Maisha yangu ya ndoa ni tofauti na nilivyoyatarajia

Maisha yangu ya ndoa ni tofauti na nilivyoyatarajia

Unapata pressure na msongo wa mawazo kwa ajili ya nini?

Binafsi naona kama unafake life mkuu. Ishi uhalisia wako na mkae chini na mkeo muelekezane muishi lwa kulingana na kipato chenu. Kwa umri wangu wa kuishi ndoani kwa miaka 25 sasa nimejifunza mwanaume ndiye anayeamua ndoa na nyumba yake iwaje.
 
Unapata pressure na msongo wa mawazo kwa ajili ya nini?

Binafsi naona kama unafake life mkuu. Ishi uhalisia wako na mkae chini na mkeo muelekezane muishi lwa kulingana na kipato chenu. Kwa umri wangu wa kuishi ndoani kwa miaka 25 sasa nimejifunza mwanaume ndiye anayeamua ndoa na nyumba yake iwaje.
Nyumba ipi
Ya mileleleeee??
 
Mke hakujua una kipato kidogo kabla ya ndoa? Ama wewe ni ile aina ya mwanaume uliyefanya una hela wakati wa uchumba ukaja kuonesha rangi yako ukiwa ndani ya ndoa?

Lakini kivyovyote vile,kama alikupenda kweli kipato kidogo haikutakiwa kuwa sababu ya migogoro hadi kufanya presha kupanda
Kama hakukupenda...pole sana
Shida ni kwamba vigezo vya msingi katika kuoa tunaviepuka tunafuata chura la mwanamke. Matokeo yake ndio tunaoa wanawake hawana akili hata ya kujiongoza wao wenyewe achilia mbali kuongoza watoto.
 
Mbona me Nina furah sana na ndoa yangu na Sina hela kihivyo.

Ukipata hela jaza vyakula achana na mambo mengine jaza unga Michele mafuta sukari sabuni maharage na dagaa halafu muachie wife kama laki moja tu inamtosha...fugafuga na vikuku
Mkuu; Sentensi ya mwanzo 👆 👆 (ya kwanza) umetupiga kamba. Haijawahi na haitokaa hali kama hiyo kuwepo hapa duniani. Never. Kwa nini nasema hivyo?
Jibu lake ni hili hapa: Ndoani mnaishi watu 2 tofauti na wa jinsia tofauti. Mmekutana ukubwani ambapo kila mmoja alikwisha kuwa na mtizamo au mwelekeo wake na mapito tofauti kivyake. Kwa mantiki hiyo wanandoa wanaishi katika Utofauti wao. Kumbuka na zingatia kwamba mwanamke kuishi na mwanaume sio eti kwamba amevikosa hivyo ulivyoorodhesha hapo eti.."Ukipata hela jaza vyakula achana na mambo mengine jaza unga Michele mafuta sukari sabuni maharage na dagaa halafu muachie wife kama laki moja tu inamtosha...fugafuga na vikuku" wewe kwa kufanya hivyo unaiita presha na sonona kali tena leo-leo.
Mbona hata (Ke) wenyewe wanasema: " hivo vitu, mali na hela zako usitubabaishe navyo, hata kwetu vipo tena zaidi ya hivo vya kwako vya kuokoteza..........Sikuja hapa kwa ajili hiyo".
Tumeambiwa "tuishi nao kwa akili" usidhani aliyesema hayo alikuwa mjinga(Hajui).
 
Mke hakujua una kipato kidogo kabla ya ndoa? Ama wewe ni ile aina ya mwanaume uliyefanya una hela wakati wa uchumba ukaja kuonesha rangi yako ukiwa ndani ya ndoa?

Lakini kivyovyote vile,kama alikupenda kweli kipato kidogo haikutakiwa kuwa sababu ya migogoro hadi kufanya presha kupanda
Kama hakukupenda...pole sana
Hao viumbe wakitaka hela wanajua ipo tu na kama haipo ni kama watoto utatupiwa lawama zote zilizo chini ya jua
 
Nimegundua kwamba changamoto za ndoa zinaweza kukuletea presha kubwa, hasa unapokuwa na kipato cha chini.
Nimeishia kusoma hapo kwenye BOLD na kugundua utafiti wako bado haujakamilika. Sikuwa na haja ya kusoma taarifa yote ya utafiti wako. Endelea kufanya utafiti pia uongeze sampuli inayojumuisha wenye ndoa lakini pia ni matajiri. Usiishie kwa wenye pesa Tanzania bali pia matajiri wakubwa wa dunia kama Elon Musk, Jeff Bezos nk.

