Maisha yangu, ushuhuda wangu; Sijafika sijachoka usikate tamaa Mungu yupo.

mwakavuta

Member
Joined
Sep 22, 2020
Posts
99
Reaction score
306
Ni kawaida kwa watu kutafuta hamasa kutoka kwa waliofanikiwa peke yao kwa sababu tunaamini ndio wanaijua njia sahihi ya mafanikio. Binafsi sijafanikiwa kiwango cha kutoa hamasa hiyo kwa wengine lakini nina Imani kuna mtu aliyekata tamaa kabisa atapata nguvu ya kupambana kwa kujua kuwa hayupo peke yake kwenye haya mapambano Mungu ataleta neema yake siku za mbele asilale, karibu jitahidi kusoma uzi wote.

Binafsi niliamini kuwa kila kitu kitakuwa sawa baada ya kumaliza chuo kwamba nitapata kazi na kila mazuri niliyotamani yatakuja hasa kuiheshimisha familia yangu lakini hali imekua tofauti kila kukicha afadhali ya jana, nimetembeza sana vyeti hadi kuomba kazi ikageuka kazi yenyewe ubaya haina mshahara.

Kila mpango niliojaribu kufanya iwe biashara au wazo lolote hakuna linapofanikiwa mpaka rafiki zangu wakaanza kuniita Utopianist (wakimaanisha mtu mwenye mawazo ya ujamaa ambayo hayatekelezeki). Kila ninachogusa hakiendi ilifika wakati nikashindwa kabisa kulipa koda mwenye nyumba akanitimua kisiasa nikahamia uswahilini napo hakuna chochote kilichofanikiwa.

Niliamua kuweka pembeni fahari ya kuwa nimesoma nikaingia site za ujenzi hakuna chochote pesa haionekani, nimetapeliwa mpaka sikumbuki namdai nani na nani na ilikuwa kiasi gani. Baada ya hapo nikageukia kwenye kufunga scaffold (mabomba ya chuma yanayofungwa kama jukwaa la kufanyia kazi hasa nje kwenye magorofa) nikazoea umbali mrefu kuning`inia kama nyani lakini napo sijafanikiwa chochote nimetapeliwa sana, hadi nikatamani niende kwa mganga niue kabisa (Nimetubu nina Imani Mungu wangu amenisamehe), Lakini wapi hakuna chochote hali imekua ngumu nikasamehe nimerudi kuwalamba miguu walionitapeli mara kibao angalau nipate chochote.

Nilipata kazi ya kufundisha shule za mitaani (education centers) nikaacha mwenyewe baada ya kuona hakuna ninachopata pesa yote ilikuwa inaishia kwenye nauli wakati mwingine hata pesa ya kula nilikosa kabisa plus kuamka saa kumi asubuhi na kulala saa sita kila siku (kwa sababu ya umbali na wingi wa kazi).

Wakati napambana angalau angalau maisha yaende msichana wangu akapata mimba na kutokana na hali yangu akataka kutoa nikamkatalia kabisa nikiamini Mungu ataniona angalau mtoto azaliwe nitamlea hata kama ni kwa shida sikutaka kuua, (hii imeleta ugomvi baina yetu nina miezi mitatu sijawahi hata kumuona nabembeleleza kama namtongoza sasa) bado hajatoa ninaomba Mungu amuondolee hiyo roho ya kuua.

Mambo hayakaa sawa kodi ya chumba ikaisha sina kitu mwenye nyumba akataka kunifukuza kweli nilichanganyikiwa kuna wakati natembea machozi yanatoka yenyewe najizuia kulia hadharani hapa ndipo kiu ya bangi na sigara ilipokuja juu angalau usiku niweze kulala na kuamka na nguvu (nashukuru Mungu amenisaidia nimeacha vyote), kitu pekee ninachoendelea kuamini ni kwamba Mungu hana ubaguzi kila mtu ana zamu yake, ya kwangu itafika nijitahidi niendelee kua hai.

