Maisha yangu baada ya miaka 37!

Maisha yangu baada ya miaka 37!

Kwanza kanisani huendi unadhulumu Hela za zaka na michango kede unaenda kulewea🤣, na bado unalalama kuwa Hela huoni. Aisee tunaenda kanisani maisha magumu na bado Kuna sadaka, zaka, harambee, shukrani, na michango ya wahitaji ambayo hulipi. .

1. Kwanza kabisa acha kumdhulumu padri unataka akale wapi?
2 Pili jitahidi kupunguza gharama angalia matumizi yasiyo ya lazima, achana nayo
3. Mtafutie mama watoto wako Kaz ambayo anaweza Fanya hata akiwa nyumbani hata kuuza viungo vya chai na pilau
4. Fanya uzazi wa mpango ikiwezekama usipate mtoto mwingine kwa sasa. Fanya Vasectomy ( fungal mirija ya pumbu usitoe mbegu)
5. Jenga amani na furaha sana na mkeo achana na watu wa dunia. Huyo anakuvumilia mengi hujui tu. .

Mwisho kabisa hata mie Niko kwenye ndoa aisee ndoa tamu ukipuuzia mambo. Ukiwaza Kila Jambo utaumwa mda mwingine tunaweza chemsha mahindi Huku tunapigana denda siku inaisha😊

Kumbuka miaka mia toka sasa utakuwa umekufa utaona Kuna mambo hayana msingi. Acha kulewea na marafiki Kaa karibu na mkeo. .
 
Panga budget kwa Kila mwezi ya matumizi ya nyumbani

Track expenses zote usitumie kitu bila kuandika mwisho wa mwezi kuja kuangalia utajikuta umetumia Hela nyingi kwenye matumizi yasiyo ya lazima uanze kuyapunguza hayo matumizi yasiyo ya lazima

Weka malengo yagawe kwa vipindi vifupi then yawekee deadline

Weka akiba Kila mwezi Kwa ajili ya kufanikisha malengo ni kosa kubwa kutumia Hela yote unayopata mwisho wa mwezi

Mfungulie mke wako biashara msaidiane humo ndani Tena ikiwezekana hii ndo uanze nayo
 
Mkosi ni akili yako tu kaka.

Fanya mambo kadhaa muhimu:

1.Kaa na mkeo na mpange budget ya matumizi ya fedha mnayopata…kwenye mshahara wako jitahidi uwe unaweka 10% kama dharura na 5% iwe budget yako ya gambe na matumizi yako binafsi (jipende).

2.Tenga kiasi cha akiba kila mwezi kwa ajili ya kufungua kitega uchumi kingine; anza na wife mwambia anaweza kujishughulisha na nini. Weka malengo ya akiba kiasi gani ya kuweka na kwa muda gani mpaka wife awe na bishara.

3.Wakati unaweka akiba kwa ajili ya biashara ya wife, fanya utafiti wa kina kuhusu hiyo biashara kumbuka kuwa tuna fedha kichele hivyo ni vyema tusiipoteze kwa kutokuwa na uelewa na tunachokifanya.

3.Punguza matumizi yasiyo ya lazima; birtdhay za kifahari, michango isiyo ya lazima, pombe n.k punguza.

4.Wakumbuke wazazi na kuwatunza: Baraka zao zitakufungua sana hutaamini.

5.Usijilinganishe na wengine. Kujilinganisha kutakufanya ukate tamaa na kuona umechelewa.

6.Jitahidi utumie uzazi wa mpango, watoto uliobarikiwa wanatosha.

7.Hakikisha familia nzima mna bima ya afya, gharama za matibabu huwa zinarudisha watu nyuma sana.

Kila la Kheri

Ushauri murua sana huu
 
Tatizo lako lipo hapa

ID yako ni Kufa Kuzikana, kwa nini umechagua ili neno. Wakati Mwingine majina yanabeba siri katika maisha yetu.

