Maisha yangu baada ya miaka 37!

Kuna watu mnazingua kweli mshahara mil 1.3 una watoto 4 halafu bado unalalamika.
Kuna sister mmoja ni jirani yangu ana watoto 3 watoto 3 ni wa marehemu mdogo wake jumla ana watoto 6 kazi yake ni kuuza nyanya na samaki sokoni anaishi vizuri na furaha ,watoto wote wana afya njema na amejenga vibanda 3.
Wewe mwenye ajira ya kudumu na mshahara wa mil 1.3 bado unalalamika.
Shenzi kabisa acha kazi ili upate furaha
 
Unadhani 20 m ni nyingi? Tena ikiwa bank unafanya tu transanctions....hata 2months inaweza isifike ..ni ndogo
Wewe nadhani levels zako ni za kina Tibaijukwa Makinda etc,20 mil ni pesa kidogo?

Mimi ktk historia yangu ya kutafuta pesa siku nilipofikisha 10mill kwenye account na nikahakikisha kweli namba zinasomeka sahihi ATM card niliivunja nikabaki na vipande viwili ushahidi kwa ajili ya kwenda ku-renew nyengine wakati ukifika,pesa ni nidhamu huwezi kutoka familia yenye njaa ukafanya masihara na pesa.

Huyu jamaa hapa anafanya masihara na pesa na kibaya zaidi anafanya masihara na muda,in reality 37 to 60 ni sawa na kutoka Dar to Bagamoyo sekunde tu atajikuta amekuwa babu alichofanya hakioni.siyo dalili nzuri hata kidogo.
 
Inachoma
 
Mtafute jobless aliesota kitaa kwa miaka 5 au 6 akufundishe maisha
 
Una 4 beautiful girls kwa nyumba, mbona ni blessing hiyo 📌📌

Ulivyoongea Sishangai maana makazini kuna mob physchology ya kushindana lifestyle la mjini. Na unavyoonekana unaishi humo

Kikubwa wewe ni mtu ambae unaendeshwa na upepo wa maneno na maisha ya watu wengine. Huangalii circumstances wala majukumu uliyonayo na ukaishi katika uhalisia wake. Hii ndio sumu kubwa

Kikubwa don't try to fit in brother, live your life katika uhalisia wako 💯💯💯
 
Kila mtu na namna anaona vitu…

Me nakula milo yote, sijibahilii kwenye kula. Nafsi ikitamamani kitu flani naipa.. kuna mdada mmoja akajaga niambia nina matumizi mabaya kwenye msosi.
 
Kabisa naumia niliona wenzangu wanaendesha Suzuki mi nipo nipo tu. Kuna mmoja mpaka alidiriki kuniuliza pesa zangu huwa napeleka wapi.
Btw thank to my girls, wao hunifanya nisikate tamaa. Very young...baba leta hiki mara leta mdoli mara sijui nini hawajui hata mboga ipo au hamna
 
Unayopitia hauko peke yako, ni muda wa kulevel up

Kwanza mkeo atafute shughuli ya kufanya, hata kama kuuza juisi ama kuuza chakula, asaidie kodi za umeme na maji na vifurushi na mboga za majani

Acha pombe, nenda huko kanisani, Kazulu makaburi ya mababu zako (kuna amani utapata moyoni- hiyo ndio asili yetu Afrika mambo y akienda vibaya usiende kwa mganga na wala huna mikosi nenda uwafanyie maombi Mungu arehemu mababu na ndugu zako waliokufa,)

Fanya kazi kwa bidii sana upande cheo kazini

Omba Mungu sana akuepushe na fitna na husda kote kazini na mitaani

Punguza stress, penda kutumia muda wako na watoto wako, watoto hawana stress watakuambukiza mentality yao

Acha kila ujinga unaoujua
Fanya mazoezi.

Mkalishe mkeo chini mwambie mambo ni magumu mjifunge kamba na mkanda filamu la maisha ndio linaanza mapambano zaidi yanafuata. Maana umri wa watoto wako huo hakika bado huna majukumu, ikifika wapo chuo itakuwaje!!
 
Fanya maamuzi magumu
  • Chagua mkoa unaotaka uwe nyumbani kwako
  • Tafuta nyumba ya vyumba viwili, visivyokuwa na gharama kubwa
  • Mkeo, ndio aende akaishi huko
  • We tafuta chumba cha bei nafuu cha ki-bachela upange
  • Punguza pombe , hii inakula pesa sana hasa kwa wale ambao wakilewa hutoa ofa
  • Kila salio unalopata, 3/4 mtumie mkeo na uumpe maelekezo ya namna ya kuzitumia/ aweke akiba ya kununua kiwanja n.k
  • Kwako, binafsi jinyime kwa kujiwekea bajeti ndogo mfano laki 2 au 3; nyingine inayobaki iende nyumbani
  • Baada ya muda utakuwa mshindi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…