Maisha yangu baada ya miaka 37!

Maisha yangu baada ya miaka 37!

Kuna watu mnazingua kweli mshahara mil 1.3 una watoto 4 halafu bado unalalamika.
Kuna sister mmoja ni jirani yangu ana watoto 3 watoto 3 ni wa marehemu mdogo wake jumla ana watoto 6 kazi yake ni kuuza nyanya na samaki sokoni anaishi vizuri na furaha ,watoto wote wana afya njema na amejenga vibanda 3.
Wewe mwenye ajira ya kudumu na mshahara wa mil 1.3 bado unalalamika.
Shenzi kabisa acha kazi ili upate furaha
 
Unadhani 20 m ni nyingi? Tena ikiwa bank unafanya tu transanctions....hata 2months inaweza isifike ..ni ndogo
Wewe nadhani levels zako ni za kina Tibaijukwa Makinda etc,20 mil ni pesa kidogo?

Mimi ktk historia yangu ya kutafuta pesa siku nilipofikisha 10mill kwenye account na nikahakikisha kweli namba zinasomeka sahihi ATM card niliivunja nikabaki na vipande viwili ushahidi kwa ajili ya kwenda ku-renew nyengine wakati ukifika,pesa ni nidhamu huwezi kutoka familia yenye njaa ukafanya masihara na pesa.

Huyu jamaa hapa anafanya masihara na pesa na kibaya zaidi anafanya masihara na muda,in reality 37 to 60 ni sawa na kutoka Dar to Bagamoyo sekunde tu atajikuta amekuwa babu alichofanya hakioni.siyo dalili nzuri hata kidogo.
 
Aisee!Kuna watu mna utani maishani.Take home ni 1.3m.Mkopo 36m.Ukabakiwa na 20 ms!Na bado hauna kiwanja wala "kipando"/gari la kukupunguzia uchovu wa kutembea.Weye jamaa una kipato kikubwa mnoo ila kuna shida katika bajeti yako.Haujachelewa kwa miaka 37.Tuliza akili na uchukue mawazo ya wakuu wa JF.Yafanyie kazi na hakika utafaulu.Kuna watu nikikueleza take home zao utalia kwa kuwaonea huruma.Mikopo yao ni midogo mnoo na wamejenga,wanasomesha na maisha yanasonga.Haujalogwa.Huna mipango tu.
Inachoma
 
Habari.
Nina miaka 37. Sifurahii maisha katika umri huu. Kama Kuna mtu anaweza kutoa ushauri wa kunikomboa asisite...Mshana Jr etc. Mtiririko wa matukio ni kama ufuatavyo.

1. Ninafanya kazi serikalini mshahara take home ni 1.3m. hapo Nina mkopo wa miaka 5 NMB.

2. Kazi nimeanza tangu 2012. Hivyo Nina miaka 9+ kazini.

3. Naishi Dar es Salaam.

4. Nina mke na watoto wanne. Mtoto wa nne bado ni kichanga.

5. Tangu nianze kazi sijui pesa zangu zinapoenda. Sina kiwanja Sina akiba. Bado nimepanga Kodi laki tatu kwa mwezi.

6. Mahusiano yangu na wife sio mazuri sana kwa sababu ya ugumu wa maisha. Lakini bado tunasonga.

7. Wife Hana kazi Hana biashara.

8. Nakunywa pombe mara kwa mara.

9. Siendi kanisani kabisa ila kwa matukio maalum mfano ndoa, ubatizo wa mtoto, etc

10. Sina gari. Nilioanza nao kazi Wana nyumba kubwa na magari mawili. Moja la wife....

Nahisi Nina mkosi nifanye nini? Yapo mengi kuonesha hasara ninayoihisi. Kazini napata marupurupu ya hapa na pale. Ila najiona sitoboi. Wadogo zangu wenye mshahara wa laki Tano wametoboa mi nipo nipo tu mpka mama yangu amekata tamaa. Faraja yangu iliyobaki ni Binti zangu ambao hawaelewi chochote kwenye hii Dunia ya vita.
Mtafute jobless aliesota kitaa kwa miaka 5 au 6 akufundishe maisha
 
Una 4 beautiful girls kwa nyumba, mbona ni blessing hiyo 📌📌

Ulivyoongea Sishangai maana makazini kuna mob physchology ya kushindana lifestyle la mjini. Na unavyoonekana unaishi humo

Kikubwa wewe ni mtu ambae unaendeshwa na upepo wa maneno na maisha ya watu wengine. Huangalii circumstances wala majukumu uliyonayo na ukaishi katika uhalisia wake. Hii ndio sumu kubwa

Kikubwa don't try to fit in brother, live your life katika uhalisia wako 💯💯💯
 
Wewe nadhani levels zako ni za kina Tibaijukwa Makinda etc,20 mil ni pesa kidogo?

Nakumbuka ktk historia yangu ya kutafuta pesa siku nilipofikisha 10mill kwenye account na nikahakikisha kweli namba zinasomeka sahihi ATM card niliivunja nikabaki na vipande viwili ushahidi kwa ajili ya kwenda ku-renew nyengine wakati ukifika,pesa ni nidhamu huwezi kutoka familia yenye njaa ukafanya masihara na pesa.