Ukimaliza rudia kuandika taarifa ya utafiti wako ukianza na marekebisho ya hapo nilipopabold.

Ndoa ni kamali, unaweza kuliwa au ukala. Ukaifurahia au ikakuondolea furaha uliyokuwa nayo kabla ya ndoa achana na uliyoitamani kuipata baada ya ndoa.
 
dogo acha uchawi wako nimekuandikia WhatsApp hujajibu sms yangu umeniblock kabisa na umeniblock messenger
Acheni Tabia za kuendekeza ushirikina Naomba tu udongo ambao umekuja kuchukuwa maeneo ya home urudishe Kabla sijakuitia watu
Nimekuandikia DM uku JM hutaki kujibu sms yangu
Umechanganyikiwa wewe..
 
Nyumba ipi
Ya mileleleeee??
"Nyumba" sio ule muundo mbinu unaotengenezwa kwa tofali, miti, bati n.k. halafu binadamu anakaa/anaishi au anajisitiri humo. La hasha. Ni zaidi ya hayo.
Nyumba ni jumla ya mazingira, mtindo wa maisha (life style), matumizi (expenses), uwezeshaji (facilitation) na Imani(Norms)yenu ili maisha yawezekane na yawe ni endelevu. (Imani hapa sio dini e.g. Je, unaamini kwamba mkeo/mumeo sio mwizi ? sio mchawi? anasema ukweli kwako siku zote? n.k.)
Nyumba ya milele ni haki ya kila mtu hapa duniani na huwa hanyimwi mtu. Mbona ni ya size ndogo tuu.
 
Kabla ya kuoa, nilidhani ndoa ni chanzo cha furaha na baraka. Nilitarajia amani na utulivu, lakini ukweli umekuwa tofauti kabisa. Nimegundua kwamba changamoto za ndoa zinaweza kukuletea presha kubwa, hasa unapokuwa na kipato cha chini.

Kipato kidogo kimekuwa chanzo cha migogoro isiyoisha. Mahitaji ya nyumbani ni mengi, na mara nyingi mapato hayatoshi. Matokeo yake ni msongo wa mawazo, mabishano, na lawama zisizo na kikomo. Nilipokuwa peke yangu, nilikuwa na uwezo wa kujipanga na kufurahia maisha kwa kipato kidogo. Lakini sasa, inaonekana kama haitoshi hata kwa mahitaji ya msingi

Zaidi ya hayo, nilitarajia mke kuja na upendo, ushirikiano, na msaada. Badala yake, nimejikuta kwenye presha ya kukidhi matarajio ambayo ni vigumu kuyafikia kutokana na hali ya uchumi. Wanawake wengi wanatarajia waume zao wawape kila kitu bila kujali hali halisi ya kipato. Hili limeongeza msongo wa mawazo na kunifanya nipoteze amani ya moyo na hata afya yangu imeanza kudorora.

Kabla ya ndoa, nilikuwa na uzito wa kilo 68 na presha yangu ilikuwa 120/80. Sasa, uzito umeshuka hadi kilo 59 na presha imepanda hadi 130/81. Hii yote ni kutokana na presha ya maisha ya ndoa na kutokuwa na amani ya akili.

Nimejifunza kuwa kuoa kwa kutegemea kwamba mwanamke ataleta baraka au neema ni kujidanganya. Badala ya baraka, nimekutana na changamoto na presha zisizo na mwisho. Ni wazi kwamba bila kipato cha kutosha na ushirikiano wa kweli katika ndoa, maisha yanakuwa magumu sana.

Ndoa inahitaji zaidi ya upendo; inahitaji uvumilivu, ushirikiano, na uelewa wa hali halisi ya maisha. Bila haya, ni rahisi kugeuka kuwa chanzo cha laana badala ya baraka.
Hukuchagua vizuri
 
Shida ni kwamba vigezo vya msingi katika kuoa tunaviepuka tunafuata chura la mwanamke. Matokeo yake ndio tunaoa wanawake hawana akili hata ya kujiongoza wao wenyewe achilia mbali kuongoza watoto.
Ewaaaa!

Mkuu, wewe ndiye umeandika cha maana.

Wengi wetu vigezo vya msingi katika kuoa tunaviepuka na ndiyo maana malalamiko yamekuwa mengi sana.

Watu wanaangalia uzuri wa mwanamke au pengine wanajipa moyo kuwa atabadilika akiwa ndani ya ndoa na matokeo yake yanakuwa ni kilio.
 
Back
Top Bottom