Maisha Yamenifundisha Jambo Moja: Usisubiri Mtu Akuokoe

Status
Not open for further replies.
Ni kweli, hakuna anayefanikiwa peke yake. Kujitegemea hakumaanishi kuwadharau watu, bali kutokuweka maisha yako kwenye huruma yao. Wateja, washirika na jamii ni sehemu ya mafanikio, lakini tofauti ni kutegemea thamani unayotoa, si kuishi ukisubiri kuhurumiwa.
Amina
 
Right people are coming to help you. Your customers might come and help you. In life everything is there because of people, kama unachokifanya sio hitaji la binadamu mwingine basi hiyo ni hobby.

Stay smart 😎, find right people.
Nakubaliana. Watu ni sehemu muhimu ya mafanikio. Lakini pia watu wanakuja pale unapojenga thamani, uaminifu na suluhisho, si kwa sababu wanakuonea huruma. Tafuta watu sahihi, lakini usiweke maisha yako kwenye kutegemea huruma yao. Hapo ndipo tofauti ilipo.
 
Hahaha mtoa mada ndicho alicho reflect kwenye andiko lake. Sisi wasomi wa btn the lines hatuishii Tu kwenye kile ulichoandika Bali kile ulichojaribu kuficha
Kusoma between the lines ni vizuri, lakini si kila tafsiri huwa ndiyo dhamira ya mwandishi. Tofautisha unachokisoma na unachokidhania. Hoja ijadiliwe kwa ushahidi wa kilichoandikwa, si kwa hisia za msomaji.
 
Huyo Mleta Uzi amepigwa na kitu kizito na heading yake ni ya mtu aliyekata tamaa
Inawezekana ukawa umeitafsiri hivyo, lakini si kila mtu anayeandika kuhusu kujitegemea huwa amekata tamaa. Wakati mwingine ni somo alilojifunza kutokana na uzoefu wa maisha. Tujadili hoja, tusihukumu hali ya mwandishi bila ushahidi.
 
Yaah usisubiri msaada, mi niliingizwa mkenge labisa nikidhani nilipo ndio tobo kumbe ndo shimo, uzuri sikukaa sana nikatembea.

Ukiweza kujisimamia mwenyewe, jitahidi usirudishe mpira kwa kipa, komaa. Waja wana nongwa sana.
 
Kipindi nipo Arusha, Kuna jamaa zangu hali ilikua poa walikua wana piga pesa balaa, yani hela ilikua inaingia ya kutosha mshikaji alikua meneja wetu, akawa ananunua simu Kali na za gharama, vitu vya ndani vya gharama, pombe na mademu yani ukija kuomba kazi akagundua we ni mzuri lazima akugonge, mpaka boss wetu wa kike jamaa kamla, nilikua nimekaa na mshikaji wangu tunamjadili hizo pesa Kwa Nini mshikaji asifungue miradi kwanza akisha kua na uhakika we pesa aanze fujo sasa, kununua vitu vya ndani nk.

Nilipo ondoka baadae miaka imesepa napata taarifa ile ofisi Isha fungwa mwana ana pitia wakati mgumu kinoma. Asee UKIPATA chance kidogo tu make it mzeer usifanye kosa piga hela wekeza achana na mambo ya hasara we Fanya muachie mungu
 
Kuna kipindi nilikuwa naamini ipo siku mtu atakuja abadilishe maisha yangu. Nilisubiri nafasi, nilisubiri bahati, nilisubiri msaada.

Lakini kadiri miaka ilivyopita, nikagundua kuwa muda ndio ulikuwa unapita, si matatizo.

Maisha hayana huruma kwa anayesubiri sana. Yanamheshimu anayechukua hatua, hata kama hatua yake ni ndogo.

Nimejifunza kwamba unaweza kuwa na ndoto kubwa, lakini bila nidhamu na juhudi zitabaki kuwa ndoto tu. Unaweza kuwa na marafiki wengi, lakini siku ya shida ukabaki peke yako. Unaweza kulaumiwa na watu leo, halafu kesho haohao wakakupigia makofi ukifanikiwa.

Usikubali hali uliyonayo leo ikuambie wewe ni nani. Hali ni ya muda, lakini maamuzi yako ndiyo yanayojenga kesho yako.

Ukikosa kazi, jifunze ujuzi. Ukikosa mtaji, jenga maarifa. Ukikosa anayekuamini, anza kwa kujiamini wewe mwenyewe.

Naomba kila anayesoma uzi huu ajibu swali moja:

Ni somo gani gumu zaidi ambalo maisha yamekufundisha, na lilibadilishaje mtazamo wako?
Tupeane uzoefu.

Huenda simulizi yako ikawa mwanga kwa mtu anayepitia kipindi kigumu leo. 🙏🙏🙏
Kuwa YATIMA aise nilipitia maisha ya magumu mno,Mungu kwanza,nidhamu,na juhudi binafsi, mwisho maisha ni Yako,walasiyo ya Baba Wala Mama Yako wala ndugu zako.
 
Right people are coming to help you. Your customers might come and help you. In life everything is there because of people, kama unachokifanya sio hitaji la binadamu mwingine basi hiyo ni hobby.

