Maisha Yamenifundisha Jambo Moja: Usisubiri Mtu Akuokoe

Status
Not open for further replies.
Niliaminigi demu nilie kua naye ndo mzuri kuliko wote akawa ananiendesha, nilipo Anza kutembea mikoa tofauti nika gundua achana kujijwngea Imani ka hizo ukisha Jenga kua huyu ni mzuri inakua hivo cha kushangaza nimekutana na wazuri wengi sana kiasi yule mwanzo simtaki tena, sitakiiiiiiii simtakiiiiiii MUNGU ana visu mzeeer, kibaooooooo babakeeeee
 
😂😂 Pole mkuu, ila usiseme "ndiye wa mwisho" mapema. Maisha yana sura nyingi, tulia tu usije ukarudi kusema, "huyu naye alikuwa somo." 😄
 
😂😂 Pole mkuu, ila usiseme "ndiye wa mwisho" mapema. Maisha yana sura nyingi, tulia tu usije ukarudi kusema, "huyu naye alikuwa somo." 😄
Hapana kaka labda huja ni nyaka vizuri, mwisho wa mapambano Huwa ni pale unapo kata roho, maana yangu ni kua usitishwe, usi nyanyaswe kisa demu kama ni mademu wakali MUNGU anao wengi, usikubali kua yeye ndo the best akikuona wa Nini we muone wa kazi gani, kitu na box
 
Wengi ambao unaweza ukawa unawategemea, ni watu wabinafsi, wanakuchekea kumbe wao ndio anguko lako.
 
Usisahau Kuna wenye bahati pia
 
Aliyeandika huu ujumbe tutenge siku yake maalum katika mwaka huenda vijana wetu wa hovyo wakaamka
 
Zaidi ya hapo mkuu, kuna ile kugusa moja kwa moja maisha ya mtu.

Ni kupe mfano, kuna mzee mmoja alienda kumsalimi mwanae dar es laam.

Wakati yule mzee anarudi yule mwanae akamuulizia bibi fulani yupo?
Alimpa shilingi 5,000 amletee yule bibi kama zawadi kulingana na mahusiano yao huyo bibi na mtoto yule mzee

Huyo bibi aliwahi kufanyia kitu udogoni huyo dada kwa hio hakuwahi kusamsahau.

Yule mzee alipo fika moshi hakulala na ile hela, wakati huo mimi nilikua darasa la nne nakuliia na mtihani nadhani ni wa ngazi ya mkoa , kuna malipo sikua nimelipa nadhani ni ada ya umitashumta kam sijakosea , ile 5,000 bibi akanipa nikalipe deni shuleni,na nika fanikiwa kufanya mtihani.

Sasa unadhani yule dada wa dar aligusa maisha yangu kwa kiasi gani.

Zaidi ya miaka 25 sasa sijawahi kumsahau japo sikuwahi kumjua kwa sura ila walifahamiana na bibi yangu

Ndio hicho ninachotamani kufanya mimi, kumgusa mtu moja kwa moja.
 

Very interesting, maisha ya binadamu yamekuwa ya kusaidiana na umoja. Ukiona unajitenga na jamii kuna kitu hujakielewa kuhusu haya maisha.

Kuna wakati pia, nilikuwa busy sio mtu wa kuongea na watu sana. Kuna siku jirani yangu akaja kwangu alikuwa amebeba mfuko sikufahamu Kuna nini. Baadae alipo nikabidhi akaniambia alitoka safarini kuna machungwa alitenga kwaajili ya jirani yake. Kwa kweli nilishindwa Cha kusema ni kitu kidogo lakini niliona thamani yake ni kubwa sana, hiyo situation imeweza kuleta heshima na maelewano mazuri zaidi. Kila nikimuona kumbukumbu ya kwanza ni siku alipokuja na zawadi hiyo.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…