Habari.
Nina miaka 37. Sifurahii maisha katika umri huu. Kama Kuna mtu anaweza kutoa ushauri wa kunikomboa asisite...Mshana Jr etc. Mtiririko wa matukio ni kama ufuatavyo.
1. Ninafanya kazi serikalini mshahara take home ni 1.3m. hapo Nina mkopo wa miaka 5 NMB.
2. Kazi nimeanza tangu 2012. Hivyo Nina miaka 9+ kazini.
3. Naishi Dar es Salaam.
4. Nina mke na watoto wanne. Mtoto wa nne bado ni kichanga.
5. Tangu nianze kazi sijui pesa zangu zinapoenda. Sina kiwanja Sina akiba. Bado nimepanga Kodi laki tatu kwa mwezi.
6. Mahusiano yangu na wife sio mazuri sana kwa sababu ya ugumu wa maisha. Lakini bado tunasonga.
7. Wife Hana kazi Hana biashara.
8. Nakunywa pombe mara kwa mara.
9. Siendi kanisani kabisa ila kwa matukio maalum mfano ndoa, ubatizo wa mtoto, etc
10. Sina gari. Nilioanza nao kazi Wana nyumba kubwa na magari mawili. Moja la wife....
Nahisi Nina mkosi nifanye nini? Yapo mengi kuonesha hasara ninayoihisi. Kazini napata marupurupu ya hapa na pale. Ila najiona sitoboi. Wadogo zangu wenye mshahara wa laki Tano wametoboa mi nipo nipo tu mpka mama yangu amekata tamaa. Faraja yangu iliyobaki ni Binti zangu ambao hawaelewi chochote kwenye hii Dunia ya vita.
Pole sana ndugu
Kufa kuzikana
You are still young bro.
Sasa tufanyeje ili ujione mwenye mafanikio ?
Basi ni rahisi sikushauri kuacha pombe ila nakushauri kupunguza ikiwa unakunywa kwa kiasi kikubwa cha hela.
Kaka mpaka sasa jitafute uko wapi? Ikiwa ni biashara jiulize ni ipi unaona waweza kuimudu basi jiwekeze huko ila hapa nikueleze ukweli kuwa usifanye biashara za kuiga mara mbona fulani imemtoa
Biashara za namna hiyo achana nazo ila jitizame ni biashara gani unahisikia toka moyoni na kuwa na amani nayo nasema hivi maana najua utaifanya kwa moyo sio kusukumwa na pia utaisimamia.
Japo sio lazima biashara kuna uwekezaji hata wa kilimo hata majumba lakini kote kutokane na willing kutoka moyoni mwako.
Nakuona unaniuliza mtaji nautoa wapi ?
Ndugu mkopo ulionao wa miaka mitano ni mdogo sana ila pia sikutumi kukopa tena .
Ila sasa nakutuma kupunguza gharama za maisha hapo nyumbani hata kutafuta nyumba ya hela kidogo kuasi walau laki na nusu.
Na pia nyumbani punguza matumizi yasiyo ya lazima na pombe kunywa kiafya na kiuchumi zaidi.
Sasa kwanini upunguze matumizi ?
Nahitaji mshahara wako ujitunzie kiasi kidogo kidogo walau hata laki sita au nne kwa mwezi.
Kutunza ni ngumu si et eeh ? Basi ni hivi fungua akaunti ya fixed ambayo kila mwisho wa mwezi toa hela peleka huko ili utunze au katika mshahara wako weka standing order ya kiasi hicho kikatwe na kitunzwe walau kwa mwaka.
Kaka ndani ya mwaka kwa hizo savings tayari hela ya kuanzia biashara unayo , Anza huku unaisikilizia ikisimama na ukajua faida na hasara zake , sasa ikuze na mkopo ili ikuzalishie zaidi .
Pole ila jitahidi kufanya haya japo najua ni kazi sana ila jicommit kama vile ulivyoamua kujieleza hapa.
Sent using
Jamii Forums mobile app