Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuhusu wife almost umepatia but it was love at the first sight. But haikuwa issue ya mimba.Ungekuwa na kiwanja ningekushauri ujenge vyumba viwili uhamie.
Kodi ni kubwa mno!
Wifey? Nahisi ni wale pata mimba kisha sogea tuje tuishi/tuoane tulee watoto.
Kazi gani hiyo unalipwa ujira Mdogo hivyo ?
Tafuta Kazi ya maana au Biashara kubwa Stress zinasababishwa Na low income earning
Mkosi ni akili yako tu kaka.
Fanya mambo kadhaa muhimu:
1.Kaa na mkeo na mpange budget ya matumizi ya fedha mnayopata…kwenye mshahara wako jitahidi uwe unaweka 10% kama dharura na 5% iwe budget yako ya gambe na matumizi yako binafsi (jipende).
2.Tenga kiasi cha akiba kila mwezi kwa ajili ya kufungua kitega uchumi kingine; anza na wife mwambia anaweza kujishughulisha na nini. Weka malengo ya akiba kiasi gani ya kuweka na kwa muda gani mpaka wife awe na bishara.
3.Wakati unaweka akiba kwa ajili ya biashara ya wife, fanya utafiti wa kina kuhusu hiyo biashara kumbuka kuwa tuna fedha kichele hivyo ni vyema tusiipoteze kwa kutokuwa na uelewa na tunachokifanya.
3.Punguza matumizi yasiyo ya lazima; birtdhay za kifahari, michango isiyo ya lazima, pombe n.k punguza.
4.Wakumbuke wazazi na kuwatunza: Baraka zao zitakufungua sana hutaamini.
5.Usijilinganishe na wengine. Kujilinganisha kutakufanya ukate tamaa na kuona umechelewa.
6.Jitahidi utumie uzazi wa mpango, watoto uliobarikiwa wanatosha.
7.Hakikisha familia nzima mna bima ya afya, gharama za matibabu huwa zinarudisha watu nyuma sana.
Kila la Kheri
Baada ya kukatwa mkopo 1.3 ni ujira mdogo nchi hii. Wewe utakua hujui mishahara ya serikali. Hiyo ni kati ya mishahara mikubwa ukiacha hii ya viongizozi.
Hela ndogo Sana hiyoKipato cha milioni 1 na laki 3 sio kidogo kwa maisha ya Kitanzania..
Zaidi ya 80 % wa raia .. hawafikii hicho kipato
Hela ndogo Sana hiyo
Huna mkosi wowote, mchawi hapo ninahisi ni hiyo namba nane hapo. Pombe, Pombe, Pombe, Pombe....Habari.
Nina miaka 37. Sifurahii maisha katika umri huu. Kama Kuna mtu anaweza kutoa ushauri wa kunikomboa asisite...Mshana Jr etc. Mtiririko wa matukio ni kama ufuatavyo.
1. Ninafanya kazi serikalini mshahara take home ni 1.3m. hapo Nina mkopo wa miaka 5 NMB.
2. Kazi nimeanza tangu 2012. Hivyo Nina miaka 9+ kazini.
3. Naishi Dar es Salaam.
4. Nina mke na watoto wanne. Mtoto wa nne bado ni kichanga.
5. Tangu nianze kazi sijui pesa zangu zinapoenda. Sina kiwanja Sina akiba. Bado nimepanga Kodi laki tatu kwa mwezi.
6. Mahusiano yangu na wife sio mazuri sana kwa sababu ya ugumu wa maisha. Lakini bado tunasonga.
7. Wife Hana kazi Hana biashara.
8. Nakunywa pombe mara kwa mara.
9. Siendi kanisani kabisa ila kwa matukio maalum mfano ndoa, ubatizo wa mtoto, etc
10. Sina gari. Nilioanza nao kazi Wana nyumba kubwa na magari mawili. Moja la wife....
Nahisi Nina mkosi nifanye nini? Yapo mengi kuonesha hasara ninayoihisi. Kazini napata marupurupu ya hapa na pale. Ila najiona sitoboi. Wadogo zangu wenye mshahara wa laki Tano wametoboa mi nipo nipo tu mpka mama yangu amekata tamaa. Faraja yangu iliyobaki ni Binti zangu ambao hawaelewi chochote kwenye hii Dunia ya vita.
Mkuu, wewe ni mlevi na kodi ya Nyumba laki tatu kwa mwezi, kisha hujui pesa inaenda wapiHabari.

Mwanaume waki Afrika toka lini akawa na pesa akakubali ushauri wa mke wake.Mke wako ndo mchawi, hajakushauri ununue kiwanja ujenge?
Anakula tuu?
Wapo wengi SanaNi ndogo kwa wachache ila kwa wengi ni nyingi
Hivi unahisi ni asilimia ngapi za raia wa Tanzania wanafikia hicho kipato?