Maisha yamekuwa magumu sana mtaani

Maisha yamekuwa magumu sana mtaani

kwa hiyo dar hakuna maisha magumu ndio maana watu wanamiliki magar kwa wingi?

Dar Kuna mzunguko wa pesa wa asili. Hata kukiwa na ukame ndani ya nchi usidhani hata vyanzo vya maji vyote hukauka kabisa
 
Utakuwa huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani, au kwakuwa vyombo vya habari vinatishwa visitangaze ukweli wa kinachoendelea, hivyo unadhani wakulima wote wamelipwa?
Nimemwambia akaulize vizur aliempa data ,inawezekan wamechakachua data zake
 
Utakuwa huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani, au kwakuwa vyombo vya habari vinatishwa visitangaze ukweli wa kinachoendelea, hivyo unadhani wakulima wote wamelipwa?
zaidi ya asilimia 95 wamelipwa , naelewa kinachoendelea kihalisia sio huu uzushi wa mitandaoni, huku jf utasikia maisha magumu lakini mtaani maisha yanasonga kama kawaida! nina jamaa yangu ni shoe shiner hapa arusha lakin kwa siku hakosi elfu 30 !
 
serikali imetoa fursa kwa kila mtu kufanyabiashara mahali popote bila vikwazo, ndio maana unaona ongezeko la machinga kila kona ya mji, mtaa, biashara zikiwa nyingi na mapato yanapungua,

Ww utakuwa una ujinga wa kipaji, unapima ubora wa maisha kwa kuangalia kiwango cha machinga hapa mjini? Hao wamachinga wanafanya hiyo kazi kwa kuwa wamekosa ajira rasmi, usishangae kukuta hao wamachinga wanakaa chumba kimoja zaidi ya watu watatu kama wako lockup. Watu wa aina hiyo unaweza kusema ndio kipimo cha ubora wa maisha?
 
Ukilalamika maisha magumu yeye ndio anafurahi kwamba anakomesha...sio kila mtu hupenda watu kuishi kwa furaha na neema wengine hutaka yeye ajitanue were uteseke tungeweza kubadili lkn wananchi imezorota kama ccm stars inayoonewa na kilamtu
 
Ww utakuwa una ujinga wa kipaji, unapima ubora wa maisha kwa kuangalia kiwango cha machinga hapa mjini? Hao wamachinga wanafanya hiyo kazi kwa kuwa wamekosa ajira rasmi, usishangae kukuta hao wamachinga wanakaa chumba kimoja zaidi ya watu watatu kama wako lockup. Watu wa aina hiyo unaweza kusema ndio kipimo cha ubora wa maisha?
kuna machinga wana maisha mazuri kuliko wafanyakazi wa benki, hapa arusha wauza mchicha, nyanya karibia wote wamejenga nyumba. kuna watembeza uji, chai kwa siku wanaingiza zaidi ya elfu 50,
 
zaidi ya asilimia 95 wamelipwa , naelewa kinachoendelea kihalisia sio huu uzushi wa mitandaoni, huku jf utasikia maisha magumu lakini mtaani maisha yanasonga kama kawaida! nina jamaa yangu ni shoe shiner hapa arusha lakin kwa siku hakosi elfu 30 !

Show shiner hapo Arusha hakosi 30 elfu@day? Fuatilia vizuri, ni maeneo mangapi kwa wastani show shiner hapo Arusha wanalaza kiasi hicho? Kama ni hivyo watu si wangeacha biashara ya hiace wanaosumbuliwa na TRA na traficc waje wawe show shiners? Hao shoe shiners wengi wanauza bangi, hicho kijiwe ni cha kuzugia tu.
 
kuna machinga wana maisha mazuri kuliko wafanyakazi wa benki, hapa arusha wauza mchicha, nyanya karibia wote wamejenga nyumba. kuna watembeza uji, chai kwa siku wanaingiza zaidi ya elfu 50,

Narudia tena hujui usemalo zaidi ya kufurahisha genge, machinga awe na maisha mazuri kuliko mfanyakazi wa bank? Kwa wastani wafanyakazi wengi wa bank wengi wanapata zaidi ya laki 6@month. Machinga wangapi wanapata zaidi ya laki sita kwa mwezi hapo Arusha? Ni kweli hao machinga wamejenga ila sio nyumba bali ni room za kulala.
 
Show shiner hapo Arusha hakosi 30 elfu@day? Fuatilia vizuri, ni maeneo mangapi kwa wastani show shiner hapo Arusha wanalaza kiasi hicho? Kama ni hivyo watu si wangeacha biashara ya hiace wanaosumbuliwa na TRA na traficc waje wawe show shiners? Hao shoe shiners wengi wanauza bangi, hicho kijiwe ni cha kuzugia tu.
biashara inahitaji ubunifu, uaminifu, hata utembeze matunda mtaani ukiwa mwaminifu, mbunifu unatoboa! kuna wauza matunda yaliyokatwa katwa kwa siku hawakosi elfu 50, acha kushinda jf ingia mtaan uone machinga wanavyopiga pesa!
 
