Maisha yangu baada ya miaka 37!

Na hiyo ndio inatakiwa kuwa sehemu ya furaha yako kaka lakini pia ikupush kujua kuwa maisha uliyonayo sasa ni yao si yako.
Ukishondwa wewe wameshindwa wao maana hata mkeo hawezi kuwasimamia

Imagine kesho yakitokea ya kutokea, unadhani mabinti zako watakuwa na future gani au hujakaa na barmaids, machangudoa, wauza genge au hata wadangaji ukajua stories zao. Sio wote wametoka familia maskini ila familia ilipoyumba wakajikuta hawana option

Je, ungependa kuwaacha mabinti zako kwenye hiyo sintofahamu katika ulimwengu katili kwa wanawake

Ukilifikiria hili utaacha kuwa mbinafsi wa kujifikiria wewe binafsi na leo yako. Utajinyima hadi senti ya mwisho kuhakikisha unatengeneza msingi wa mabinti zako

Hao wote unapwafurahisha kwa maisha ya kuigiza hawatokuwa na msaada ukiumwa na wala kuwasaidia wanao utakapoondoka. Then kwa nini unawapa umuhimu

Pia usijilaumu sana, binadamu wote tunafanya makosa lakini kujilaumu haifuti makosa ambayo yameshatokea. Focus na masaa na siku zijazo maana hizo ndo zitabadili kila kitu ,all the best brother πŸ™πŸ™
 
1.3m hauwezi kuwa na maendeleo kwa mshahara.

Umechezea mkopo ,hauwezi kuitapakanya yote 36m , ilikuaje ukalipa loan board pesa yote hiyo kwa pamoja?
Hio pesa ni ndefu,Watu wanalipwa laki 3 na wanafanya maendeleo.
Aanze na alichonacho.

unakuta mama ntilie kapiga room zake mbili safi,maji,umeme kaweka na anasomesha.Maisha ni mipango,kashindwa kupanga
 
Mchawi wako ni pombe.
 
Mke wako ndo shida.

Anakuwaje Goli kipa katika ulimwengu huu.
 
Nilikua namjibu yule wa juu anayehis ni uongo..ishu zingine take it easy
 
Nadhani hiyo Milioni 20 sio hela ulipata cash but inatokana na top up.kuna uwezekano ulichukua mkopo kidogo mwanzoni mwa miaka ulipokuwa unaanza kazi kisha bafaye uka top up tens ndio maana hukuona hela ilipokwenda.
 
Mbona nahisi umebarikiwa Sana kuliko Mimi,maana Nina umri angalau chini kidogo ya huo
1.Sina nyumba
2.sina mke
3.sina mtoto
4.nina mkopo
5.nashukuru Mungu sinywi pombe na sijachangangikiwa kesho ni Bora na nitafanikiwa
Usiwe na hofu brother umebarikiwa sana kuanzia sasa acha pombe nenda kanisani furahia maisha upangaji sio laana ni hatua ya maisha wasalimie watoto hapo nyumbani
 
Hio pesa ni ndefu,Watu wanalipwa laki 3 na wanafanya maendeleo.
Aanze na alichonacho.

unakuta mama ntilie kapiga room zake mbili safi,maji,umeme kaweka na anasomesha.Maisha ni mipango,kashindwa kupanga

Mkuu usichangamshe genge , 1.3m hauwezi kufanya kitu cha kushangaza labda utajiri wa kibongo kuwa na vyumba viwili polisi post na kibakuli(duet,vitz,fan cargo,bB,march etc) ,kumbuka ana mkopo maana yake anapigwa panga kwenye hiyo 1.3m.

 
Jaribu kuhama Dar ujaribu maisha sehemu nyingine
 
Mkuu, Naomba unisaidie Soft copy ya hiki kitabu.
Ntakuwekea hapa ila Kuna huu uzi jamaa alikiweka hapa Kwa tafsiri ya kiswahili.

 
Download app inaitwa 'Money Lover' mkuu. Kisha ingiza matumizi yako ya kila siku kwa miezi 3 ijayo..

Utajua pesa zako zinaenda wapi na nini cha kurekebisha.
Asante sana
Very powerful, asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…