Maisha ya Udalali: Kumzunguka dalali ni sawa?


Hapo ni sawa, bora umlipe kihalali kuliko kumlipa mtu ambaye kwanza kazi aliyofanya hailingani na malipo anayodai na halipi kodi popote. Binafsi siwezi mlipa dalali pesa ya mwezi mmoja, mpaka walete hiyo sheria.
 
Hio ndio inatakiwa yani, hawa madalali wanahisigi hela ni nyepesi sana. Yani nikupe laki 2 kwa kunionesha nyumba tu! Na labda usinikutanishe na mwenye nyumba maana nikikutana nae tu umeisha!
 
Kesi ya kuzungukwa hiyo ni kati yake na Mmiliki sio mimi Mteja, kama Mmiliki kakubali biashara bila Dalali wake basi wamalizane wao kwa wao.
 
Kuna baadhi ya business dalali yuko kihalali na ana sheria inayolinda kazi yake.

Mfano: Insurance Brokers (hawa ni madalali), kuna brokers wa shares/stocks (huwezi kuuza share zako bila kupita kwa hawa watu), kuna mawakala wa michezo (sports agents), kuna sales agents kama wa flights nk nk.

Tatizo la hawa wa nyumba na mazao ni kwa sababu nchi yetu haijaamua kurasimisha hizi biashara, ndiyo maana kuna janja janja nyingi sana. Wateja tunaona kama tunapigwa, na mifumo ya malipo haiko sawa, kwa sababu unapolipa miezi 12 ya kupanga nyumba, dalali alitakiwa achukue kule kwa aliyepokea hela na si kwa wewe uliyetoa, au kuwe na 50 50.
 
Hapo ni sawa, bora umlipe kihalali kuliko kumlipa mtu ambaye kwanza kazi aliyofanya hailingani na malipo anayodai na halipi kodi popote. Binafsi siwezi mlipa dalali pesa ya mwezi mmoja, mpaka walete hiyo sheria.
Saingine wanakupeleka kwenye nyumba ambazo hazikaliki unakuta ushampa hela na kodi umelipa usiku hulali! ila watasema nyumba nzuri haina shida 🤣🤣🤣
 
Kesi ya kuzungukwa hiyo ni kati yake na Mmiliki sio mimi Mteja, kama Mmiliki kakubali biashara bila Dalali wake basi wamalizane wao kwa wao.
Na hata hio ya kulipa mwezi mmoja kiutaratibu anatakiwa alipe mwenye nyumba. Amuachie dalali mwezi mmoja katika ile 6!
Ila ujanja unatumika kumtwisha mpangaji gunia la misumari.
 
Mimi baadhi ya shughuli zangu huwa nahitaji huduma ya Dalali...kuna wakati nasema ngoja nikaze nisiwatafute wale hela yangu bure...ila najikuta mambo yanasinzia naamua kuwatafuta na mambo wanafanikisha.

Ingawa nao wana nafasi yao ila kuna wakati wanakera.
 
Hahaaaaa, wale jamaa wanakera sanaaaa...
Anakufuata kuanzia nje, Unamwambia kabisa wewe usijisumbue kama unavyonisindikiza hivi nikifika nitapanda basi lako au nikupe chochote,
Anaitikia kabisa "wewe hunipi chochote watanipa kule" Cha kushangaza ukifika anaanza "ukinisaidia hata mia tano sio mbaya"... hapa ndio wanachefuaga,

Mimi sikuhizi nikienda stend natembea na ticket niliyokwisha itumia mkononi nimeining'iniza,
Hakuna anaye kufuata.
 
Ukutane na mwenye nyumba Mbea...
Unamfuata kimya kimya muyamalize..

Anamtonya dalalii..
"mtu wako yupo hapa anakuzunguka"...
Bongo kuna mambo yamekaa kikatuni katuni, ila ni watu ndio wanayafanya.
 
Na imagne vyenye ulivokuwa unaongea kwan ukali, nmebaki kucheka had mbavu znauma mweeeeeeh.
 
Dalali ni kazi Kama kazi zingine hata Mino Raiola ni dalali was CR7 ila tu kwa sababu tunatumia neno agent ndio maana anaheshimika.

Dalali azungukwi Wala madalali hatuzungukani "what goes around comes around around",ukimzunguka dalali atajua tu coz hiyo sehemu anayokupeleka ndio shamba lake huwa tunakusanya elf 20 ishurini za service charge kila siku ,siku nikileta mteja kwa hiyo chumba lazima mwny nyumba atanitonya bwana chumba kimechukuliwa na mteja X Mara paap nakukuta ndio unatoka chooni na kitaulo chako akiya Mungu naondoka na taulo nakuacha kama ulivyo.

Muhimu kuheshimu pale mwenzio anapopatia kipato ,usimdharau mtu sababu anafanya hyo job,just nimekutana na dalali wa magari ambaye ni dokta wa hospital kapiga vitu vyake MUHAS hapo akaanza kunitisha nikamwambia tulia mm mwnywe dalali wa nyumba ila mhandis alikuja kuniuzia gari.Kwa hiyo tuka merge now akipata wateja wa nyumba ananipasia na mm nikipata wa magari nampasia tunagawana asilimia kitu na box.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…