Huyu jamaa hapa anafanya masihara na pesa na kibaya zaidi anafanya masihara na muda,in reality 37 to 60 ni sawa na kutoka Dar to Bagamoyo sekunde tu atajikuta amekuwa babu alichofanya hakioni.siyo dalili nzuri hata kidogo.
Kila mtu na namna anaona vitu…

Me nakula milo yote, sijibahilii kwenye kula. Nafsi ikitamamani kitu flani naipa.. kuna mdada mmoja akajaga niambia nina matumizi mabaya kwenye msosi.
 
Una 4 beautiful girls kwa nyumba, mbona ni blessing hiyo 📌📌

Ulivyoongea Sishangai maana makazini kuna mob physchology ya kushindana lifestyle la mjini. Na unavyoonekana unaishi humo

Kikubwa wewe ni mtu ambae unaendeshwa na upepo wa maneno na maisha ya watu wengine. Huangalii circumstances wala majukumu uliyonayo na ukaishi katika uhalisia wake. Hii ndio sumu kubwa

Kikubwa don't try to fit in brother, live your life katika uhalisia wako 💯💯💯
Kabisa naumia niliona wenzangu wanaendesha Suzuki mi nipo nipo tu. Kuna mmoja mpaka alidiriki kuniuliza pesa zangu huwa napeleka wapi.
Btw thank to my girls, wao hunifanya nisikate tamaa. Very young...baba leta hiki mara leta mdoli mara sijui nini hawajui hata mboga ipo au hamna
 
Habari.
Nina miaka 37. Sifurahii maisha katika umri huu. Kama Kuna mtu anaweza kutoa ushauri wa kunikomboa asisite...Mshana Jr etc. Mtiririko wa matukio ni kama ufuatavyo.

1. Ninafanya kazi serikalini mshahara take home ni 1.3m. hapo Nina mkopo wa miaka 5 NMB.

2. Kazi nimeanza tangu 2012. Hivyo Nina miaka 9+ kazini.

3. Naishi Dar es Salaam.

4. Nina mke na watoto wanne. Mtoto wa nne bado ni kichanga.

5. Tangu nianze kazi sijui pesa zangu zinapoenda. Sina kiwanja Sina akiba. Bado nimepanga Kodi laki tatu kwa mwezi.

6. Mahusiano yangu na wife sio mazuri sana kwa sababu ya ugumu wa maisha. Lakini bado tunasonga.

7. Wife Hana kazi Hana biashara.

8. Nakunywa pombe mara kwa mara.

9. Siendi kanisani kabisa ila kwa matukio maalum mfano ndoa, ubatizo wa mtoto, etc

10. Sina gari. Nilioanza nao kazi Wana nyumba kubwa na magari mawili. Moja la wife....

Nahisi Nina mkosi nifanye nini? Yapo mengi kuonesha hasara ninayoihisi. Kazini napata marupurupu ya hapa na pale. Ila najiona sitoboi. Wadogo zangu wenye mshahara wa laki Tano wametoboa mi nipo nipo tu mpka mama yangu amekata tamaa. Faraja yangu iliyobaki ni Binti zangu ambao hawaelewi chochote kwenye hii Dunia ya vita.
Unayopitia hauko peke yako, ni muda wa kulevel up

Kwanza mkeo atafute shughuli ya kufanya, hata kama kuuza juisi ama kuuza chakula, asaidie kodi za umeme na maji na vifurushi na mboga za majani

Acha pombe, nenda huko kanisani, Kazulu makaburi ya mababu zako (kuna amani utapata moyoni- hiyo ndio asili yetu Afrika mambo y akienda vibaya usiende kwa mganga na wala huna mikosi nenda uwafanyie maombi Mungu arehemu mababu na ndugu zako waliokufa,)

Fanya kazi kwa bidii sana upande cheo kazini

Omba Mungu sana akuepushe na fitna na husda kote kazini na mitaani

Punguza stress, penda kutumia muda wako na watoto wako, watoto hawana stress watakuambukiza mentality yao

Acha kila ujinga unaoujua
Fanya mazoezi.

Mkalishe mkeo chini mwambie mambo ni magumu mjifunge kamba na mkanda filamu la maisha ndio linaanza mapambano zaidi yanafuata. Maana umri wa watoto wako huo hakika bado huna majukumu, ikifika wapo chuo itakuwaje!!
 
Fanya maamuzi magumu
  • Chagua mkoa unaotaka uwe nyumbani kwako
  • Tafuta nyumba ya vyumba viwili, visivyokuwa na gharama kubwa
  • Mkeo, ndio aende akaishi huko
  • We tafuta chumba cha bei nafuu cha ki-bachela upange
  • Punguza pombe , hii inakula pesa sana hasa kwa wale ambao wakilewa hutoa ofa
  • Kila salio unalopata, 3/4 mtumie mkeo na uumpe maelekezo ya namna ya kuzitumia/ aweke akiba ya kununua kiwanja n.k
  • Kwako, binafsi jinyime kwa kujiwekea bajeti ndogo mfano laki 2 au 3; nyingine inayobaki iende nyumbani
  • Baada ya muda utakuwa mshindi
 
Back
Top Bottom