Dar Kuna mzunguko wa pesa wa asili. Hata kukiwa na ukame ndani ya nchi usidhani hata vyanzo vya maji vyote hukauka kabisa
Sio kweli Sasa hivi mzunguko wa pesa dar Ni mdogo sababu wafanyakazi wengi wa serikali Wamehamia Dodoma .Sinza waliyokuwa vigogo wanapangishia nyumba nzima na kulipa Kodi ya mwaka mzima kwa Bei mabaya kwa ajili kuwapangishia hawara zao kujificha wasionekane guest au hotel Sasa hivi nyumba hazina wapangaji wa pesa nyingi mabaa medi,wachoma nyama choma na akina mama nitilie ndio wanapanga tena chumba kimoja kimoja kwa bei poa.ukijitia mwenye nyumba unataka mpangaji wa nyumba nzima na Kodi ya mwaka mzima nyumba yako watalala mijusi na panya hupati mpangaji
 
Wakulima wa pamba kanda ya ziwa bado hakijaeleweka vizuri wamuuzie nani, hawana wanunuzi.
 
Sio kweli Sasa hivi mzunguko wa pesa dar Ni mdogo sababu wafanyakazi wengi wa serikali Wamehamia Dodoma .Sinza waliyokuwa vigogo wanapangishia nyumba nzima hawara zao kujificha wasionekane guest au hotel Sasa hivi nyumba hazina wapangaji wa pesa nyingi mabaa medi,wachoma nyama choma na akina mama nitilie ndio wanapanga tena chumba kimoja kimoja kwa bei poa.ukijitia mwenye nyumba unataka mpangaji wa nyumba nzima na Kodi ya mwaka mzima nyumba yako watalala mijusi na panya hupati mpangaji

Muambie huyo kiazi anayesema magari yamesongamana hapo Dar.
 
Narudia tena hujui usemalo zaidi ya kufurahisha genge, machinga awe na maisha mazuri kuliko mfanyakazi wa bank? Kwa wastani wafanyakazi wengi wa bank wengi wanapata zaidi ya laki 6@month. Machinga wangapi wanapata zaidi ya laki sita kwa mwezi hapo Arusha? Ni kweli hao machinga wamejenga ila sio nyumba bali ni room za kulala.
laki 6 kwa mwezi hata wauza michicha wanaipata, nimetembelea vicoba vingi kuna watu wanachangishana elfu 10 kila siku na wengi ni mama ntilie, wauza samaki za kukaanga mtaani, mchicha na wanauwezo wa kuchanga na bado matumizi yake ya nyumbani, hapo wanaingiza zaidi ya elfu 20 kwa siku, wapiga debe tu wa stand hawakosi elfu 10 kwa siku
 
biashara inahitaji ubunifu, uaminifu, hata utembeze matunda mtaani ukiwa mwaminifu, mbunifu unatoboa! kuna wauza matunda yaliyokatwa katwa kwa siku hawakosi elfu 50, acha kushinda jf ingia mtaan uone machinga wanavyopiga pesa!

Hivi unadhani unaniambia kitu kipya ambacho sikijui wala kukifanyia utafiti? Hao wazungusha matunda waulize wakupe siri ya urembo, wako wengi wakifukuzia wateja wachache wenye uthubutu wa kununua matunda. Walio wengi huku mijini wanakula chakula kisichozidi shilingi 2,000 tena kwenye vijicontainer vya plastiki, huo ubavu wa kula matunda wautoe wapi? Na bado hao wazungusha matunda wanakutana na usumbufu mkubwa wakati wa kudai kila wakipita mara nipitie baadae, mara kesho. Hujui unaloongea bosi zaidi ya kupiga faida za kwenye karatasi.
 
Sio kweli Sasa hivi mzunguko wa pesa dar Ni mdogo sababu wafanyakazi wengi wa serikali Wamehamia Dodoma .Sinza waliyokuwa vigogo wanapangishia nyumba nzima na kulipa Kodi ya mwaka mzima kwa Bei mabaya kwa ajili kuwapangishia hawara zao kujificha wasionekane guest au hotel Sasa hivi nyumba hazina wapangaji wa pesa nyingi mabaa medi,wachoma nyama choma na akina mama nitilie ndio wanapanga tena chumba kimoja kimoja kwa bei poa.ukijitia mwenye nyumba unataka mpangaji wa nyumba nzima na Kodi ya mwaka mzima nyumba yako watalala mijusi na panya hupati mpangaji
hata wafanyakazi wote wa serikali wakihama dar hawawezi kupunguza mzunguko wa pesa, hao watumishi hata elfu 20 hawafiki wakati dar kuna watu milioni 6, hao wafanyakaz hawana impact yoyote kwa uchumi wa dar, dar jiji la wafanyabiashara
 
Back
Top Bottom