Kuna kipindi nilikuwa naamini ipo siku mtu atakuja abadilishe maisha yangu. Nilisubiri nafasi, nilisubiri bahati, nilisubiri msaada.
Lakini kadiri miaka ilivyopita, nikagundua kuwa muda ndio ulikuwa unapita, si matatizo.
Maisha hayana huruma kwa anayesubiri sana. Yanamheshimu anayechukua hatua, hata kama hatua yake ni ndogo.
Nimejifunza kwamba unaweza kuwa na ndoto kubwa, lakini bila nidhamu na juhudi zitabaki kuwa ndoto tu. Unaweza kuwa na marafiki wengi, lakini siku ya shida ukabaki peke yako. Unaweza kulaumiwa na watu leo, halafu kesho haohao wakakupigia makofi ukifanikiwa.
Usikubali hali uliyonayo leo ikuambie wewe ni nani. Hali ni ya muda, lakini maamuzi yako ndiyo yanayojenga kesho yako.
Ukikosa kazi, jifunze ujuzi. Ukikosa mtaji, jenga maarifa. Ukikosa anayekuamini, anza kwa kujiamini wewe mwenyewe.
Naomba kila anayesoma uzi huu ajibu swali moja:
Ni somo gani gumu zaidi ambalo maisha yamekufundisha, na lilibadilishaje mtazamo wako?
Tupeane uzoefu.
Huenda simulizi yako ikawa mwanga kwa mtu anayepitia kipindi kigumu leo. 🙏🙏🙏