Maisha yangu baada ya miaka 37!

Maisha yangu baada ya miaka 37!

Pia hao watoto 4 wanatosha mkuu,shida sisi wabongo ukiwa huna hela na hamu ya kufanya ngono ndo inazidi. Mwambie mkeo atumie njia za uzazi then muanzie hapo kujikwamua...maana wakikua hao shule zikianza ndo utapagawa.

Ndiomaana wengine wanawakatiza watoto wao masomo, yani siku hizi shule sio ishu kabisa 😁😁😁 yani unampeleka mtoto wako kutoa ujinga tu
 
Nimesoma stori yako mkuu imenigusa mimi sina umri huo ila napitia 60% ya ulichoandika na ni wengi pia wanapitia.

Changamoto iliyopo mshahara wako umekuwa fixed kwenye

1. kodi
2. Ada
3. Chakula
4. Matibabu
5. Mavazi na shida za mama na watoto

yaaani ukijumlisha yote hapo juu total ni mshahara wako na sometimes inazidi mshahara

SOLUTION 1

Please think of the side hustle cut your budget from anywhere in the list above and strictly anza kuweka akiba. Unatakiwa kuwa committed sana kwenye hili usisubiri iwe nyingi invest kwenye side hustle uta FAIL na kupata challenge mwanzoni but i tell you it will become the main money stream unayotegemea kuliko salary. Fanya hivyo kabla hujapoteza hiyo ajira.

SOLUTION 2

Wanawake wanaweza kukufanya uwe tajiri lakini pia masikini dont listen too much to your wife kwenye financial decisions be bold. Kama ana-upeo fulani tafuta namna ya kumfanya atengeneza stream of income you cant rely on single source

I thank God kwangu nina streams mbili za income ukitoa mshahara hii imekuwa solution kiukweli japo bado naona kuna changamoto lakini zitaisha tu

Pole sana mkuu

Please note: Shida zako sio spiritua sio sababu huendi kanisani wala si sababu unakunywa pombe lakini sababu ni mahitaji ni makubwa ukilinganisha na idadi ya streams

God bless you.
 
Mkosi ni akili yako tu kaka.

Fanya mambo kadhaa muhimu:

1.Kaa na mkeo na mpange budget ya matumizi ya fedha mnayopata…kwenye mshahara wako jitahidi uwe unaweka 10% kama dharura na 5% iwe budget yako ya gambe na matumizi yako binafsi (jipende).

2.Tenga kiasi cha akiba kila mwezi kwa ajili ya kufungua kitega uchumi kingine; anza na wife mwambia anaweza kujishughulisha na nini. Weka malengo ya akiba kiasi gani ya kuweka na kwa muda gani mpaka wife awe na bishara.

3.Wakati unaweka akiba kwa ajili ya biashara ya wife, fanya utafiti wa kina kuhusu hiyo biashara kumbuka kuwa tuna fedha kichele hivyo ni vyema tusiipoteze kwa kutokuwa na uelewa na tunachokifanya.

3.Punguza matumizi yasiyo ya lazima; birtdhay za kifahari, michango isiyo ya lazima, pombe n.k punguza.

4.Wakumbuke wazazi na kuwatunza: Baraka zao zitakufungua sana hutaamini.

5.Usijilinganishe na wengine. Kujilinganisha kutakufanya ukate tamaa na kuona umechelewa.

6.Jitahidi utumie uzazi wa mpango, watoto uliobarikiwa wanatosha.

7.Hakikisha familia nzima mna bima ya afya, gharama za matibabu huwa zinarudisha watu nyuma sana.


Kila la Kheri
Real Author, ishi huku.
 
I can feel you.
Pole sana Mkuu.
Kuanzia sasa naona umeashajua tatizo hivo anza kuchukua hatua.

Jitahidi weka akiba kila mwezi hata kama ni kidogo au ikiwezekana hayo marupurupu kila unapoyapata yafanye ndio akiba fungua account weka na hakikisha hutoi kwa namna yoyote ile.

Pia mkeo jitahidi apike hata maandazi atakusaidia majukumu mana anakuwa mjeuri wakati hana mchango wowote badala ya kukuonea huruma.Kama mtoto bado mdogo sana mwache akue kidogo halafu mpe mtaji auze hata genge au kupika mihogo hatokosa visent vyakumsupport nawe pia atakuwa amekupunguzia mzigo Mana vingine atatatua yeye bila kusubiri msaada wako.

Pia punguza matumizi yasiyo ya lazima wala kutaka kuishi kama fulani ilhali hali yako haifanani na wao.Kama ni mnywaji epuka kwenda baa na marafiki zaidi nunua zako mbili tatu nywea nyumbani.Punguza kuchangia sherehe mana sio kila sherehe lazima uchangia chagua zile muhimu sana tu.Matumizi ya nyumbani yalimit jitahidi kila ukipokea mshahara weka stock ndani ya vyakula na gas au mkaa na ukomae vitumike kwa usahihi sio wajinyime ile watumie wanachoeeza kumaliza hii itakusaidia katika kufanya saving.

Nahisi wanao pia wanasoma shule za kulipia hivo unajikuta una mzigo wa kulipa ada hapa wadau wengine watakupa solution.

Usikate tamaa mi naona wewe bado umri haujaenda sana kiasi Cha kupata stress hivo bado mapema anza sasa weka malengo na hakikisha unayaishi hayo malengo.
Mungu akutie nguvu na kukuvusha katika hali hii.
 
Kiukweli Dsm maisha yapo juu sana, kwa ukubwa wa familia uliyo nayo itakuchukua muda mrefu hata kujenga nyumba ya kuridhisha, zaidi utakuwa unamalizia fedha zote kwenye mahitaji ya watoto na chakula,

Omba uhamisho uende mikoani utafanikiwa kwa urahisi kuliko mahali ulipo.
 
Acha hizo, hivi nani anawapumbaza eti pombe inakwamisha maendeleo.
Mkuu sio kila mtu ana self control na pombe. Hujawahi kutana na mtu yeye kila anachokipata anapeleka kwenye pombe baada ya wiki mshahara wote amemalizia kwenye pombe? Kuna watu wa aina hiyo. Kama hauna self control pombe inakutoa kwenye msitari trust me
 
Pole Sana, Unapitia Changamoto Kubwa Sana
Jitahidi Ufanye Maisha Yako Wewe Mwenyewe Usijiringanishe Na Mwingine
Kazi Yako Naona Umeanza Mkopo NMB Haraka Sana
Unatakiwa Umudu Kutunza Cash Yako
 
Mkuu sio kila mtu ana self control na pombe. Hujawahi kutana na mtu yeye kila anachokipata anapeleka kwenye pombe baada ya wiki mshahara wote amemalizia kwenye pombe? Kuna watu wa aina hiyo. Kama hauna self control pombe inakutoa kwenye msitari trust me
Mkuu sasa hapo siyo pombe,
Tatizo ni la mtu mwenyewe pombe tuitoe kabisa kwenye hili.
 
Back
Top Bottom