Unahitaji Ukombozi wa kufunguliwa so tafuta Mchungaji wa kweli upate kufunguliwa. Inawezekana umeunganishwa unachokipanga kinajulikana wanakuja kuharibu mipango yako.
 
Habari.
Nina miaka 37. Sifurahii maisha katika umri huu. Kama Kuna mtu anaweza kutoa ushauri wa kunikomboa asisite...Mshana Jr etc. Mtiririko wa matukio ni kama ufuatavyo.

1. Ninafanya kazi serikalini mshahara take home ni 1.3m. hapo Nina mkopo wa miaka 5 NMB.

2. Kazi nimeanza tangu 2012. Hivyo Nina miaka 9+ kazini.

3. Naishi Dar es Salaam.

4. Nina mke na watoto wanne. Mtoto wa nne bado ni kichanga.

5. Tangu nianze kazi sijui pesa zangu zinapoenda. Sina kiwanja Sina akiba. Bado nimepanga Kodi laki tatu kwa mwezi.

6. Mahusiano yangu na wife sio mazuri sana kwa sababu ya ugumu wa maisha. Lakini bado tunasonga.

7. Wife Hana kazi Hana biashara.

8. Nakunywa pombe mara kwa mara.

9. Siendi kanisani kabisa ila kwa matukio maalum mfano ndoa, ubatizo wa mtoto, etc

10. Sina gari. Nilioanza nao kazi Wana nyumba kubwa na magari mawili. Moja la wife....

Nahisi Nina mkosi nifanye nini? Yapo mengi kuonesha hasara ninayoihisi. Kazini napata marupurupu ya hapa na pale. Ila najiona sitoboi. Wadogo zangu wenye mshahara wa laki Tano wametoboa mi nipo nipo tu mpka mama yangu amekata tamaa. Faraja yangu iliyobaki ni Binti zangu ambao hawaelewi chochote kwenye hii Dunia ya vita.
Huna mkosi wowote, mchawi hapo ninahisi ni hiyo namba nane hapo. Pombe, Pombe, Pombe, Pombe....

Acha pombe ndugu yangu, baada ya miaka mitatu tu, utakuja hapa kunishukuru.
 
Habari.
Nina miaka 37. Sifurahii maisha katika umri huu. Kama Kuna mtu anaweza kutoa ushauri wa kunikomboa asisite...Mshana Jr etc. Mtiririko wa matukio ni kama ufuatavyo.

1. Ninafanya kazi serikalini mshahara take home ni 1.3m. hapo Nina mkopo wa miaka 5 NMB.

2. Kazi nimeanza tangu 2012. Hivyo Nina miaka 9+ kazini.

3. Naishi Dar es Salaam.

4. Nina mke na watoto wanne. Mtoto wa nne bado ni kichanga.

5. Tangu nianze kazi sijui pesa zangu zinapoenda. Sina kiwanja Sina akiba. Bado nimepanga Kodi laki tatu kwa mwezi.

6. Mahusiano yangu na wife sio mazuri sana kwa sababu ya ugumu wa maisha. Lakini bado tunasonga.

7. Wife Hana kazi Hana biashara.

8. Nakunywa pombe mara kwa mara.

9. Siendi kanisani kabisa ila kwa matukio maalum mfano ndoa, ubatizo wa mtoto, etc

10. Sina gari. Nilioanza nao kazi Wana nyumba kubwa na magari mawili. Moja la wife....

Nahisi Nina mkosi nifanye nini? Yapo mengi kuonesha hasara ninayoihisi. Kazini napata marupurupu ya hapa na pale. Ila najiona sitoboi. Wadogo zangu wenye mshahara wa laki Tano wametoboa mi nipo nipo tu mpka mama yangu amekata tamaa. Faraja yangu iliyobaki ni Binti zangu ambao hawaelewi chochote kwenye hii Dunia ya vita.
Mkuu, wewe ni mlevi na kodi ya Nyumba laki tatu kwa mwezi, kisha hujui pesa inaenda wapi
 
Back
Top Bottom