Njia rahisi ya kuondokana na umasikini kwa mtu asiye na kipato.
Ardhi still bado ndio mtaji rahisi wa kutokea kimaisha.
Nje ya mji mapori tele yamejaa hata bure au kukodi unaweza pata safisha angalau si chini ya heka 10,panda mazao yasiyo na changamoto mfano kunde, alizeti, mtama, nk.
Chukua zao moja hili ni uhakika.
Baada ya kusafisha heka 10 au zaidi panda mmea wa nyonyo castro oil huu unavuna baada ya miezi 3 na utaendelea kuvuna kwa mda wa miaka 2.
Heka moja ya nyonyo utapata gunia 15 ukizikamua utapata lita 500 za mafuta, so heka 10 ni lita elf 5.
Jifunze kutengeneza sabuni za mche za mawingu
Lita moja ya mafuta utapata miche 2 mara lita elf 5 utapata miche elf 10.
Uza mche kwa sh 1500 mara elf 10 utapata milioni 15.
Jinsi ya kutengeneza mashine ya kukamua mbegu za mafuta tafuta bomba inchi nne tafuta Nondo mm 12 ikunje mfano wa spring ingiza ndani ya bomba mbele ya bomba ziba acha tundu dogo.Toboa toboa Bomba vitundu vidogo Ili mafuta yamwagike chini, weka mshikio wa kunyongea Ili ukamue mafuta.
Ukipata pesa kodi nyumba nenda viwandani kafunge bidhaa ambazo ni daily use kisha jaza kwenye nyumba uliyokodi kisha uwe tengeneza network na wauzaji wa dogo uwe unawasambazia bidhaa wanazoishiwa.
Kwa kufanya hivi ndani ya mwaka utakua mbali sana utaoa, utajenga, nk.