witnessj
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 28,704
- 47,260
We jamaa huna roho mbaya, wachache sana wa kushea hivi[emoji848][emoji848]Okay mimi nilifanya hivi hapa sitatoa siri zote bwa shehe.
1.Eneo ambalo nimefungua maabara yangu imezingukwa na vitu vifuatavyo..
[emoji117]Gereji
[emoji117]Wafyatua matofali
[emoji117]Wachana mbao
Sasa niligundua wale wote hawana sehemu ya kula mpaka waagize stand ambapo ni kama mita 200 kutoka biashara zilipo na vyakula vyao ni low quality mno kwa bei kubwa.
Ninapofanya kazi ,wanapika ugali wa buku lakini wanajitahidi wanaweka dagaa,maharage,samaki na mboga za majani,wakati huo huo pale nilipofungua Lab ugali wanauza 1500 kwa mboga zile zile kwa low quality.
Nikafanya hivi Ugali nimeweka kwa buku jero ila nimeongeza tunda kwenye sahani naweka ndizi kipande au kipande cha nanasi(matunda nchakulia stirio au buguruni).Kwenye sahani najitahidi na nimewaambia wadada wanaonisaidia chakula lazima kiwe bora watie viungo vinavyohitajika na kwa ubora mkubwa hata kama faida itakua ndogo(mwanzoni target yangu ilikua ni biashara kwanza faida nilitegemea kupata kwenye vinywaji na si chakula)..hivyo mtu akinunua ugali wa buku jero anakutana na tunda hilo likawa bao la kwanza.
2.Wali nako nimejitahidi kuwaelesha uwe mzuri na wanapika vyema wanaweka njegere mara moja moja kwenye wali hivyo watu wanavutiwa kuja pale,,,
4.Usafi wa hali ya juu kuanzia mazingira hadi vyombo na lugha nzuri
5.Supu nauza buku lakini kwenye kila bakuli naweka na kiazi hivyo bakuli inapendeza na ni safi mno(natarajia kuweka kipande cha mkate huko mbeleni ila bado ndo nafikiria.
6.Wafanyakazi wawili ,huyu mmoja nimemtoa ninapofanya kazi baada kumona mchapa kazi na analipwa elfu 4 kwa siku nikamvuta kwangu kwa elfu 7. Na yule mwingine yeye makubaliano yetu awe msimamizi mkuu halafu tunalipana kutokana na kinachopatikana hivyo anafanya kazi kwa ubunifu mkubwa ukizingatia ni mtu wa dini sana na mpishi mzuri balaa.
Mahitaji yote sinunui rejareja
[emoji117]Mchele,unga,viazi ,mafuta nk nanunua jumla
[emoji117]Nyanya sterio nk
Natarajia kufanya haya
1.kununua mafriza makubwa mawili ili nianze kuweka na vinywaji
2.Kuweka na mtu wa chipsi auze kwa bei chee
Nk
Nb:Sio muandishi mzuri ila nina imani kwa uchache ndugu umeambulia kitu muhimu fanya kitu bora hata kama faida ndogo baada ya muda wateja wakizidi utapata kubwa.
God bless u[emoji120][emoji120]