Maisha yamekuwa magumu sana mtaani

Maisha yamekuwa magumu sana mtaani

Tuache utani jamani, hali ni mbaya sana huku mtaani.

Hela haipatikani, bei ya vitu inazidi kupanda, shambani nako vurugu mechi tupu. Kifupi hali ni tete na sio kwamba watu hatufanyi kazi kwa bidii la hasha.

Kwa hapa tulipofikia tunahitaji kufanya maamuzi magumu haki ya Mungu Wallah!!
 
maisha magumu lakini foleni za magari hazipungui, au magari yanatumia maji siku hizi?

Acha ujinga ww demu. Tanzania ina wananchi 55m, idadi ya magari haifiki 1.5m. au ukiona magari mengi yako sehemu ndogo unadhani nchi hii ina magari mengi hivyo? Nenda vijijini huko ukaone kulivyo na uhaba wa magari. Unakaa mahali kwa siku huoni magari zaidi ya matano. Na hiyo ni karibu asilimia 80 ya nchi nzima. Au unadhani Tanzania ni Dar pekee?
 
Mkuu watu wanafanya kazi kwa juhudi na maarifa ila purchasing power Ni ndogo mpaka watu mitaji inakata. Hapo inakuaje?
serikali imetoa fursa kwa kila mtu kufanyabiashara mahali popote bila vikwazo, ndio maana unaona ongezeko la machinga kila kona ya mji, mtaa, biashara zikiwa nyingi na mapato yanapungua,
 
Hali ngumu kwa mwanaume rijali hebu fikiria kwa wajane wanaouza mchicha huku wakiwa na hofu ya kukamatwa na kufilisiwa mchicha wao au walipe elfu 20

Wananchi huu ndio muda wa kutafakari na kuikataa ccm
 
Unafanya shughuli gani mkuu, upewe ushauri? Wakati mwingine jisemee nafsi yako tu. Acha na wengine wajisemee. Muda unaotumia kutype hayo maisha magumu kuna wengine wanaingiza pesa. Mfumo wetu wa elimu unazalisha wavivu wa kufikiri.
 
Tuache utani jamani,hali ni mbaya sana huku mtaani,hela haipatikani,bei ya vitu inazidi kupanda,shambani nako vurugu mechi tupu,kifupi hali ni tete na sio kwamba watu hatufanyi kazi kwa bidii la hasha.Kwa hapa tulipofikia tunahitaji kufanya maamuzi magumu haki ya Mungu Wallah!!

Ndio maisha tuliyoyachagua tunavuna tulichopanda tulitadharishwa atusikia,wenzetu Wakenya walistuka wakachagua fungu jema wangekosea kuchagua wangelimia meno.MTU yeyeto mwenye mawazo ya kijima ujamaa mnampa vipi leseni ya udereva? Kwenye ulimwengu wa Kisasa.
 
Tuache utani jamani,hali ni mbaya sana huku mtaani,hela haipatikani,bei ya vitu inazidi kupanda,shambani nako vurugu mechi tupu,kifupi hali ni tete na sio kwamba watu hatufanyi kazi kwa bidii la hasha.Kwa hapa tulipofikia tunahitaji kufanya maamuzi magumu haki ya Mungu Wallah!!
Pole sana, ukweli ni bado, mpaka wake zeru wavae kaniki!! 🤬 😡
 
Acha ujinga ww demu. Tanzania ina wananchi 55m, idadi ya magari haifiki 1.5m. au ukiona magari mengi yako sehemu ndogo unadhani nchi hii ina magari mengi hivyo? Nenda vijijini huko ukaone kulivyo na uhaba wa magari. Unakaa mahali kwa siku huoni magari zaidi ya matano. Na hiyo ni karibu asilimia 80 ya nchi nzima. Au unadhani Tanzania ni Dar pekee?
kwa hiyo dar hakuna maisha magumu ndio maana watu wanamiliki magar kwa wingi?
 
kwa hiyo dar hakuna maisha magumu ndio maana watu wanamiliki magar kwa wingi?
Bado hadi wote wapaki hizo Ist ndo tutaamini maisha ni magumu, Mzee azidi kukaba zaidi hata pa kukopana tukose
 
wakulima wa korosho wamelipwa pesa zao za mauzo, iliyopata hasara ni serikali kwa kukosa soko nje ya nchi sio mkulima

Utakuwa huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani, au kwakuwa vyombo vya habari vinatishwa visitangaze ukweli wa kinachoendelea, hivyo unadhani wakulima wote wamelipwa?
 
Back
Top Bottom