Baada ya kukwama sana niliamua kujilipua na kwenda ferry kutafuta kazi za uvuvi nikiwa sijui chochote wala simjui yeyote nilichohitaji ni kupata pesa ya halali, ukweli hata kuogelea sijui na sijawahi kupanda chombo chochote cha majini Zaidi ya pantone. Mungu alisaidia nikapata nafasi nikakesha baharini siku mbili mfululizo (sikupata hata mia ya faida Zaidi ya samaki wadogo sita nilirudi nikala na ugali). Baada ya hapo nikakosa hata nauli ya kwenda ferry kufanya kazi nitaanza kwenda tena Mungu akijalia uzima.

Nakumbuka sikumwambia mtu yeyote kua naenda kuvua samaki nilichofanya nilichukua kitambulisho changu nikakifunga kwenye nguo ili lolote likitokea watu wanitambue baadae hofu ikazidi nikamwambia dada yangu kwa sharti la kutosema kwa yeyote Mungu ananitunza kila leo kesho itakua njema.

Wakuu siongopi kuna wakati zinakata hadi wiki mbili chakula changu ni ugali mboga ni uji wa chumvi mambo yakikaa sawa ni uji sukari angalau nikiwa site ndio nakula kawaida sitaki kila mtu ajue tabu yangu. Nashukuru Mungu ameweka tabasamu kwenye uso wangu kila wakati si rahisi kujua hadi nikwambie. Mama yangu amekua mgonjwa kwa kazi ngumu hadi alilazwa nilichoweza kusaidia ni kulia tu nilikosa hata mia ya kumtumia, anajikaza anatoka kufanya kazi Mungu mwema anamtunza siku moja apate nafsi ya kula jasho langu ndicho ninachoomba kila siku.

Kuna wakati nawaza kuhusu mwanangu aliyeko tumboni ambaye sijui kama mama yake atabadilisha mawazo au vipi maumivu yanazidi najihisi kuhumiwa sana moyoni nitakuwa baba gani iwapo hiyo mimba ikitolewa ninayeruhusu mwanangu afe kwa sababu nimeshindwa kumudu maisha lakini kesho itafika Mungu ataachilia neema naendelea kuomba tu (kufunga siwezi vidonda vya tumbo vitaniua). Nikiongeza madeni niliyoshindwa kulipa nazidi kuchoka, niuze laptop yangu iliyochoka ambayo sitapata hata laki moja na haitamaliza shida akili inagoma au niifanye mtaji wa biashara naogopa nayo itakufa kama nyingine zilizopita kikubwa uzima tu. Nikifikiria kurudi nyumbani mkoani hali ni ngumu nachanganyikiwa kabisa ni bora niwe mbali nisiione hiyo hali nilijiapiza kufa nikitafuta pesa ya halali siwezi kufanya hila.

Nimejaribu kufupisha wakuu samahani kwa post ndefu Mtafutaji mwenzangu usichoke jipe moyo kazana Mungu hajatutupa wakati wetu utafika usiwaze kutajirika kwa dhuluma afya ndiyo zawadi kubwa kuliko zote Mungu aliyotupa, omba pambana Mungu atasaidia hakuna utajiri wenye Amani kama hautoki kwa Mungu na kama huwezi kuutumia kusaidia ndugu na jamii inayokuzunguka. Kwenye Biblia (nimesahau ilipoandikwa) Yesu alimwambia mtume Petro kuwa kuna wakati shetani atampepeta kama ngano lakini amemuombea ili Imani yake isiyumbishwe atakapokuwa imara awaimarishe wengine.

Kuna siku Mungu atafungua malango ya mbingu mvua itatunyeshea jiitahidi usije ukasahau kuwasadia wahitaji ndio njia pekee ya kurudisha shukrani kwa Mungu.

Inuka songa mbele kesho hatuifahamu kazi yako ni kuamini kuwa Mungu anakuwazia mema siku zote hawezi kukuacha hajakusahau anakujua wewe ni wa kwake na atakupa kwa wakati wake kuwa na uvumilivu. Jitahidi sana kutunza Amani ya moyo wako.

