Maisha yangu, ushuhuda wangu; Sijafika sijachoka usikate tamaa Mungu yupo.

Mkuu pole sana

Si uende hapo kariakoo kutana na wakinga wenzio waambie ukweli watakupa hata kibarua chchote huku ukiendelea kusoma mchezo

Usijaribu kurudi kwenu mwakavuta utaishia kunywa ulanzi tu
Hahahah dadaq, mwakauta not mwakavuta ( mwakavuta ni shule ). ( Mwakauta ni Kijiji ).

Kule asirudi mamaq ,, Kuna ulanzi kama nini ....hahah

N b ...pambana huko huko uliko ...c hatuna msaada aisee
 

Mkuu kama unajua njia zote za kupita ili afanikiwe katika haya unayosema, mpe connection na pa kuanzia. Kwa hali aliyonayo pengine si tatizo la pesa au mawazo bali mtu wa kushika mkono katika hicho kidogo
 
Yaani una smartphone .....

Una laptop


Unaweza kununua bando ...

Harafu unasema maisha yamekuchapa...


Acha kudanganya watu mkuu ,Wewe ni miongoni mwa matajiri hapa Tanzania....

Hujakutana na watu waliopinda...
Hivi huwa mnajisikiaje kumtamkia mtu maneno ya kejeli anapotoa shida zake. Kesho ukisikia kajiua au kajidhuru utaweza kufuta haya maneno yako
 
I beg to differ. Never go back home. I insist, endelea kupambana. Mi mambo yaliniharibikiaga wakati nina familia ya watoto wawili. I lost all friends na hadi ndugu wengine walininanga... Wife hakua na kazi na tuliisha kwa neema ya Mungu tu huku familia yangu ikiwa ndo mfariji wangu pekee, watoto ndo walibaki marafiki zangu wa kunirudishia tabasamu na kusahau kwa muda ninayopitia. Imani yangu kwa Mungu ilisaidia sana na wife alisimama sana kwenye maombi. Nikahama chuga kwenda Dar kuhustle nikaacha familia kwa muda,huko ndo ikawa inapita siku mbili sijala chochote siku ya tatu ndo nakula..ukilala usiku unahisi huna hata nguvu kupump heart beats unaona zinapiga kwa slow motion. Mungu mwema hatimae mapito yakapita na haikua rahisi na haikua muda mfupi. Sembuse wewe single boy utashindwaje? Wenzio tumepitia hiyo hali tukiwa na familia...unapigwa mkwara na landlord hadi anaamua kujisahaulisha miez 8 hujalipa hata mia. Kikubwa muombe Mungu uzima tu...mengine atakubariki ni suala la muda tu. Nilishawahi pia comment kitambo sana kwenye ule uzi wa watu tuliowahi kufilisika.
Na nikuhakikishie kuna ninaowafaham walipitia changamoto zaidi hadi familia kusambaratika kabisa kila mtu na njia yake,wakakomaa hivyohivyo plus maumivu ya family kusambaratika na wakatoboa na ukikutana nao leo hutoamini waliyopitia
 
Mkuu kama unajua njia zote za kupita ili afanikiwe katika haya unayosema, mpe connection na pa kuanzia. Kwa hali aliyonayo pengine si tatizo la pesa au mawazo bali mtu wa kushika mkono katika hicho kidogo
Mafanikio yanaanza na mtu mwenyewe,pili mafanikio ni bahari hayana njia moja.
Tatu kwenye mitandao ndipo kuna majibu yote ya matatizo yote ya mwanadamu maana hadi sasa hakuna tatizo jipya duniani.Yote watu wameyashapitia na kuyatatua.
 
Mafanikio yanaanza na mtu mwenyewe,pili mafanikio ni bahari hayana njia moja.
Tatu kwenye mitandao ndipo kuna majibu yote ya matatizo yote ya mwanadamu maana hadi sasa hakuna tatizo jipya duniani.Yote watu wameyashapitia na kuyatatua.

Usiepuke wajibu wa kumsaidia mtu kama utaweza, mwisho wa siku hakuna aliyeweza kufanikiwa pasipo watu wa kumsaidia katika namna mbali mbali. Ukimsoma kijana kwenye kila mstari kaonesha nia na ari ya kufanya kazi ila kakwama. Anahitaji msaada wa karibu zaidi

Mungu amsaidie pengine kupitia humu atapata mtu sahihi inshaalaah
 
Hahahah dadaq, mwakauta not mwakavuta ( mwakavuta ni shule ). ( Mwakauta ni Kijiji ).

