Maisha yangu baada ya miaka 37!

Maisha yangu baada ya miaka 37!

Kama vipi toa ushauri hili Mshana akija akute umeshatema cheche..
Mtu akishaitwa rasmi ili kutoa ushauri, maana yake ushauri wake ndiyo unahitajika zaidi, wengine tunatakiwa tutulize mikwizu kwanza.
 
Habari.

Nina miaka 37. Sifurahii maisha katika umri huu. Kama kuna mtu anaweza kutoa ushauri wa kunikomboa asisite, Mshana Jr n.k. Mtiririko wa matukio ni kama ufuatavyo;

1. Ninafanya kazi serikalini mshahara take home ni 1.3 m., hapo nina mkopo wa miaka 5 NMB.
Mkosi ni huyo mkeo na si ajabu ulimwambia asifanye kazi. Mtoto wa mwisho akifikisha umri flani mwambie afanye biashara au atafute kazi. Mkiweza afanye hata online business.
 
Screenshots_2022-10-28-07-14-43.jpg
 
Pia hao watoto 4 wanatosha mkuu,shida sisi wabongo ukiwa huna hela na hamu ya kufanya ngono ndo inazidi. Mwambie mkeo atumie njia za uzazi then muanzie hapo kujikwamua...maana wakikua hao shule zikianza ndo utapagawa.
Kweli kabisa aisee
 
Acha pombe rafiki, pombe haiingizi bali hutoa, na pombe, ukiwa ni myanji wa kila siku hiyo nayo ni kesi kubwa
 
Una 1.3 take home, una maanisha milion na laki tatu au laki na thelasini?
 
Mkosi ni akili yako tu kaka.

Fanya mambo kadhaa muhimu:

1.Kaa na mkeo na mpange budget ya matumizi ya fedha mnayopata…kwenye mshahara wako jitahidi uwe unaweka 10% kama dharura na 5% iwe budget yako ya gambe na matumizi yako binafsi (jipende).

2.Tenga kiasi cha akiba kila mwezi kwa ajili ya kufungua kitega uchumi kingine; anza na wife mwambia anaweza kujishughulisha na nini. Weka malengo ya akiba kiasi gani ya kuweka na kwa muda gani mpaka wife awe na bishara.

3.Wakati unaweka akiba kwa ajili ya biashara ya wife, fanya utafiti wa kina kuhusu hiyo biashara kumbuka kuwa tuna fedha kichele hivyo ni vyema tusiipoteze kwa kutokuwa na uelewa na tunachokifanya.

3.Punguza matumizi yasiyo ya lazima; birtdhay za kifahari, michango isiyo ya lazima, pombe n.k punguza.

4.Wakumbuke wazazi na kuwatunza: Baraka zao zitakufungua sana hutaamini.

5.Usijilinganishe na wengine. Kujilinganisha kutakufanya ukate tamaa na kuona umechelewa.

6.Jitahidi utumie uzazi wa mpango, watoto uliobarikiwa wanatosha.

7.Hakikisha familia nzima mna bima ya afya, gharama za matibabu huwa zinarudisha watu nyuma sana.


Kila la Kheri
aisee, thank you sana mkuu

huu ushauri tuuchue wengi utatuvusha
 
Asante sana
Pole ndugu,usifananishe Manisha yako na ya Ntu mwingine,Kwani unayeona anefanikiwa pamoja na kipato kidogo anaweza kuwa mwizi,Ila wewe huamini katika kuiba,hivyi kwa za ridhika na Hali yako,tuliza akili pangilia nini ni muhimu zaidi kufikia malengo yako,mapeema asubuhi utatoboa.

Watoto 4, Mke na 300k kodi, gambe kimtindo, hapo balaa, kwa maisha ya kibongo noma hapo bado zile dharula za hapa na pale, Muhimu wife angekuwa naye anapiga mishe ingesaidia sana, bila ya hvyo komaa upate biashara ya maana kwa pesa unayolipwa unaweza kuanzisha kitu kikakutoa zaidi
Usipofanya maamuzi mapema madogo wote wakiwa school ndo shughuli yako imeishia hapo , utapanga for long time ukizingatia age ishaenda mzee, m namjua mtu mzima mmoja hivi anakazi lakini anaishi kwenye chumba na sebure (kapanga) yeye , mke, watoto wake wawili na mmoja wa hao watoto wake nayeye ana mtoto, na jamaa anakaribia 60 sasa hivi, haya mambo yanaogopesha sana kwa sisi vijana maada muda hausimami
Asante sana kwa ushauri
 
Kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya usitumie pesa zaidi ya mapato yako. Lakini jaribu kusoma vitabu vya uchumi I recommend you to read The richest man in Babylon it might help you, pia usione kama umechelewa amini bado muda unao wa kurekebisha ulipokosea.
Asante sana kwa ushauri
 
Bro shida ipo kwenye akili yako tu ila we ndo wa kuamua kuishi nayo au kuachana nayo dat all
Habari.

Nina miaka 37. Sifurahii maisha katika umri huu. Kama kuna mtu anaweza kutoa ushauri wa kunikomboa asisite, Mshana Jr n.k. Mtiririko wa matukio ni kama ufuatavyo;

1. Ninafanya kazi serikalini mshahara take home ni 1.3 m., hapo nina mkopo wa miaka 5 NMB.

2. Kazi nimeanza tangu 2012, hivyo nina miaka 9+ kazini.

3. Naishi Dar es Salaam.

4. Nina mke na watoto wanne, mtoto wa nne bado ni kichanga.

5. Tangu nianze kazi sijui pesa zangu zinapoenda, sina kiwanja, sina akiba, bado nimepanga, kodi laki tatu kwa mwezi.

6. Mahusiano yangu na mke siyo mazuri sana kwa sababu ya ugumu wa maisha, lakini bado tunasonga.

7. Mke hana kazi, hana biashara.

8. Nakunywa pombe mara kwa mara.

9. Siendi kanisani kabisa ila kwa matukio maalum mfano ndoa, ubatizo wa mtoto, n.k.

10. Sina gari, niliyoanza nao kazi wana nyumba kubwa na magari mawili, moja la mke.

Nahisi nina mkosi, nifanye nini? Yapo mengi kuonesha hasara ninayoihisi. Kazini napata marupurupu ya hapa na pale, ila najiona sitoboi. Wadogo zangu wenye mshahara wa laki tano wametoboa mi nipo nipo tu mpaka mama yangu amekata tamaa. Faraja yangu iliyobaki ni binti zangu ambao hawaelewi chochote kwenye hii Dunia ya vita.
 
Wadau nashukuru kwa maoni na ushauri. Nitafanyia kazi maeneo yafuatayo; gambe; biashara ya familia; saving; na kujifunga mkanda(kubana matumizi). Nikifika miaka 38 nitaleta Uzi kuona nini kimebadilika. Asanteni sana.
 
Always hela sometime huendana na bahati.
Kwa hiyo hiyo milion 20 huenda ungepeleka kwenye biashara,ingebuma.

Nakushauri kwa jinsi navokuana ulivoanza kupanick na stress,ukianzisha biashara huenda ikabuma.

Nakushauri tafuta eneo anza ujenzi taratibu,hata kama utaambiwa unazika pesa fresh tu,as long unaona hela imeenda wapi.Kichwa kikitulia ndo uanze na biashara taratibu

Mimi ni wale waumini wa kuwekeza kwenye ardhi,nimeona faida nyingi sana japo nilianzisha na biashara huku nikiendelea na kazi.
 
Back
Top Bottom