IMG_20211125_114048.jpg
 
Mkuu maisha unayopitia wewe ndyo tunayopitia wengi huku tukiamin ipo kesho pia

Mungu n mwema daima tusikate tamaa ipo siku isyona jina itatengeneza tabasamu usoni pako ukayasahau yote yakaraha na hapo ndipo ibada inatakiwe izidishwe ibada sio kuswal au kusali Bali ibada ya kwel n kuwasaidia wahitaji Kama wewe mda huu unavyowaza

Shujaa n yule anayefia vitani na siyo getoni kwake

Nakuombea mguu wa kesho utakapotoka nyumbam ukawe wa mafanikio na furaha zaidii

Amiiiiina

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Na wengi wakipata maisha umsahau Mungu
 
Maisha ya sasa yamemnyoosha kila mtu, yaani yanapiga mpaka afya ya mwili inatetereka unajikuta unapoteza hadi radha ya kuishi,

Weka aibu pembeni rudi nyumbani, huko Dar utajikuta unakuwa mwizi,

Afadhali kuishi kwenu kwa amani kuliko kukaa huko mbona masela kibao tumerudisha mpira kwa kipa tunajipanga kujilipua tena,

Rudi nyumbani
 
Mkuu maisha unayopitia wewe ndyo tunayopitia wengi huku tukiamin ipo kesho pia

Mungu n mwema daima tusikate tamaa ipo siku isyona jina itatengeneza tabasamu usoni pako ukayasahau yote yakaraha na hapo ndipo ibada inatakiwe izidishwe ibada sio kuswal au kusali Bali ibada ya kwel n kuwasaidia wahitaji Kama wewe mda huu unavyowaza

Shujaa n yule anayefia vitani na siyo getoni kwake

Nakuombea mguu wa kesho utakapotoka nyumbam ukawe wa mafanikio na furaha zaidii

Amiiiiina

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
amen mkuu asante sana.
 
Ni kawaida kwa watu kutafuta hamasa kutoka kwa waliofanikiwa peke yao kwa sababu tunaamini ndio wanaijua njia sahihi ya mafanikio. Binafsi sijafanikiwa kiwango cha kutoa hamasa hiyo kwa wengine lakini nina Imani kuna mtu aliyekata tamaa kabisa atapata nguvu ya kupambana kwa kujua kuwa hayupo peke yake kwenye haya mapambano Mungu ataleta neema yake siku za mbele asilale, karibu jitahidi kusoma uzi wote.

Binafsi niliamini kuwa kila kitu kitakuwa sawa baada ya kumaliza chuo kwamba nitapata kazi na kila mazuri niliyotamani yatakuja hasa kuiheshimisha familia yangu lakini hali imekua tofauti kila kukicha afadhali ya jana, nimetembeza sana vyeti hadi kuomba kazi ikageuka kazi yenyewe ubaya haina mshahara.

Kila mpango niliojaribu kufanya iwe biashara au wazo lolote hakuna linapofanikiwa mpaka rafiki zangu wakaanza kuniita Utopianist (wakimaanisha mtu mwenye mawazo ya ujamaa ambayo hayatekelezeki). Kila ninachogusa hakiendi ilifika wakati nikashindwa kabisa kulipa koda mwenye nyumba akanitimua kisiasa nikahamia uswahilini napo hakuna chochote kilichofanikiwa.

Niliamua kuweka pembeni fahari ya kuwa nimesoma nikaingia site za ujenzi hakuna chochote pesa haionekani, nimetapeliwa mpaka sikumbuki namdai nani na nani na ilikuwa kiasi gani. Baada ya hapo nikageukia kwenye kufunga scaffold (mabomba ya chuma yanayofungwa kama jukwaa la kufanyia kazi hasa nje kwenye magorofa) nikazoea umbali mrefu kuning`inia kama nyani lakini napo sijafanikiwa chochote nimetapeliwa sana, hadi nikatamani niende kwa mganga niue kabisa (Nimetubu nina Imani Mungu wangu amenisamehe), Lakini wapi hakuna chochote hali imekua ngumu nikasamehe nimerudi kuwalamba miguu walionitapeli mara kibao angalau nipate chochote.