Kule asirudi mamaq ,, Kuna ulanzi kama nini ....hahah

N b ...pambana huko huko uliko ...c hatuna msaada aisee
Nakujua kule kama maji ya kunywa
 
Samahani mkuu, umeandika au umeandikiwa na mtu hapa?
 
Mleta mada nilichokipenda kwako una spirit ya kazi,huchagui kazi,una Imani na Mungu pamoja na magumu unayopitia bado una muona Mungu Kama hajakusahau Ila bado upo kwenye foleni,unangojea zamu yako...Mungu akukumbuke akukutanishe na watu Sahihi hata kupitia hapa
 
Yaani una smartphone .....

Una laptop


Unaweza kununua bando ...

Harafu unasema maisha yamekuchapa...


Acha kudanganya watu mkuu ,Wewe ni miongoni mwa matajiri hapa Tanzania....

Hujakutana na watu waliopinda...
Ila atleast kafikisha msg, kwa hali yako utaelewa alichosema. Kupitia shida haina maana huna smartphone au laptop. Mambo yakigoma yamegoma.
Issue hapa . Ni mapambano yaendelee mpaka siku hela itapotosha.
Kuna jamaa yangu alikua na smartphone, laptop, cheni ya Gold na pete mbili, na account NMB elfu 30 tu, na ni dalali, anaishi kwao, kula kulala bure. Akipata kidogo anafanya jambo hata nyumbani kwao, maisha yake kama ya jamaa, kila bishara inaisha. Akipata hela kidogo inaisha kwenye matumizi. Akampa mwanamke mimba, kila dili akipiga la udalali ndipo na mwanamke anashida, anatuma hela yote. Muda wa kujifungua umefika madili yamenuna haelewi kitu. Issue haikua kuuza vitu. Ila alipambana, akafanikiwa kuweka kila kitu sawa. Mtoto alizaliwa kwenye neema, arobaini na ubatizo wa kutisha. Jamaa saiv anaishi kwake, gari yake, dada yule na watoto wa wawili wa kike. Na sasa ana cheni kubwa zaidi ya Gold. Na pete kaongeza design nne tofauti. True story.
ISSUE NI KUPAMBANA, HAKUNA KULIA. IPO SIKU.
 
asante sana mkuu
 
asante sana mkuu kwa ushauri, binafsi sijisifu lakini najitahidi kutoa kadri ya uwezo wangu sijawahi kuombwa msaada na mtu yeyote nikaacha kumsaidia kama nina uwezo, nitajitahidi sana kuongeza
 
Nusoma uzi huku nikila mchicha na muhogo wa kuchoma


Point kubwa
Unatkiwa kuhakikisha hufi kizembe
kweli mkuu mapambano yanaendelea najua wapo wenye changamoto kunizidi, ninaamini kuna mtu aliyekaribia kukata tamaa kwa kusoma huu uzi atasonga. tutatoboa mungu mwema.
 
asante mkuu nilishaamua kutorudi nyumbani nakomaa hadi kieleweke as long as Mungu ananipa afya kila siku, ipo siku kila kitu kitakua sawa.
 
Yaani una smartphone .....

Una laptop


Unaweza kununua bando ...

Harafu unasema maisha yamekuchapa...


Acha kudanganya watu mkuu ,Wewe ni miongoni mwa matajiri hapa Tanzania....

Hujakutana na watu waliopinda...
hahaha! mkuu hii laptop yangu hata kwa laki moja hununui imechoka sio kitoto natumia kiswaswadu sio smartphone, angalau napunguza mawazo na kujifunza kupitia hii laptop nzee, Binafsi najiona napunguza mzigo mkubwa sana na kujifunza mengi ninapoingia JF nikipata nafasi. Pia inawezekana nina mtazamo mbaya mimi sio muumini wa kuuza vitu angalau nafarijika kuona vitu vichache nilivyo navyo. what if nikiuza vyote na matatizo yasiishe nitakua nimeongeza tatizo.
 
Ingia mafinga hapo kuna viwanda vya wachina kibao kwa siku buku 5...sasa sijui mke wako utamchukuaje....maaana ungekiwa alone atleast ungekuwa na 50ty...ungesonga
 
Nakuombea mwamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…