Mkosi ni akili yako tu kaka.
Fanya mambo kadhaa muhimu:
1.Kaa na mkeo na mpange budget ya matumizi ya fedha mnayopata…kwenye mshahara wako jitahidi uwe unaweka 10% kama dharura na 5% iwe budget yako ya gambe na matumizi yako binafsi (jipende).
2.Tenga kiasi cha akiba kila mwezi kwa ajili ya kufungua kitega uchumi kingine; anza na wife mwambia anaweza kujishughulisha na nini. Weka malengo ya akiba kiasi gani ya kuweka na kwa muda gani mpaka wife awe na bishara.
3.Wakati unaweka akiba kwa ajili ya biashara ya wife, fanya utafiti wa kina kuhusu hiyo biashara kumbuka kuwa tuna fedha kichele hivyo ni vyema tusiipoteze kwa kutokuwa na uelewa na tunachokifanya.
3.Punguza matumizi yasiyo ya lazima; birtdhay za kifahari, michango isiyo ya lazima, pombe n.k punguza.
4.Wakumbuke wazazi na kuwatunza: Baraka zao zitakufungua sana hutaamini.
5.Usijilinganishe na wengine. Kujilinganisha kutakufanya ukate tamaa na kuona umechelewa.
6.Jitahidi utumie uzazi wa mpango, watoto uliobarikiwa wanatosha.
7.Hakikisha familia nzima mna bima ya afya, gharama za matibabu huwa zinarudisha watu nyuma sana.
Kila la Kheri