Stay smart 😎, find right people.
Huwa na tamani sana na kumuomba Mungu mimi ndie sababu ya mtu kuinuka, mimi niwe msaada kwa mtu mmoja ambae daima atamshukuru Mungu kwa sababu yangu.
 
Kipindi nipo Arusha, Kuna jamaa zangu hali ilikua poa walikua wana piga pesa balaa, yani hela ilikua inaingia ya kutosha mshikaji alikua meneja wetu, akawa ananunua simu Kali na za gharama, vitu vya ndani vya gharama, pombe na mademu yani ukija kuomba kazi akagundua we ni mzuri lazima akugonge, mpaka boss wetu wa kike jamaa kamla, nilikua nimekaa na mshikaji wangu tunamjadili hizo pesa Kwa Nini mshikaji asifungue miradi kwanza akisha kua na uhakika we pesa aanze fujo sasa, kununua vitu vya ndani nk.

Nilipo ondoka baadae moska imesepa napata taarifa ile ofisi Isha fungwa mwana ana pitia wakati mgumu kinoma. Asee UKIPATA chance kidogo tu make it mzeer usifanye kosa piga hela wekeza achana na mambo ya hasara we Fanya muachie mungu
Kwa mishahara aliyokuwa anawalipa , wewe na wenzako mliwekeza wapi na maendeleo ya uwekezaji wenu ni yapi?
 
Kuwa YATIMA aise nilipitia maisha ya magumu mno,Mungu kwanza,nidhamu,na juhudi binafsi, mwisho maisha ni Yako,walasiyo ya Baba Wala Mama Yako wala ndugu zako.
Heshima kwako. Kupitia maisha magumu ukiwa yatima si jambo dogo. Uzoefu wako unaonyesha kwamba imani, nidhamu na juhudi binafsi vina nafasi kubwa. Mwishowe kila mmoja anawajibika kujenga maisha yake mwenyewe.

Pole Sana Pya...
 
Nimejifunza samtiimu tusitegemee sana mwanamke atupe uroda ni kukwea mnazi ndio njia sahihi wanawake sio watu kabisa tupige puchu wanangu
Asante mleta uzi
 
Huwa na tamani sana na kumuomba Mungu mimi ndie sababu ya mtu kuinuka, mimi niwe msaada kwa mtu mmoja ambae daima atamshukuru Mungu kwa sababu yangu.

Ni kupambana tu boss. Maana kila unapojijengea thamani unakuwa tegemeo la watu wengine. Kazi/shughuli unayoifanya Incase ipo kwaajili ya kusaidia watu kutatua changamoto zao, kuwafanyia maisha yawe rahisi, kuwapa huduma fulani basi wewe ni msaada kwa watu.
 
Nimejifunza samtiimu tusitegemee sana mwanamke atupe uroda ni kukwea mnazi ndio njia sahihi wanawake sio watu kabisa tupige puchu wanangu
Asante mleta uzi
😂😂 Kila mtu ajifunze kujitegemea, lakini tusiwalaumu wanawake kwa maamuzi yetu. Uhusiano ni uchaguzi, si lazima. Jikite kwenye malengo yako, mengine yatakuja kwa wakati wake.
 
Kuna kipindi nilikuwa naamini ipo siku mtu atakuja abadilishe maisha yangu. Nilisubiri nafasi, nilisubiri bahati, nilisubiri msaada.

Lakini kadiri miaka ilivyopita, nikagundua kuwa muda ndio ulikuwa unapita, si matatizo.

Maisha hayana huruma kwa anayesubiri sana. Yanamheshimu anayechukua hatua, hata kama hatua yake ni ndogo.

Nimejifunza kwamba unaweza kuwa na ndoto kubwa, lakini bila nidhamu na juhudi zitabaki kuwa ndoto tu. Unaweza kuwa na marafiki wengi, lakini siku ya shida ukabaki peke yako. Unaweza kulaumiwa na watu leo, halafu kesho haohao wakakupigia makofi ukifanikiwa.

Usikubali hali uliyonayo leo ikuambie wewe ni nani. Hali ni ya muda, lakini maamuzi yako ndiyo yanayojenga kesho yako.

Ukikosa kazi, jifunze ujuzi. Ukikosa mtaji, jenga maarifa. Ukikosa anayekuamini, anza kwa kujiamini wewe mwenyewe.

Naomba kila anayesoma uzi huu ajibu swali moja:

Ni somo gani gumu zaidi ambalo maisha yamekufundisha, na lilibadilishaje mtazamo wako?
Tupeane uzoefu.

Huenda simulizi yako ikawa mwanga kwa mtu anayepitia kipindi kigumu leo. 🙏🙏🙏
Kichwa chako ndio serikali Yako,chukua maamuzi!
 
Kwa mishahara aliyokuwa anawalipa , wewe na wenzako mliwekeza wapi na maendeleo ya uwekezaji wenu ni yapi?
Sisi tuliKua tunalipwa efu mbili Kwa siku mara elfu Moja sio ZAMAN miaka hii, na Kuna muda hata hiyo efu moja usipate, ACHA TU bro maisha ni tofauti na unavo Dhani,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom