Maisha yangu baada ya miaka 37!

Nenda Instagram kamtafute joelnanauka anafundisha sana namna ya watu kujikomboa kiuchumi...na wengi kupitia mafundisho yake wamejikomboa na madeni pia wamesimama kiuchumi hata kama awali walianguka.....Mimi binafsi tumejiari na tunapata pesa kidogo tu lakini life linasonga..yaani haya maisha ni kuwa na nidhamu ya pesa...ukiwa huna mipango ya kuitumia pesa basi pesa yenyewe ndiyo itakupangia matumizi kwa sababu wewe huipangii matumizi...

Ushauri wa awali ni huu...fungua account, ukipata hata kidogo tupia huko...jipe muda..utakuta umenunua kiwanja na hata kujenga....jiwekee malengo lazima utayatimiza tu...lakini usiache kusali na pia acha pombe na kufuja pesa....

Nidhamu ya pesa ni muhimu.
 
Asante sana. Yaani pamoja na kupokea pesa kila mwisho wa mwezi suala la mahitaji ya nyumbani limekua topic. Lazima nidhibiti hali hii
 
Aise asante! Ila mirija sifungi
 
Labda. Hii ID niliiandika tu baada ya kusoma riwaya moja iliyoandikwa na mwandishi wa KENYA inaitwa KUFA KUZIKANA. Ni riwaya tamu sana hivyo kwa ajili ya mapenzi nikatumi hilo jina.
 
Nita
Nitafuatilia hiyo account ya IG. Asante kwa ushauri
 
Tangu nianze kazi sijui pesa zangu zinapoenda. Sina kiwanja Sina akiba. Bado nimepanga Kodi laki tatu kwa mwezi.
Kosa lilianzia hapa.
Na sio wewe tu wapo vijana wengi.

Ishi nyumba ya kawaida huku ukijiandaa kujenga yako.

Usijali marafiki zako wanasemaje.
Jifunze kwa wahindi wanarundikana familia na ukoo mzima kwenye magofu huku wakitengeneza mitaji ya biashara inayowapa uyajiri baadae
 
Tazizo hizo starehe unazifanya kwa nidhamu???

Ninaye rafiki yangu akinywa akifika chupa ya tano anatoa simu yake kuita washkaji zake hovyo kuna siku aliita watu tisa (9 people just imagine wanakunywa na kula kwa hela zake) sikuweza kuvumilia nikaaga nikaondoka na toka siku hiyo kampan yake sikuitamani tena.

Na mpaka sasa na yeye anaishi kwenye nyumba ya kupanga Tegeta huku mwanae aged 5½ kampeleka shule ada 2.5 mill na baadhi ya anaowanunulia pombe wanaishi kwenye nyumba zao,starehe bila nidhamu ni laana mleta mada shida ipo hapo kwenye pombe hakuna kingine.
 
Pombe kama huna hela ya Walamba asali umekwisha.

Watu wana mbinu nyingi ya kupata pesa. Ukiwa wewe ni mvuja jasho starehe ya pombe unatakiwa ujicontrol kweli kweli.

Pesa za michongo ndizo watu wananywea pombe na starehe sio hizi za kulala njaa
 
Kosa lingine watu wengi wanafanya ni kujikakamua kusomesha watoto kwenye shule za gharama wakidhani ni sifa.

Kama huna uwezo peleka mtoto kwenye shuke unayomuda ili upate salio la kuendeleza gurudumu.

Huku makazini tunafanya kazi na watu full stress. Ukiuliza eti anasomesha mtoto mwenyewe nursery
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…