Nilipata kazi ya kufundisha shule za mitaani (education centers) nikaacha mwenyewe baada ya kuona hakuna ninachopata pesa yote ilikuwa inaishia kwenye nauli wakati mwingine hata pesa ya kula nilikosa kabisa plus kuamka saa kumi asubuhi na kulala saa sita kila siku (kwa sababu ya umbali na wingi wa kazi).

Wakati napambana angalau angalau maisha yaende msichana wangu akapata mimba na kutokana na hali yangu akataka kutoa nikamkatalia kabisa nikiamini Mungu ataniona angalau mtoto azaliwe nitamlea hata kama ni kwa shida sikutaka kuua, (hii imeleta ugomvi baina yetu nina miezi mitatu sijawahi hata kumuona nabembeleleza kama namtongoza sasa) bado hajatoa ninaomba Mungu amuondolee hiyo roho ya kuua.

Mambo hayakaa sawa kodi ya chumba ikaisha sina kitu mwenye nyumba akataka kunifukuza kweli nilichanganyikiwa kuna wakati natembea machozi yanatoka yenyewe najizuia kulia hadharani hapa ndipo kiu ya bangi na sigara ilipokuja juu angalau usiku niweze kulala na kuamka na nguvu (nashukuru Mungu amenisaidia nimeacha vyote), kitu pekee ninachoendelea kuamini ni kwamba Mungu hana ubaguzi kila mtu ana zamu yake, ya kwangu itafika nijitahidi niendelee kua hai.

Baada ya kukwama sana niliamua kujilipua na kwenda ferry kutafuta kazi za uvuvi nikiwa sijui chochote wala simjui yeyote nilichohitaji ni kupata pesa ya halali, ukweli hata kuogelea sijui na sijawahi kupanda chombo chochote cha majini Zaidi ya pantone. Mungu alisaidia nikapata nafasi nikakesha baharini siku mbili mfululizo (sikupata hata mia ya faida Zaidi ya samaki wadogo sita nilirudi nikala na ugali). Baada ya hapo nikakosa hata nauli ya kwenda ferry kufanya kazi nitaanza kwenda tena Mungu akijalia uzima.

Nakumbuka sikumwambia mtu yeyote kua naenda kuvua samaki nilichofanya nilichukua kitambulisho changu nikakifunga kwenye nguo ili lolote likitokea watu wanitambue baadae hofu ikazidi nikamwambia dada yangu kwa sharti la kutosema kwa yeyote Mungu ananitunza kila leo kesho itakua njema.

Wakuu siongopi kuna wakati zinakata hadi wiki mbili chakula changu ni ugali mboga ni uji wa chumvi mambo yakikaa sawa ni uji sukari angalau nikiwa site ndio nakula kawaida sitaki kila mtu ajue tabu yangu. Nashukuru Mungu ameweka tabasamu kwenye uso wangu kila wakati si rahisi kujua hadi nikwambie. Mama yangu amekua mgonjwa kwa kazi ngumu hadi alilazwa nilichoweza kusaidia ni kulia tu nilikosa hata mia ya kumtumia, anajikaza anatoka kufanya kazi Mungu mwema anamtunza siku moja apate nafsi ya kula jasho langu ndicho ninachoomba kila siku.

Kuna wakati nawaza kuhusu mwanangu aliyeko tumboni ambaye sijui kama mama yake atabadilisha mawazo au vipi maumivu yanazidi najihisi kuhumiwa sana moyoni nitakuwa baba gani iwapo hiyo mimba ikitolewa ninayeruhusu mwanangu afe kwa sababu nimeshindwa kumudu maisha lakini kesho itafika Mungu ataachilia neema naendelea kuomba tu (kufunga siwezi vidonda vya tumbo vitaniua). Nikiongeza madeni niliyoshindwa kulipa nazidi kuchoka, niuze laptop yangu iliyochoka ambayo sitapata hata laki moja na haitamaliza shida akili inagoma au niifanye mtaji wa biashara naogopa nayo itakufa kama nyingine zilizopita kikubwa uzima tu. Nikifikiria kurudi nyumbani mkoani hali ni ngumu nachanganyikiwa kabisa ni bora niwe mbali nisiione hiyo hali nilijiapiza kufa nikitafuta pesa ya halali siwezi kufanya hila.

