Maisha yamekuwa magumu sana siku hizi

Maisha yamekuwa magumu sana siku hizi

APPROXIMATELY

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2021
Posts
2,035
Reaction score
2,715
Kusema la kweli hali mtaani imekuwa hatari, nimeshuhudia biashara nyingi zinafungwa, kuna mshikaji wangu alikuwa na office ya uwakala mitandao ya simu, kafilisika kabisa kafunga banda lake miezi 3 inaisha sasa, mpaka majani yameota, niliwekeza kwenye baadhi ya biashara kwa mfano nilifungua office 3 za library ya cd,mapato kwa siku yalikuwa kwanzia 25000-40000, ila sasa kupata 15000 ni kwa tabu mnoo.

Jiji limezidi kuwa gumu na fikria nifunge office zote Dar nikatafute chaka lingine bush, kuna machaka kibao Tanzania sijui kwanini mpaka sasa na ng'ang'ania Dar, ni swali ambalo naliwaza sipati usingizi kabisa, nimeingiwa naroho ya kuichukia bongo kinoma noma. Nafikria niwekeze kwenye kilimo kila nikifikiria hali ilivyo kwenye kilimo nakata tamaa, nimeona nibakiwe na office zAngu zilizopo Arusha tu.

Jamani wenzangu hali ni ngumu kwangu tu au pia kwenu ni tete kama mimi? Biashara za mikoani zipo fresh ila tatizo bongo hii ishakuwa bongo nyoso, eti wanasema mama anaupiga mwingi, au hIzi tozo mama ndio anaupiga mwingi? au hizo vita za wazungu zinafanya uchumi kubadilika?

Sijawahi kulizika na maisha na itaka itokee hata siku moja kwa maisha ninaotamani kuwa nayo nikifikisha 40, nimekuwa mfano kwenye ukoo wetu na hata kijiji nilipotoka huwa wananiona bonge la genius kinyama kwenye kusaka ela ila hii hali inanitisha sana ni hayo tu ndugu zangu nimejaribu kusema yote yaliyopo moyoni mwangu.

Kama kuna nilichokiandika kitamkwanza yeyote humu nisameheni, nimejaribu kuandika jinsi nilivyo maana mimi ndo nilivyooo ndoo hayo tuuu
 
NI kweli mkuu I feel your pain...ila NI suala la muda TU wakati mwingine angalia msimu upo wapi unaweza kujichanganya kwenye ishu nyingi...

Hela kila mtu anaitaka na hata ikikutoka itakurudia TU.wote tunatumia inapokuwa mavuno hela nyingi inapelekwa shamba mikoani ila nusu inarudi dar ila inafikia wafanyabiashara wakubwa kwanza then mdogomdgo inaanza kuingia mitaani kingine bajeti kuu inaanza utekelezwaji matumizi muda sio mrefu yataongezeka usikate tamaa...

Hint:
Spend less af save

Acha kbs matumizi yasiyo na Tija...

Kumbuka Kuna kipindi Cha kulia na kipindi Cha kucheka...Cha kuzaliwa na cha kufa.
 
Toka nazaliwa huko karne ya 20 aka ka phrases nimekua nikikasikia " maisha yamekua magumu sana siku hizi"

Iyo siku hizi hainaga mwisho
Duniani nzima Jinsi siku zinavyozid kwenda hela zinazidi kuwaponyoka maskini zinakwenda kwa matajiri wakubwa WACHACHE na wao kuzitoa mpk zije zirudi Huku chini ni ngumu.. mfano assume TU bill gate tunamchangia Bei gani je yeye mpka aje afanye kununua bidhaa kwetu ili hio pesa iturudie NI lini..simple TU km hivo
 
Yaan kulialia kote huko kumbe una office sijui ni tatu na Arusha pia una ofisi wewe sema mapato yameshuka maana inawezekana ulikuwa unalaza Million per day sasa unalaza let say 300k ndo unakuja kwa kishindo humu kulialia,,kumbuka kuna graduate kamaliza Md ana mwaka wa 4 sasa Hana ramani! Kikubwa tu mshukuru Mungu kwa yote
 
Kila mtu Ana anglia upande wake jombiii,alafu mimi ni wa kiume man,ndo maana nilisema mwishoni sijawahi kulizika,tatizo wewe hujui nina ndugu ambao wanauwezo kinoma ishu inakuja mwenzi wa kumi na 12 Christmas,nataka nami niwavimbie
 
Jinsi siku zinavyozid kwenda hela zinazidi kuwaponyoka maskini zinakwenda kwa matajiri wakubwa WACHACHE
Kuna Jamaa aliwahi kuniambia:

Ujanja ni kua na Akili ya utafutaji nje ya mfumo

Yaan mfumo wa Tajiri kuchukua kwa Masikini na kujilimbikizia yeye tu anatajirika yeye tu na sio vinginevyo

Lakini nilipomuhoji huo mfumo unaendaje endaje yaan unaanzaje anzaje kuwapora Masikini huku wao wanakuchekea tu?

Hadi leo hajawahi kunipa jibu
 
Idea kama hizi zinahitajika sana,binadamu hawezi kukupa siriya utajiri wake
 
Mi nilipoona Bi Mkubwa alipoingia tu , kaanza kwa kupandisha gharama za bundle , Nikaona basi huyu sera zake sio nzuri , nikahama Dar na ku-change biashara

Hatimae nilichokitabiria kimekamilika , vijana walokua wanapiga pesa online wamekufa kifudifudi
 
Wakati wewe unasema maisha magumu
Kuna watu wananunua magari mapya
Wanafungua makampuni makubwa
Wanaagiza magari nje
Tuendelee kupiga kazi hakuna ugumu ila kuna fursa hakuna kufeli ila kuna kujifunzab
Tupige kazi tu wakuuu
Atleast umeandika kitu nice
 
Mi nilipoona Bi Mkubwa alipoingia tu , kaanza kwa kupandisha gharama za bundle , Nikaona basi huyu sera zake sio nzuri , nikahama Dar na ku-change biashara

Hatimae nilichokitabiria kimekamilika , vijana walokua wanapiga pesa online wamekufa kifudifudi
Uliona mbali mkuu
Mfumo wa kuwanyooonya Masikini na kujitajirisha wewe mwenyewe

Namaanisha mfumo wa kuchukua kwa masikini na kujilimbikizia wewe mwenyewe alimaarufu km Ubepari

Mkuu haujaelewa nini hapo kwani?
Kununua mashamba yao,na vitu walivyonavyo na kuwacha masikini
 
Kununua mashamba yao,na vitu walivyonavyo na kuwacha masikini
Ndio sasa kwa huo huo mfano wa kuchukua mashamba yao na vitu walivyonavyo kaa chini kwa mfumo huo huo fikiria tuliza Akili alafu fanya ujitafutie nje ya huo mfumo sio ndani ya mfumo unapiga pesa mingi au bado haujaelewa hapo?
 
Back
Top Bottom