BusinessOriented
JF-Expert Member
- Oct 23, 2022
- 259
- 565
Nenda Instagram kamtafute joelnanauka anafundisha sana namna ya watu kujikomboa kiuchumi...na wengi kupitia mafundisho yake wamejikomboa na madeni pia wamesimama kiuchumi hata kama awali walianguka.....Mimi binafsi tumejiari na tunapata pesa kidogo tu lakini life linasonga..yaani haya maisha ni kuwa na nidhamu ya pesa...ukiwa huna mipango ya kuitumia pesa basi pesa yenyewe ndiyo itakupangia matumizi kwa sababu wewe huipangii matumizi...Habari.
Nina miaka 37. Sifurahii maisha katika umri huu. Kama Kuna mtu anaweza kutoa ushauri wa kunikomboa asisite...Mshana Jr etc. Mtiririko wa matukio ni kama ufuatavyo.
1. Ninafanya kazi serikalini mshahara take home ni 1.3m. hapo Nina mkopo wa miaka 5 NMB.
2. Kazi nimeanza tangu 2012. Hivyo Nina miaka 9+ kazini.
3. Naishi Dar es Salaam.
4. Nina mke na watoto wanne. Mtoto wa nne bado ni kichanga.
5. Tangu nianze kazi sijui pesa zangu zinapoenda. Sina kiwanja Sina akiba. Bado nimepanga Kodi laki tatu kwa mwezi.
6. Mahusiano yangu na wife sio mazuri sana kwa sababu ya ugumu wa maisha. Lakini bado tunasonga.
7. Wife Hana kazi Hana biashara.
8. Nakunywa pombe mara kwa mara.
9. Siendi kanisani kabisa ila kwa matukio maalum mfano ndoa, ubatizo wa mtoto, etc
10. Sina gari. Nilioanza nao kazi Wana nyumba kubwa na magari mawili. Moja la wife....
Nahisi Nina mkosi nifanye nini? Yapo mengi kuonesha hasara ninayoihisi. Kazini napata marupurupu ya hapa na pale. Ila najiona sitoboi. Wadogo zangu wenye mshahara wa laki Tano wametoboa mi nipo nipo tu mpka mama yangu amekata tamaa. Faraja yangu iliyobaki ni Binti zangu ambao hawaelewi chochote kwenye hii Dunia ya vita.
Ushauri wa awali ni huu...fungua account, ukipata hata kidogo tupia huko...jipe muda..utakuta umenunua kiwanja na hata kujenga....jiwekee malengo lazima utayatimiza tu...lakini usiache kusali na pia acha pombe na kufuja pesa....
Nidhamu ya pesa ni muhimu.