

Picha za tukio hilo zilizotolewa na televisheni ya ABC zilionyesha damu zikiwa zimetapakaa kwenye chumba ambacho Osama bin Laden alikuwemo.

Osama aliuliwa kwa kupigwa risasi kwenye jicho lake la kushoto. Maiti yake ilichukuliwa na kupelekwa kwenye kambi ya jeshi la Marekani nchini Afghanistan.

Baada ya vipimo vya DNA kuthibitisha kwa asilimia 99 kuwa mtu waliyemuua alikuwa ni Osama bin Laden baada ya kulinganishwa na vipimo vya DNA vya ndugu zake, maiti yake ilizikwa baharini baada ya Saudi Arabia na nchi zingine kuukataa mwili wake.

Helikopta moja kati ya nne za jeshi la Marekani zilizotumika kufanya mashambulizi toka angani, ilitunguliwa na roketi zilizorushwa na wapambe wa Osama bin Laden.

Nyumba aliyokuwa akiishi Osama ilikuwa takribani mita 200 toka kituo cha polisi na kilomita mbili toka kambi ya jeshi la Pakistan.

Taarifa ya Marekani ilisema kuwa maafisa wa Pakistan walikuwa hawajui kuwa Osama alikuwa amejificha kwenye jumba hilo lenye thamani ya dola milioni moja ambalo lilijengwa miaka mitano iliyopita likiwa na uzio mrefu wa kuta nene.

Wamarekani wameendelea kushangilia kuuliwa kwa Osama bin Laden ambaye alikuwa ndiye mtu aliyekuwa akitafutwa sana kuliko watu wote duniani.

Kiongozi wa Hamas katika ukanda wa Gazza, Ismail Haniyeh akiongelea kuuliwa kwa bin Laden alisema kuwa kuuliwa kwa bin Laden ni muendelezo wa umwagaji damu za Waarabu na waislamu unaofanywa na Marekani.

"Tunalaani kuuliwa kwa shujaa mtukufu wa Waarabu, Osama bin Laden na tunamuomba Mwenyezimungu amrehemu na kumweka mahali pema pamoja na waja wake wema", alisema kiongozi huyo wa Hamas.
 
Back
Top Bottom