Maisha yamekuwa magumu sana awamu hii

Maisha yamekuwa magumu sana awamu hii

Kwa mtu ambaye yupo serikalini ukimwambia hali mbaya hawezi kukuelewa kwa kuwa pesa za mshahara wanapata kwa wakati..ila tulioajiriwa sekta binafsi,na amabao waliojiajiri wanaelewa hali ilivyo mtaani.

Ukweli ni kwamba pesa kwenye mzunguko imepungua sana biashara imekua ngumu mwaka jana mwezi wa tisa lilipita panga hapa kazini nashukuru hatukuguswa baadhi ya watu ila boss anaongea mpaka anatia huruma kwa sasa tunafanya kazi ili kulinda tu kazi lakini hakuna pesa (hatupati kwa wakati na kiduchu)

Sent using Jamii Forums mobile app
Na huyo mfanyakazi ambaye yuko serikalini na akawa hajui kuwa hali ni ngumu sana kupita kiasi basi nasema atakuwa hana akili na hapaswi kuwa mtumishi wa umma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siamini kuwa wanaolalamika kuwa maisha ni magumu wote walikuwa mafisadi.

Hembu tulete ushuhuda kama wewe
- Mfanyakazi
- Mkulima
- Muuza hoteli
- Muuza nguo
- Muuza genge Nk.

Tunaomba viongozi waweze kuchukua hatua hali mtaani ni worse.

Ushuhuda:
Nina kakibanda ulipaji wa kodi ni tabu mno kila siku wapangaji wanadai hawapati hela hivyo niwavumilie.
Hii hali imetengenezwa kwa makusudi,mkuu wa kaya anataka wote tuwe mafukara ili aturusherushe vichura vizuri
 
hali ni ileile tu hakuna kilichobadirika maana kama mfanya kazi mshahara anapata kama kawaida kinachobadirika hapo labda alikuwa mwizi au mla rushwa hao ndio wengi wanalalamika lakini sisi tuliozoea kula vya kuchinja vya kunyonga hatuviwezi yaani maisha tambarare tu kama kawaida
Tambarare iko wapi?uko wapi mzunguko wa pesa uliokuwepo awali?
Watanzania tuwe waelewa huu woga huu utatu cost
Hata serikali nayo ina suffer,hali ni mbaya sana biashara,kilimo,ajira hakuna....pesa hakuna...kila mtu analia nchi nzima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mtu ambaye yupo serikalini ukimwambia hali mbaya hawezi kukuelewa kwa kuwa pesa za mshahara wanapata kwa wakati..ila tulioajiriwa sekta binafsi,na amabao waliojiajiri wanaelewa hali ilivyo mtaani.

Ukweli ni kwamba pesa kwenye mzunguko imepungua sana biashara imekua ngumu mwaka jana mwezi wa tisa lilipita panga hapa kazini nashukuru hatukuguswa baadhi ya watu ila boss anaongea mpaka anatia huruma kwa sasa tunafanya kazi ili kulinda tu kazi lakini hakuna pesa (hatupati kwa wakati na kiduchu)

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuuuuuu usiseme serikalini wote wana pesa mwalimu anahali ngumu sana kama hujui
 
Changamoto kubwa kwa sasa inayokabili sector ya biashara ni KUSHUKA KWA PURCHASING POWER ya wateja.

Nguvu ya manunuzi kwa wateja imepungua sana compaired na zamani. Sasa hivi wateja wetu wanafanya manunuzi yale ya msingi tuu (bidhaa za chakula, elimu, pango la nyumba, nishati na matibabu).

Manunuzi ya ziada yamepungua sana, wateja wanabana matumizi kwenda sawa na hali ya uchumi wa nchi.

Mzunguko wa pesa ukiongezeka, purchasing power inaongezeka hence wafanyabiashara tunafanya biashara nzuri. Gharama za kukodi frame, maeneo, kodi za serikali, mishahara hazitakuwa mzigo kama purchasing power ya wateja wetu inaongezeka.

Na kwa sisi wafanyabiashara wateja wetu wengi ni watumishi wa serikali na sector binafsi. Mwaka wa 4 sasa hakuna ongezeko la mishahara, posho na marupurupu.

Sasa hivi wafanyabiashara wengi tunafanya biashara kwa uzoefu tuu ila ile kasi ya mzunguko wa biashara imepungua kwa sababu nilizozitaja hapo juu.

Sent using Cash Money Wings

Sent using Jamii Forums mobile app
Full stop..na hii ndo point kubwa

Pia hakuna ajira,kwahiyo hata idadi wa watu wenye uwezo wa kufanya manunuzi pia umepungua na kuongeza idadi ya vijana tegemezi
 
Rudia kusoma ulichoandika, kisha ruhusu akili yako iwaze kwa upana zaidi
Watanzania wengi wana fikra za kimasikini huwezi ukasema maisha mugumu kwenye nchi yenye soko la watu zaidi ya milioni 55 na ardhi ya kilimo ya kutosha tena yenye rutuba na upatikanaji wake ni rahisi. Tatizo watu wengi mnataka mpate pesa bila kujishughulisha. Watu hawataki kubadilika kutokana na wakati. Watu wanatoka Kenya kuja kulima miti ya mbao na parachichi Tanzania sisi tupo tu tunasema maisha magumu. Kwa sasa mnasema nyanya moja shilingi 500, kupanga ni kuchagua wewe uliwekeza kununua iPhone Mimi niliwekeza kwenye kilimo cha nyanya matokeo yake ndiyo hayo, hivyo hutakiwa kulalamikia bei ya nyanya nakusema maisha magumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasema tena hali ngumu kitaa anaebisha ni kichaa au mnufaika wa system maisha ni magumu sio mchezo ndio maana kumeongezeka kwa wimbi la vijana wa kike wanaojiuza baadaya ajira na kujiajiri hakueleweki kifupi fedha hamna kitaa
 
Nasema tena hali ngumu kitaa anaebisha ni kichaa au mnufaika wa system maisha ni magumu sio mchezo ndio maana kumeongezeka kwa wimbi la vijana wa kike wanaojiuza baadaya ajira na kujiajiri hakueleweki kifupi fedha hamna kitaa
True true true
 
Back
Top Bottom