Nimejaribu kufupisha wakuu samahani kwa post ndefu Mtafutaji mwenzangu usichoke jipe moyo kazana Mungu hajatutupa wakati wetu utafika usiwaze kutajirika kwa dhuluma afya ndiyo zawadi kubwa kuliko zote Mungu aliyotupa, omba pambana Mungu atasaidia hakuna utajiri wenye Amani kama hautoki kwa Mungu na kama huwezi kuutumia kusaidia ndugu na jamii inayokuzunguka. Kwenye Biblia (nimesahau ilipoandikwa) Yesu alimwambia mtume Petro kuwa kuna wakati shetani atampepeta kama ngano lakini amemuombea ili Imani yake isiyumbishwe atakapokuwa imara awaimarishe wengine.

Kuna siku Mungu atafungua malango ya mbingu mvua itatunyeshea jiitahidi usije ukasahau kuwasadia wahitaji ndio njia pekee ya kurudisha shukrani kwa Mungu.

Inuka songa mbele kesho hatuifahamu kazi yako ni kuamini kuwa Mungu anakuwazia mema siku zote hawezi kukuacha hajakusahau anakujua wewe ni wa kwake na atakupa kwa wakati wake kuwa na uvumilivu. Jitahidi sana kutunza Amani ya moyo wako.

View attachment 2147147
Pole sana imani uliyonayo ndio mtaji wako. Hakika kesho njema yaja. Hatahivyo mambo yakigoma usiogope kurudi kijijini maana umeshakua na uelewa mpana na dhamira ya kujikwamua hivyo ukirudi hata kama utajishughisha na kilimo utakifanya kwa tija. Kwa juhudi uliyonayo naamini ukienda kulima msimu mmoja tu utapata kianzi. Yapo mazao yasiyokua na ghalama kubwa kumaintain na ni kilimo biashara kinacholipa mfano kwasasa mafuta ya alizeti yapo juu sana na ukilima alizeti kama eneo lina rutuba huhitaji mbole wewe ni palizi tu.
Hatahivyo kumbuka "wanaume tumeubwaaa mateeesooomatesao kuhangaika" TX moshi willium
 
Mungu kama yupo na nife hapa hapa muda huu
 
Huwezi fanikiwa lolote bila kwanza kutengeneza ulimwengu wako wa kiroho.
Funga kwa mda wa siku 3 au zaidi.
Unaweza ukafunga kwa masaa 24 kwa kufungua na maji tu, tumia ndimu, maji ya chumvi hai kwa kuoga na kunywa, tumia mmea wa kivumbasi kwa kuogea na kunywa, huku ukifanya toba na kujipatanisha na Mola wako, huku ukinua ukitamka vitu vizuri vije kwako. Hapa kama kuna uchawi au negative energy ulitupiwa zitapotea zote. Ruhusu positive power/energy zije kwako kwa kuzivuta. Saidia masikini mfano ombaomba wape hata shilingi 100 au zaidi kulingana na uwezavyo.
Fanya zoezi la kushukuru ulivyo jaliwa na Mola mfano afya, uzima, nk.
Ndani ya mwezi mmoja utaanza kuona milango ikifunguka.
 
Kivumbasi ndio nini?
 
keep hustling bro... tupo vitani tuna mengi ya kuandika lakini hatuna utulivu wa nafsi wa kutosha kuweza kutiririka vizuri ila vita ni kali sana...
wengine tulishasahau hata hawa viumbe wa kike tunawaona nuksi tu japo bado tunawahitaji
 
Yaani una smartphone .....

Una laptop

Unaweza kununua bando ...

Harafu unasema maisha yamekuchapa...

Acha kudanganya watu mkuu ,Wewe ni miongoni mwa matajiri hapa Tanzania....

Hujakutana na watu waliopinda...
 
Back
Top Bottom